Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla

mosi?mkuu pasco kwanza nikukosoe, upinzani dhidi ya CCM na serikali yake siyo wa vyama ni wa wananchi waliojitambu dhidi ya watawala walafi, ili upinzani ufe au ufutike, itabidi watawala walafi waondoke au walau wabadilike, upinzani uko kwenye mioyo ya watu hizi taassisi kama vyama vina kazi ya kucoordnate tu. mbona wlidhani wameiua NCCR, ikaja CUF, then CDM and then...............

pili! kama CCM na serikali yake wameshindwa kuendesha nchi ili kupata faida kubwa kiuchumi, kila siku tunakopa tu, wameshindwa kupata mafanikio ya kiuchumi kwa kuiongoza serikali, wakati nchi ina rasilimali maji aridhi madini,bila kusahau rasilimali watu mill45 na wasomi kibao ambao tuko mitaani hatuna shughulizenye tija, hakika hawawezi kufanikiwa, by simple logic siyo kama umeshindwa nchi yenye resource nyingi,chama hakiwezi hakina resource

tatu! kma chama kimeshindwa kudhibiti rushwa serikalini ni ni kitazuia rushwa isiathiri na kuua hiyo miradi ya kiuchumi itakayoanzishwa,hata kama chama hakitaanzisha na kusimamia miradi moja kwa moja, i wapi nidhamu ya matumizi ambayo hatuioni kwenye serikali yao sikivu??
 
mosi?mkuu pasco kwanza nikukosoe, upinzani dhidi ya CCM na serikali yake siyo wa vyama ni wa wananchi waliojitambu dhidi ya watawala walafi, ili upinzani ufe au ufutike, itabidi watawala walafi waondoke au walau wabadilike, upinzani uko kwenye mioyo ya watu hizi taassisi kama vyama vina kazi ya kucoordnate tu. mbona wlidhani wameiua NCCR, ikaja CUF, then CDM and then...............

pili! kama CCM na serikali yake wameshindwa kuendesha nchi ili kupata faida kubwa kiuchumi, kila siku tunakopa tu, wameshindwa kupata mafanikio ya kiuchumi kwa kuiongoza serikali, wakati nchi ina rasilimali maji aridhi madini,bila kusahau rasilimali watu mill 45 na wasomi kibao ambao tuko mitaani hatuna shughulizenye tija, hakika hawawezi kufanikiwa, by simple logic siyo kama umeshindwa nchi yenye resource nyingi,chama hakiwezi hakina resource

tatu! kma chama kimeshindwa kudhibiti rushwa serikalini ni ni kitazuia rushwa isiathiri na kuua hiyo miradi ya kiuchumi itakayoanzishwa,hata kama chama hakitaanzisha na kusimamia miradi moja kwa moja, i wapi nidhamu ya matumizi ambayo hatuioni kwenye serikali yao sikivu??
 
Preamble!.

"Ukiona mwenzako ananyolewa!,...."

"Ukiona kwa mwenzako kuna ungua!, kwako kunateketea!"

Wale wote wenye mategemeo kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!, ni vizuri wakijiandaa kisaikolojia, ili kuwazui kupata depression inayotokana na despair, kufuatia too much great expectations kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!.

n
doto ya CCM Kutawala Milele!, huenda sasa ndilo linakwenda kutimizwa!.)Quote


Pasco,
mara nyingi nakubaliana na mchango wako, huwa unazungumza logic japokuwa wakati mwingi unadhihirika tu kuwa uko biased.
Kwa hili la leo basi niseme tu kuwa una mawazo sahihi wala hakuna utata, ila nikuulize swali; Hivi unaweza kuamini kuwa miongoni mwa jamii au watu wengi ni wewe tu mjanja, unayeweza kuwa na plans, unayeweza ku cheat, ku maneuver na kutekeleza mambo bila wenzio kujua, kufikiri, kuzuia hadi ukafanikiwa vikwazo vyote- as if ni kama mpira unaocheza na mpinzani wako hawezi kabisa kukuzuia mpaka unamfunga mabao mengi tu! Ili uwe mshindi si struggling inabidi iwe ya juu sana, na bado kuna kushinda au kushindwa.
In short, nataka kusema kuwa hao wapinzani nao si wana akili, plans, goals na vyote huwezi kufikia bila kuwa na strategies mfano za kumwin rival wako? Don't worry Pasco, time will tell na CCM kama unavyoiona wanaweza wakakuta mambo yao yanabuma.

CCM watafanya yote, lakini si guaranteed kuwa watashinda
, wanaweza kuwa losers altogether
 
Hakuna upinzani tanzania ni makundi ya wahuni tu.
Mbona mnahangaika kupambana nao kama sio upinzani. Mbona hamuwapuuzi. Kwako wewe mpinzani anatakiwa aweje? Mimi kinachonishangaza ni kwamba upinzania tanzania ni wapole sana. Ni wavumilivu sana. natamani sasa huu upole na uvumilivu usihe twende sasa jino kwa jino.
 
nimekuelewa sehemu mbili kwanza unaposema lililopangawa ni lazima litimizwe,kwa hili naamini hata upinzani wanaenda ikulu kwani ilishasemwa na Baba wa Taifa juu ya Cdm mwaka 1995 alilitabiri lakini pia kama chama kimejipanga ever since,pili umekubali kwamba sasa ccm inaelekea kupigwa chini na kupoteza viti vingi mno vya mitaa mpaka Taifa,mmeanza kukiri kwa vinywa vyenu yale yaliyonenwa na manabii
 
Mabadiloko ya tawala hayaendi hivyo Pasco.Mara nyingi hujitokeza external element ambayo haikutarajiwa.Na hicho ndicho kitaweza tu kuiondoa CCM kwenye madaraka bila yenyewe kujua au wapinzani kujua.Lini sijui
 
Chochote chenye mwanzo kina mwisho hivyo haiwezekani ccm kutawala milele.
Wanapodhani wapo salama,kifo chake kinakuwa mlangoni. Amini amini nawaambia ccm kitakuwa katika shida kubwa sana mwakani licha ya mipesa yake ya wizi.
Nguzo ya CCM katika chaguzi ni tume yao ya uchaguzi na si vinginevyo.
 
Ukitaka kumuelewa Pasco unatakiwa kusoma mabandiko yake ukiwa umetulia. Baada ya kusoma mi nimekuja na tafsiri kwamba CCM kuendelea kutawala ni ujanja ujanja tu lakini sikwa sababu kinapendwa na watu.
 
CCM haitegemei ruzuku hata siku moja. CCM wanachukua hela kila kona ya hii nchi, wanauza meno ya tembo, unga, mikataba ya kihuni, michango ya lazima nchi nzima, kodi za wananchi n.k lkn baaado inaogopa upinzani.
Sasa leo hii ni biashara gani watafanya CCM ili wapate fedha za kujiendesha kama kwa sasa tu wanabiashara kibao+serikali lkn bado inakuwa ngumu.
Kama ni kuuwa upinzani hilo wasahau kwa sababu wanachama tu wanatosha kuchangia vyama vyao otherwise iwe ni vyama vidogo vidogo vyenye wanachama wachache.

Na ikumbukwe kwamba unapofanya ubaya kwa upinzani ndivyo unavyozidi kuuupa upinzani umaarufu zaidi na zaidi.
Mbinu ya CCM kutawala milele ni ndogo sana, only kuwatumikia wananchi ipasavyo kitu ambacho kwa sasa ni ngumu mno kwao.
Kwahiyo hapa unakuta CCM inajiondoa automatically madarakani.
 
Mkuu Pasco unatatanisha sana wewe.
Turudi kwenye mada. Sio kila plan huwa zinafanikiwa, plan nyingine huwa ni kaburi la mtengeneza plan. Mfano mdogo tu ili Israel iiue PLO ilitengeneza Hamas ndani ya Wapalestina kwa nia ya kuwafarakanisha PLO. Matokeo yake Hamas imekuja kuwa moto mkali kwa Israel.Kuliko PLO ya Fatah.Turudi kwenye Plan ya CCM kusababisha ruzuku iondolewe kwa vyama ili vyama .vidogo vife. Kwa maoni yangu ni sawa na kuviunganisha vyama vyote vya upinzani vyenye nia ya kweli ya kuiondo CCM kwa pamoja na kwa unyonge wao. Kumbuka nguvu ya unyonge ni UMOJA.. Fitina hii ya CCM itapelekea kuupata upinzani wenye nguvu kuwahi kutokea Tanzania hii. Hata hivyo kwa upande mwingine huamini kuwa Chama kama CHADEMA watu huwa wanakichangia kwa hiari na bila vitisho kama CCM?. Na huamini kama CCM ina maadui wa siri wakati CHADEMA ina marafiki wa siri?. Pasco kuna mipango mingine ni ya hila, na hila ni chukizo kwa watu na Mungu. Unaweza kupanga jambo la kumuangamiza adui yako ambae ni kimbilio la wasiokua na sauti halafu ukawaongezea hasira. Hata hili la katiba we subiri tu huko tuendako litakuja kuwa mwiba mkali kwa CCM. Haya ninayoyasema yameshatokea duniani.
 
