Wenye Viwanda vya Sukari, Mshukuruni na kumuombea Mh.Magufuli

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Kwa wenye viwanda vya sukari mnakumbuka MLIVYOPUUZWA na Serikali ya awamu ya nne kila mlipotoa kilio chenu kuhusu sukari inayoagizwa kutoka nje na inavyouwa soko la ndani kwa kuuzwa kwa bei ya chee kwa kutolipa ushuru wa Serikali na ninyi kukosa mahali pa kuuza.

Leo Mhe. Magufuli amepiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje. Kwa uamuzi huu wa busara kabisa wa Mhe.Rais Magufuli mnatakiwa MUMSHUKURU na KUMUOMBEA kwa kitendo hiki.

Nawashauri muwateue wajumbe wachache miongoni mwenu muende Ikulu ili kumshukuru Mhe. Rais.
 
Kwa wenye viwanda vya sukari mnakumbuka MLIVYOPUUZWA na Serikali ya awamu ya nne kila mlipotoa kilio chenu kuhusu sukari inayoagizwa kutoka nje na inavyouwa soko la ndani kwa kuuzwa kwa bei ya chee kwa kutolipa ushuru wa Serikali na ninyi kukosa mahali pa kuuza. Leo Mhe. Magufuli amepiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje. Kwa uamuzi huu wa busara kabisa wa Mhe.Rais Magufuli mnatakiwa MUMSHUKURU na KUMUOMBEA kwa kitendo hiki. Nawashauri muwateue wajumbe wachache miongoni mwenu muende Ikulu ili kumshukuru Mhe. Rais.
Kwakweli serikali iliyopita ilikua sio serikali bali nyonya damu.
 
Mapema sana wakuu tujifunze kukosoa pia hili sio sahh ktk medani ya soko huria na cc tukiambiwa tusiuze pamba na tumbaku nje hawa wakulima wetu mtawapa nn??
 
Shukrani pekee ni kukidhi soko la ndani na sukari iuzwe bei ya kawaida.
 
Mapema sana wakuu tujifunze kukosoa pia hili sio sahh ktk medani ya soko huria na cc tukiambiwa tusiuze pamba na tumbaku nje hawa wakulima wetu mtawapa nn??
mkuu badala ya kuwaza viwanda vya nguo vijengwe ili wakulima wetu wauze pamba humo bado unawaza kupeleka pamba njee tu... ??

ishu ya sukari ulikuwa mradi wa wafanyabiashara wachache. ngoja nikudokolee kidogo.

Sukari ikitoka kiwandani inapewa distributors na hawa ndo walikuwa wanasababisha bei ya sukari inapanda kwa kuirundika kwenye maghala yao, moja wa hawa distributors ni kijana "bilionea" Africa. cha kushangaza zaid huyu huyu distributor alikuwa amelobby na kupata kibali cha kuagiza sukari nje kwa bei ya chini na kwa magendo magendo... hii ilimnufaisha huyu distributor na watu wachache serikalini sana. maana hawakuwa wakisambaza sukari inayotoka viwandani bali wanayotoa nje. hii ilipelekea maelfu ya wakulima wa miwa kukosa hata hela ya kununulia sukari au kupeleka watoto wao shule maana viwanda vingi vilipunguza au kuaha kabisa uzalishaji wa sukari maana hakukuwa na soko.

sasa kwa hali hiyo bora lipi? kuwanufaisha wakulima maelfu au kuendeleza cartel la wahujumu uchumi wanaoingiza sukari kwa njia za magendo.

nampongeza sana Magufuli kwa kufumua cartels za hawa wahujumu uchumi.
 
Tatizo wafanyabiashara wetu wanakuaga wajinga..mnakumbuka kipindi cha nyuma walifungia sukari yao kwenye maghala hawataki kuuza wanasubiri iadimike waongeze bei? Magufuli anavyoamua awe na dawa pia ya kuwafanya hawa wajinga wote wanaohujumu wananchi kwa kufungia sukari kwenye maghala...vinginevyo atakua hajui nini anachokifanya...besides sidhani hata kama anajua uwezo wa hivi viwanda kuzalisha kukidhi mahitaji ya ndani
 
Bidhaa inazalishwa hapa nchini inakuwa na bei juu kushinda inayoingizwa kutoka nchi za nje...Nadhani kweli tutaisoma namba ghafla utasikia kg 1 ya sukari inauzwa kwa 5000...Na sisi tunakenua kenua tu.
 
Zakutoka nje zingekuaje ghali wakati hazilipiwi kodi? Unadhani zingelipiwa kodi zingekua bei ya ChinI?
 
Zakutoka nje zingekuaje ghali wakati hazilipiwi kodi? Unadhani zingelipiwa kodi zingekua bei ya ChinI?

Hata Kama zikilipiwa kodi, bado bei yake inakuwa chini kuliko hii ya ndani. Tujiandae kununua sukari elfu tano kilo
 
Tatizo wafanyabiashara wetu wanakuaga wajinga..mnakumbuka kipindi cha nyuma walifungia sukari yao kwenye maghala hawataki kuuza wanasubiri iadimike waongeze bei? Magufuli anavyoamua awe na dawa pia ya kuwafanya hawa wajinga wote wanaohujumu wananchi kwa kufungia sukari kwenye maghala...vinginevyo atakua hajui nini anachokifanya...besides sidhani hata kama anajua uwezo wa hivi viwanda kuzalisha kukidhi mahitaji ya ndani

Kuna kitu muhimu cha kuangalia. Viwanda hivi huenda vikalemaa kwa 'kudekezwa' na kutokutaka 'kujiongeza' kwa kutumia mwanya huu waliopewa. Wakatumia teknolojia na maarifa yale yale ya kizamani pasi kujua hii ni fursa pekee ya kujiongeza ili kuongeza tija.
Hawa wazalishaji wetu wa sukari katika kipindi hiki watataka kupata faida kwa kuwanyonya wakulima wa miwa na walaji kwa kujineemesha na hii hati milki ya soko la sukari. Wakajisahau na kujua fursa hii itadumu daima dawamu.
Cha umuhimu ni vyema kukawa na kipindi maalumu cha kuwaangalia hawa wazalishaji wetu. Katika kipindi hiki wawe wanakaguliwa na kutizama maendeleo wanaliofanya, hatua za kifanisi na tija iliyopatikana. Tusije kuanza kulaumiana na kuwaacha "wajanja" wakitucheka na kutuona mabwege na kusema tulikurupuka na hatukufanya utafiti wa kutosha katika maamuzi.
 
Back
Top Bottom