Wenye msimamo kinyume na babu nendeni mkamsimamishe sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye msimamo kinyume na babu nendeni mkamsimamishe sasa

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by NewDawnTz, Mar 25, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwanza niseme yafuatayo


  1. Kama namuunga mkono babu wa Loliondo sijui, na kama simuungi mkono babu wa Loliondo mimi sijui....
  2. MoD pamoja na kuwa kuna nukuu za Biblia tafadhali naomba msiihamishe kwenda kwenye dini maana kule kuna restricted acces na wengi hawataiona...hii ni kwa kuzingatia kama ni kuponya dawa ya Loliondo itaponya wengi wenye dini na wasio na dini, na kama ni kuangamiza itaangamiza wote....Mnisamehe kwa kuomba omba kila mara. Ninafanya hivi kwa kuzingatia ukweli kuwa mijadala imekuwa mingi kwa kutumia Biblia kuonesha kuwa Babu wa Loliondo sio kitu zaidi ya mjumbe wa Shetani kuwaongoza watu upotevuni

  Katika kutaka kujua kama babu ni mjumbe wa shetani anaepotosha watu (kama Juddy na MediaMan wanavyotuaminisha) nilitaka nijifunze humo ndani kujua kama liliwahi kutokea na nini kilifanyika/hatua iliyochukuliwa

  Katika pita ya Biblia nimegsoma Matendo 13:6-11 na kukutana na kisa cha mtu ambae kwa tafsiri ya kina Juddy naweza kumfananisha na babu........

  Huyu anaitwa Mchawi Elymas wa kule Paphos......Huyu kwa mujibu wa Biblia inasema hivi (Paulo akimwambia yule mchawi), Nanukuu "You are a a child of the Devil and an enemy of everything that is right! You are full of all kinds of deceit and trickery. Will you never stop perverting the right ways of the Lord?". Mwisho wa kunukuu

  Kwa kusoma kifungu hiki, akili yangu ikayaona maneno haya sawa na yale ambayo wakina Judith wanasema kwa babu (kimantiki hayana tofauti)

  Sasa hoja yangu hapa ni hii: Wakina Judith, hivi ndivyo watumishi wa kweli wa Mungu wanavyofanya...hupambana na upotovu na wanaoleta upotovu na sio tu kuishia kushauri wale wanaofuata upotovu wasiufuate......Mpingeni Shetani na sio wanaomfuata shetani...

  Mmetoa elimu nzuri sana ndani ya JF lakini JF haina member zaidi ya 40M...............ni karibu 34,000 tu. Hivyo kama ni kupotea wako wengi wanaopotea....dawa ni kwenda kukata mzizi na sio kukata majani ya mti usioutaka.........Bila hivyo tutahisi ni hofu ya kupoteza waumini (may be na sadaka) wanaofuata huduma ya uponyaji kwa maombi

  Kama kweli iko imani ndani yenu kuwa babu anapotosha nakuupotosha ulimwengu na walimwengu tafadhali kimbieni upesi kwa babu na kwa ujasiri kama wa Paulo simameni mbele ya Babu na kumwambia maneno kama haya Paulo aliyomwambia Mchawi Elymas na kuponya wengi kutoka upotevuni

  Bila hivi hamyasaidia chochote na watu wataendelea zaidi upotevuni

  Kama mmjewa na Roho na kujiamni kabisa kuwa babu ni mpotoshaji wa watu, tafadhali hima nendeni Loliondo mkamsimishe kwa mamlaka ya jina la Yesu....kule kule Loliondo na sio JF kwa kufanya kama Paulo...."Filled with the Holy Spirit. looked Straight at Elymas..."

  Bila hivyo mtadaiwa damu za wengi ambazo zifuata opotovu....msijesema sikuwashauri
   
Loading...