Preamble!.

"Ukiona mwenzako ananyolewa!,...."

"Ukiona kwa mwenzako kuna ungua!, kwako kunateketea!"

Wale wote wenye mategemeo kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!, ni vizuri wakijiandaa kisaikolojia, ili kuwazui kupata depression inayotokana na despair, kufuatia too much great expectations kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!.

CCM inandaa kifo rasmi cha upinzani na kaburi la kuuzika jumla!, for good!.

Mkakati wenyewe uko hivi!...............

Siri ya Utajiri wa CCM!

Utajiri na rasilimali za CCM ni michango ya lazima kwa Watanzania wote waliokichangia toka katika jasho lao katika kipindi chote cha miaka 30 ya utawala wa chama kimoja, na rasilimali zake karibu zote, zimetokana na uporaji wa jasho la Watanzania.

Hitimisho.
Hivyo basi, Wale wote wenzangu na mimi, wenye matumaini na upinzani kuja kushika dola!, ni bora muendee kutumaini kwa kanuni ya "hope for the best!" but get prepared for the worst!".
Siku hizi, jambo likipangwa lisipotimia, linatimilizwa, na ili litimie kama kuna kitu kinapaswa kufanywa ili kitoshe, kisipotosha kinatosheshwa!.

CCM Hoyee!.

NB. Hii ni opinion yangu!. Everybody has the right to his or her own opinion, wengine sisi tuoneni hivi hivi, tunaona mbali!.
Wasalaam


Pasco.


Pasco,

Katika Watz ambao ni majuha wewe ni nambari wahedi! Mbona umeshahu chanzo muhimu cha mapato cha CCM?? Chanzo hicho ni UFISADI !
Inasikitisha kuona jitu llinapiga makelele mpaka povu linatoka kushabikia ujinga,upuuzi,wizi,ufisadi,udikteta na ubabe wa CCM! Ni aibu kwa kuona jitu au mtu hawezi kujitambua kwa madhila yote haya yanayosababishwa na CCM huku skiendelea kuchekelea na kukenua meno kama zuzu!

Pole sana Bwana Pasco. Leo katika pitapita zangu nilikutana na jamaa moja linafanya katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya fulani hapa nchini. Jamaa huyu akawa analalamika sana kuwa leo tarehe 18/10/2014 lakini bado hajapata mshahara wa Mwezi Septemba,2014!!!

Nikamwuliza unajua ni kwanini hujapata Mshahara akasema ati hawajapelekewa hela ya Matumizi(OC)! Mimi nikamwambia kwamba Hela yote ya Serikali imeishia kwa Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba! Akasema siyo kweli hela ipo ila imechelewa tu. Nikamwambia basi endelea kusubiri. Baadaye tukaendelea na stori zingine na tukagusia mambo ya CCM, mara jamaa akaanza kudai uwa yeye ni shabiki na mpenzi wa CCM na ukimkata inatoka damu ya kijani!!!

Nikamwuliza kwamba wewe umesema unalalamika hujapata mshahara mpaka leo unawezaje kusema wewe ni CCM damu? Hvi hujui kuwa Serikali ya CCM ndiyo inasababisha usipate mshahara wako kwa wakti???Yeye akasema si kweli hata kama tukichagua Wapinzani hela itachelewa tu maana hata hao CHADEMA hawana hela!!!

Nikamwambia kuwa hakuna chama kinachoingia Ikulu na fedha zake mfukoni baali chama ndicho kinaweka sera za namna ya upatikanaji wa mapato kwa maana ya Kodi na vyanzo mbalimbali vya mapato. Nikaendelea kumwelimisha kuwa Tanzania ni nchi tajiri sana maana imejaaliwa na Mwenye enzi Mungu kuwa na Raslimali Lukuki kwa maana ya MADINI,MBUGA ZA WANYAMA,GASI ASILIA n.k. Kinachotakiwa ni kubadilisha mfumo wa Utawala wa chama uliopo kwa sasa ili kupata chama chenye sera bora zenye kusimamia Raslimali hizi na hatimaye ziweze kuwanufaisha Watz!!!

Nashukru kuwa alianza kuona na kuielewa mantiki niliyokuwa namwelewesha na akaanza kufunguka. Bila shaka hapo alipo anaendelea kutafakuri ili mwisho wa siku aweze kuchukua maamuzi sahihi na hatimaye kuachana na ri-CCM lao!

Bwana Pasco naomba uanze kujielewa vinginevo utaishia kuwa....................!!!!!
 
Preamble!.

"Ukiona mwenzako ananyolewa!,...."

"Ukiona kwa mwenzako kuna ungua!, kwako kunateketea!"

Wale wote wenye mategemeo kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!, ni vizuri wakijiandaa kisaikolojia, ili kuwazui kupata depression inayotokana na despair, kufuatia too much great expectations kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!.

CCM inandaa kifo rasmi cha upinzani na kaburi la kuuzika jumla!, for good!.

Mkakati wenyewe uko hivi!.

Miongoni mwa maazimio ya kikao cha NEC ya CCM kilichomalizika leo mjini Dodoma, kimeazimia CCM kuachana kabisa na kutegemea ruzuku, na badala yake CCM sasa kijigeuze kutoka chama cha kijaa, kugeuka chama cha kibepari, kianze kufanya biashara kubwa, kizalishe fedha nyingi, kijitegemee, badala ya hali ilivyo sasa, kinajiendesha kwa kutegemea ruzuku!.

CCM Chama Kubwa!, Chama Tajiri!
Watu wote wanajua fika kuwa CCM ndio chama kikubwa kuliko vyote Tanzania!, ndicho chama chenye wanachama wengi kuliko chama kingine chochote Tanzania!, ndicho chama tajiri, kuliko chama kingine chochote tanzania, na ndicho chama chenye rasilimali nyingi kuliko chama kingine chochote, hivyo kikiamua kujitegemea, ndicho chama pekee chenye uwezo huo wa kujitegemea, bila kutegemea ruzuku!.

Siri ya Utajiri wa CCM!
Utajiri na rasilimali za CCM ni michango ya lazima kwa Watanzania wote waliokichangia toka katika jasho lao katika kipindi chote cha miaka 30 ya utawala wa chama kimoja, na rasilimali zake karibu zote, zimetokana na uporaji wa jasho la Watanzania.

Historia ya Ubinafsishaji!
Ubinafsishaji wa mabenki ulipoanzishwa nchini, wataamu wa benki ya Dunia waliishauri serikali ya Tanzania, kwamba zoezi la ubinafsishaji kwa Tanzania, haliwezekani kwa sababu li bemki la NBC ni kubwa mon na limetapakaa Tanzania nzima, hivyo ndilo lenye monopoly ya mabenki, hivyo hakuna benki nyingine yoyote inaweza kuja na kustawi Tanzania!. Hivyo wakashauri ili kuleta ushindani halali wa mabenki, Li NBC kwanza livunjwe, ligawanywe kwenye vibenki vidogo vidogo, na rasilimali zake ziuzwe ili benki za nje zije ziweze kushindana, hivyo NBC ikavunjwa, na kuundwa NBC, NMB na CHC. Mwalimu Nyerere alishangaa na kukasirika sana!.

CCM Yapora Mali ya Umma!.
Tulivyoanzisha vyama vingi, ili kuleta ushindani halali wa vyama vyote, CCM ilibidi ivunjwe, rasilimali zake zichurudishwe serikalini, wyama vyote vianze moja from the scratch, lakini CCM kilianza hivyo hivyo na mali zake zote ilizo loot toka kwa Watanzania, hivyo kuwa ni chama kubwa tajiri, chenye nguvu ya pesa na rasilimali!, kuvishindanisha na vyama vidogo masikini, sio ushindani halali!. Niliwahi kushauri, siku ikitokea upinzani kuchukua nchi, kazi ya kwanza ni kuipurura CCM mali zote ilizo loot toka kwa Watanzania!.

