WENYE UZOEFU NIMEITWA KWENYE USAHILI

Habari zenu ndugu zangu jamani nisaidieni Abc namna ya maswali yanavyokuwa, technic, na jinsi yakujibu

Nafasi:Mtendaji wa kijiji daraja la III

Sent from my SM-G781U1 using JamiiForums mobile app
Soma kuhusu majukumu ya Mtendaji

Soma kuhusu namna ya kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza katika eneo unalofanyia kazi baina yako na wananchi. Au wananchi na wananchi.

Soma kuhusu matumizi ya tehama kazini.

Tuliza temper mtangulize MUNGU na umshukuru ukimaliza usikose leta mrejesho.
 
Ni maswali ya uwelewa tu

Ila hakikisha unafahamu current issues zinazotokea katika NCHI

Kingine kumbuka kwenye mtihani wa written una lisaa limoja tu

Pia kumbuka kwenye written Wana sahihisha points na sio maelezo maama wasailiwa mpo wengi ivo usije ukapoteza muda kwa kueleza sana ukajikuta umejibu maswali matatu kati ya matano
 
Fahamu yafuatayo:

1. Ngazi za utawala, kuanzia ngazi ya kijiji mpaka juu (Halmashauri, DED).

2. Majukumu yako kama mtendaji wa kijiji (Siku hizi hakuna Afisa mtendaji - Iliondolewa).

3. Fahamu muundo na tofauti kati ya Halmashauri ya kijiji na Serikali ya kijiji.

4. Utawasaidia vipi wananchi:-

  • Kutatua changamoto katika jamii
  • Kuweka mazingira rafiki/ wezeshi kwa wawekezaji kijijini.
  • Kutokusababisha migogoro na kutatua migogoro katika jamii.
  • Kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ya kijiji.

5. Majukumu yako kwa ujumla
6. Unaweza kuulizwa swali la kizushi, unawajibika vipi kwa mwenyekiti wa kijiji na diwani ndani ya kata yako?
 
Moja ya nafasi ya chini kabisa ya kiutendaji basi ni kuwa mtendaji wa kijiji, wewe boss wako ni mwenyekiti wa kijiji yani can you imagine mwenyekiti wa kijiji anakuwa mkubwa wako

Yani wewe hata viongozi wa vitongoji wote na mitaa yote wanakukoromea maana wao ni wanasiasa wewe kabwera tu wa mkurugenzi yani duuuh!!!
 
Habari zenu ndugu zangu jamani nisaidieni Abc namna ya maswali yanavyokuwa, technic, na jinsi yakujibu

Nafasi:Mtendaji wa kijiji daraja la III

Sent from my SM-G781U1 using JamiiForums mobile app
Mkuu kikubwa nikutakie kila la heri. Jipange, jiamini, vaa vizuri.

Binafsi sina cha kukusaidia kwa sababu sina chochote nachojua juu ya hiyo kada.
 
Mbali nakujiamini usijisahau ukavaa jeans utaua bendi,piga zile pigo za mkanda nje na chini tia choma moyo,Good luck mkuu this is yours.
 
Soma kuhusu majukumu ya Mtendaji

Soma kuhusu namna ya kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza katika eneo unalofanyia kazi baina yako na wananchi. Au wananchi na wananchi.

Soma kuhusu matumizi ya tehama kazini.

Tuliza temper mtangulize MUNGU na umshukuru ukimaliza usikose leta mrejesho.
Ahsante sana kaka

Sent from my SM-G781U1 using JamiiForums mobile app
 
Soma kuhusu majukumu ya Mtendaji

Soma kuhusu namna ya kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza katika eneo unalofanyia kazi baina yako na wananchi. Au wananchi na wananchi.

Soma kuhusu matumizi ya tehama kazini.

Tuliza temper mtangulize MUNGU na umshukuru ukimaliza usikose leta mrejesho.
Sawa sawa kaka

Sent from my SM-G781U1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom