Wenye ndoto za kwenda state pitia hapa

Acheni kukatisha watu tamaa. siyo kila mtu aliyeko Ulaya anabeba mabox au anafanya kazi za kuzoa takataka. Yes hata hizo ni kazi. lakini si kwamba kila mtu anafanya hizo. Kuna watu wamefanikiwa sana huko huko Ulaya. Mbona hakuwaonyesha? kuna madaktari pia, kuna mainjinia nk. leo naibu waziri wa fedha wa US ni kijana mwenye asili ya Naijeria. Si kwamba kila mtu atakuwa waziri au meneja, lakini wapo! hivyo vijana hawana budi kupambana.

Hoja ni kwamba hata Tanzania kuna akina Mo na wenzake wanaokula keki ya taifa..kuna akina Msukuma na Gwajiboy na akina Halima...wanaopewa ubunge wa zawadi na wahusika..... na kuna akina Kuli na Shida ambao hawajui hata mlo wao wa kwanza wacha wa pili..utatoka wapi. kila sehemu masikini na wenye shida wapo.

Tuwahimize vijana wanaotaka kwenda kutafuta maisha. Waende wakijua watakutana na vitu gani. ila mafanikio yapo na wanaweza kutoboa vilevile.

daima tujifunze kuwa positive!
 
Hivi mzoa taka wa bongo na wa ulaya yupi mwenye nafuu?? 😅😅😅 Huyo mwenyewe anayeongea hapo akiambiwa kurudi kwao hatakubali, au inawezekana hii video Ni kwa ajili ya kukatisha watu tamaa ya kujilipua, jamani eeh wenye kutaka kwenda na waende wanajitoa kwa vyao

Japo katoa ushauri mzuri sana hapo mwishoni
 
Back
Top Bottom