Lengo la CCM Kujitegemea!.
Uamuzi wa CCM kuamua kujitegemea, ukiuchukulia juu juu, ni jambo zuri!, lakini ukizama ndani deep, kuhusu the motive behind uamuzi huu!, utakubalia na mimi just to "fear the greeks especially when they bring gifts!".
"ulterior motive behind" ya hatua hiyo, kwa CCM kuamua kujitegemea, could be, imegundua ruzuku ndio roho ya vyama vyote vya siasa vyenye nguvu!, kuna uwezekano mkubwa CCM ikapoteza wabunge wengi kwenye bunge lijalo, hivyo kupoteza kiwango kikubwa cha ruzuku!, hivyo sasa CCM inajiandaa kunyolewa!, wapinzani makini wote, watakapoliona hili dubwana kubwa hivi kama CCM, tajiri kama CCM na rasilimali kama CCM, anajianda kunyolewa!, what about hivi vyama sisimizi?!.

Utegemezi wa Ruzuku!.
CCM ndie mfaidika mkuu wa ruzuku, CCM ndie mtegemea mkuu wa ruzuku, lakini vyama vingine vyote ni totally dependant on ruzuku!. Sasa inapotokea chama cha kijamaa kinachofaidi ruzuku, kujipanga kutotegemea tena ruzuku, hili likifanikiwa, kwa CCM kweli kujitegemea, na kuweza kujiendesha bila ruzuku!, amini msiamini, kuna jambo la siri limejificha, usikute wamepanga CCM ikiisha jitegemea, then, zoezi ugawaji ruzuku kwa vyama vya siasa ndio litafikia mwisho, kwa vyama vyote sasa kutakiwa kujitegemea, na kwa vile vingi ya vyama vya upinzani ni vyama ruzuku, ruzuku ikikatwa, huenda huo ndio ukawa mwisho rasmi wa upinzani nchini!, hivyo hili nililowahi kulisema hapa,
[FONT=arial, sans-serif]Ndoto ya [/FONT]CCM Kutawala Milele!, huenda sasa ndilo linakwenda kutimizwa!.

Hitimisho.
Hivyo basi, Wale wote wenzangu na mimi, wenye matumaini na upinzani kuja kushika dola!, ni bora muendee kutumaini kwa kanuni ya "hope for the best!" but get prepared for the worst!".

Siku hizi, jambo likipangwa lisipotimia, linatimilizwa, na ili litimie kama kuna kitu kinapaswa kufanywa ili kitoshe, kisipotosha kinatosheshwa!.

CCM Hoyee!.

NB. Hii ni opinion yangu!. Everybody has the right to his or her own opinion, wengine sisi tuoneni hivi hivi, tunaona mbali!.

Wasalaam

Pasco.
Nimelikumbuka bandiko hili kwa ajili ya ziara ya jana ya Mwenyekiti wa CCM kutembelea Ofisi ndogo ya CCM Lumumba na Ofisi ya Gazeti la Chama Uhuru na kutoa maagizo ya kiserikali.

Ambapo Rais wa nchi ndiye Mkuu wa nchi na Serikali hivyo ndio Mkuu wa dola, na wakati huo huo ndiye Mwenyekiti wa Chama Tawala hivyo hicho chama Tawala ni chama dola, the dividing line is very thin kati ya majukumu ya rais kama Mkuu wa nchi na majukumu ya rais kama Mwenyekiti wa Chama Tawala, gharama zote tunazigharimia sisi Watanzania katika ujumla wetu, hivyo CCM ni chama dola! . Wanaosubiri chama kingine kuja kushika dola, watasubiri sana! .
Cc. Yericko Nyerere
Pasco
 
Mwendo wa siasa za upinzani Tanzania ni huu, halafu kama bado kuna watu wanamatumaini kuna siku Upinzani Tanzania utashika dola, then, watasubiri sana!.

CCM ni chama dola!.

Paskali
 
Back
Top Bottom