Wenye upendo wa dhati please karibuni, 2016 ni wetu.

mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
2,162
3,086
Jinsi gani mtu unayempenda sana anaweza kuwa malaika au shetani, mzuri sana au mbaya sana kwako! mtu ambaye anaweza kukupa kiwango cha furaha ambacho haujawahi kukihisi ndiye mwenye uwezo wa kukutengenezea maumivu ambayo haujawahi kuyahisi pia. Kwa sababu hisia zako zinamtegemea yeye, na yeye anafuata hisia zake, kuna muda unaweza ukahisi umeachwa uchi kabisa. Unaweza ukajichukia mwenyewe Kwa kushindwa kuweza kuishi nje ya uwepo wake, lakini utafanya nini na hisia zako zinamtegemea? Na kama utamwomba Mungu basi utamwomba ampe yeye moyo wa kukuthamini na sio wewe ujasili wa kuachana naye, Kwa sababu umeuaminisha moyo wako ya kuwa "YEYE PEKEE NDIYE ATAYEKUFAA" bye bye #2015. Please #2016 be fair Kwa kwenye upendo wa dhati, they need to be loved back. #MyOpinion.
 
Back
Top Bottom