Wenye nursery hamuwasaidii watoto wetu bali mnawaongopea wazazi na walezi wa watoto

fizo talent

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
2,257
3,882
Habari wanabody,
Km heading ilivyotangulia baadhi ya shule za awali maaruf kwa jina la nursery zimekua zikifanya ulaghai kwa watoto na wazazi na sina uhakika km anaepanga tatizo ni mmiliki wa kituo ama walimu wanaotoa huduma.
Tatizo la msingi ambalo nimelifanyia research kwa eneo ninalotoka ni matokeo ya hawa watoto baada ya kuwafanyia mtihani.Uchunguzi wangu mdogo niliofanya unaonesha kwa nursery hususani hizi za mtaani km nursery ina wanafunz takribani 30 Bas kwenye majibu huwezi kukutana na mwanafunz aliyeshika nafasi 30 ktk
watoto 30.Uchunguzi wangu umeonesha km kituo kina watoto 30 bas watabalance wajuavyo wao na mtoto wa mwisho atashika nafasi ya 10 ktk watoto 30.Lengo la kufanya hivi ni kumhadaa mzazi kwamba mtoto wake anafanya ili aendelee kudumu ktk kituo chake maana mzazi hupata faraja akiona mwanae anafanya vizuri,na ukizingatia siku hizi watoto wanaanza nursery mapema tu kuanzia miaka mitatu hivyo mpaka akianza la kwanza kituo kinakua kishapiga hela ya kutosha tu.
Wazazi na walezi tuwe makini kuwafatilia watoto wetu na nursery tunazowapeleka ili kuepuka kujiuliza maswali mtoto akianza la kwanza mbona watu wanamburuza na shule zenyewe za elim bure unaweza kuta mwanao kashika nafasi ya 160 ktk watoto 250 kumbe tatizo lilianzia ktk nursery walimu walishindwa kujua njia mbadala za kumsaidia mwanao.
 
Upimaji wa nursery na primary tofauti, mara nying nursery mitihani yao ni kuandika herufi au kutaja majina ya vitu hivyo rahisi Kwa mtoto kufanya vizuri.
 
kazi kuwaandikisha notes tu, hao hata awali hawajafika, wanapelekwa kule waweze kutenda vitu rahisi vinavowahusu, sio kuandika, hata mikono yao haikakomaa kushika penseli.
 
Upimaji wa nursery na primary tofauti, mara nying nursery mitihani yao ni kuandika herufi au kutaja majina ya vitu hivyo rahisi Kwa mtoto kufanya vizuri.
Ila yote ni kumrahisishia mwanafunz akianza la kwanza awe vizuri ila wapi chenga tupu
 
Back
Top Bottom