Waziri wa Fedha na Mipango; Ushauri wangu kuhusu suala la sukari sokoni

Fahami Matsawili

Senior Member
Mar 8, 2018
172
153
Mhe Waziri wa Fedha na Mipango Dr Philipo Mpango. Pole na Kazi Kiongozi wangu. Nina Ushauri kwa serikali yangu kupitia kwako kama waziri mwenye dhamana ya wizara ya fedha na Mipango. Kuna Suala la Sukari ukiachia kiasi kidogo kilichoagizwa nje ili kuziba gape iliyokuwa inapungua ndani ya nchi na serikali yetu kutoa Bei elekezi kila Mkoa ya sukari...

Kuna huu Utaratibu wa Muda mrefu wa Viwanda vya Sukari kutumia mfumo wa kuuza sukari kupitia Agent mmoja kila eneo hii suala lina changamoto kadhaa kwa wananchi wetu.

1. Moja kupitia Agent mmoja serikali inashindwa kuratibu kufuatilia wafanyabiashara wakubwa (Wholesaler) na wafanyabiashara wadogo (retailers) ambao wananunua sukari kwa hao wakubwa kupitia mwanya huu sukari ya ndani inaweza kufichwa Sokoni na wafanyabiashara wadogo au wakubwa kwa lengo la kusubilia bei ipande sokoni ndio waitoe hivyo sukari iliyoagizwa kutoka nje kufidia gape iliyokuwepo ndani ya nchi inaweza isionekane kuzaa matunda kama serikali yetu ilivyokusudia kwa nia njema.

2. Kwenye Uchumi wa viwanda kupitia viwanda tunategemea serikali yetu ikusanye kodi, viwanda pia vizalishe ajira kwa Wananchi wetu na mwisho Wananchi wanaozunguka viwanda wanufaike na upungufu wa bei ya bidhaa kutokana na ukaribu wa Viwanda hivyo kwa wananchi walio karibu na Viwanda hivyo.

Mfano Dar es salaam mfuko mmoja wa saruji ni Shilingi 13000 lakini Kagera unafika hadi shilingi 25000 kutokana na gharama za Usafirishaji jambo ambalo halipingiki pamoja na Jitihada za Rais wetu John Pombe Magufuli za kujenga miundombinu ya Reli na meli ili kupunguza gharama kubwa ya usafishaji na kupelekea bei kuwa kubwa kwa wananchi ili wapate bidhaa kwa bei nafuu...

Mfano Mkoa wa kagera tuna kiwanda cha Sukari, Kagera Sugar cha ajabu mwananchi aliye karibu na kiwanda kilometers 5 kutoka kwenye kiwanda ananunua kilo moja ya sukari sawa au zaidi ya bei na mwananchi aliyepo kilometers 800 kutoka kwenye kiwanda cha Sukari Kagera sugar.

Ushauri wangu tunapoelekea kwenye bajeti yetu 2020/2021 serikali yetu ichukue hatua zifuatazo ili kuzibiti hili suala pamoja na Jitihada njema za serikali yetu za kuchochea uzalishaji wa sukari kwa viwanda mbalimbali vya Sukari nchini.

1. Serikali ivisimamie na kuvielekeza viwanda vya Sukari kufungua center of sales kila mkoa husika na wafanyabiashara Wakubwa (Wholesaler) wenye uwezo wa kununua kuanzia Tani 1 na kuendelea waruhusiwe wanunue kwenye center hizo na kupeleka kwenye maduka yao ambayo wafanyabiashara wadogo (retailers) wataweza kununua kwa urahisi kama ambavyo makampuni ya vinywaji vya pombe yanafanya kwa kuwa na centers of sales badala ya kutegemea mtu mmoja (Agent) mfumo wa kizamani huu.

Utaratibu huu mhe Waziri wa Fedha Dr Philipo Mpango utakuwa na faida zifuatazo ambazo zinajibu changamoto nilizozianisha hapo juu.

1. Serikali yetu itakuwa rahisi kumonitor sekta ya sukari ili kuondoa ukiritimba wa kuficha sukari kwa wafanyabiashara wa hovyo wanaficha sukari..

2. Itakuwa rahisi kwa serikali ndani ya mkoa kuwatambua wafanyabiashara wakubwa (Wholesaler) kupitia database kuhusu mzunguko wao wa biashara ya sukari lini waliingiza sukari mpya lini sukari imetoka kwenda kwa wafanyabiashara wadogo (retailers).

3. Wananchi wanaozunguka viwanda hivi watapata sukari kwa bei kulingana na Umbali wao na kiwanda cha kuzalisha sukari kama serikali ilivyotumia kanuni bei ya elekezi kutoka umbali wa kutoka dar es salaam hadi kwenye mikoa husika na kutoa bei elekezi kwa sukari iliyoagizwa kutoka nje ya nchi kuziba gape iliyokuwa inapungua kwenye sukari yetu inayozalishwa nchini na Viwanda vyetu.

Mhe Waziri wa Fedha nina imani ushauri wangu utazingatiwa kwa ajili ya mama Tanzania.

Fahami Matsawili.
Mjumbe wa baraza kuu uvccm Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini bia hazijawahi kupungua mtaani,
Hawa wauza sukari si wafuate modeli ya Bia,mji mmoja agents hata 30 wa bia za kiwanda hicho hicho
 
Tatizo la msingi wa nchi hii ni administration ya serikali na si vyama vya siasa kwa sana.

Unapokuwa technocrat halafu unafuata matakwa ya wanasiasa kwa matamko bila ya strategic plan this is bound to happen.

Issue hapo ni capacity planning, inventory control in relation to seasonal variation na kuelewa lead time.

Kwa kifupi tutapiga makelele CCM sijui, ooh CDM vile; isipokuwa bila ya kufanya proper succession planning ya vigogo wizarani na taasisi za serikari kwa watu wanaopewa nafasi zinazohitaji high technical reasoning Tanzania maendeleo ya haraka haraka tutayasikia bombani.

2025 anahitajika mtu wa kuja ku change how civil service works kumejaa vilaza wenye Phd fake.
 
Hapo kwenye sukari, tuache siasa, hili ni jipu sugu na linatesa wapiga Kura na hasira Yao wataijua kwenye sanduku la Kura, waache watudharau
 
Hivi hiyo sukari imeagizwa kutoka nchi gani bado haijafika tu, kuna kipindi sukari kutoka Zanzibar ilizuiliwa kuuzwa bara nafikiri ni muda mwafaka kuiruhusu maana hali ni mbaya, jana nimenunua kwa 3800/kg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom