Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,602
Preamble!.

"Ukiona mwenzako ananyolewa!"
na "Ukiona kwa mwenzako kuna ungua!, kwako kunateketea!"

Wale wote wenye matumaini na mategemeo kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!, hawa ni wishful thinkers na day dreamers, wanao ota ndoto za mchana, wasahau kabisa!.

Lengo la uzi huu ni kuwaanda kisaikolojia, wale wote wenye matumaini chanya, kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi vya siasa, hivyo kuwa na mategemeo, kuna siku itafika, ambapo wapinzania pia watashika dola, na CCM itakuwa ni chama cha upinzani!, wasahau kabisa hili jambo, ili kuwazui kupata depression inayotokana na despair, kufuatia kuwa na too much great expectations kuwa kuna siku upinzani wa nchi hii, utakuja kushika dola!.

CCM inandaa kifo rasmi cha upinzani kwa dose za taratibu, na kuandaa kaburi la kuuzika jumla upinzani wa Tanzania!, na utauzika for good!.

Mkakati wenyewe uko hivi!

Miongoni mwa maazimio ya kikao cha NEC ya CCM kilichomalizika leo mjini Dodoma, kimeazimia CCM kuachana kabisa na kutegemea ruzuku, na badala yake CCM sasa kijigeuze kutoka chama cha kijamaa, kugeuka chama cha kibepari, kianze kufanya biashara kubwa kubwa kwa kuanzia na real estates, kizalishe fedha nyingi, kijitegemee, badala ya hali ilivyo sasa, kinajiendesha kwa kutegemea ruzuku!.

CCM Chama Kubwa! Chama Dola, Chama Tajiri!
Watu wote wanajua fika kuwa CCM ndio chama kikubwa kuliko vyote Tanzania!, licha ya kuwa ni chama dola, yaani ukizungumzia serikali ya Tanzania, unazungumzia CCM, yaani CCM ndio serikali ya Tanzania yenye jeshi, polisi, bunge na mahakama!, ndicho chama chenye wanachama wengi kuliko chama kingine chochote Tanzania!, ndicho chama tajiri, kuliko chama kingine chochote tanzania, na ndicho chama chenye rasilimali nyingi kuliko chama kingine chochote, hivyo kikiamua kujitegemea, ndicho chama pekee chenye uwezo huo wa kujitegemea, bila kutegemea ruzuku!.

Siri ya Utajiri wa CCM!
Utajiri na rasilimali za CCM ni michango ya lazima kwa Watanzania wote waliokichangia kwa michango ya lazima toka katika jasho lao katika kipindi chote cha miaka 30 ya utawala wa chama kimoja, na rasilimali zake karibu zote, zimetokana ama na michango ya lazima ya jasho la Watanzania wote, ama kupitia uporaji wa rasilimali za taifa ilizokuwa inajimegea kutoka serikalini ambazo ni mali halali za Watanzania.

Historia ya Ubinafsishaji!
Ubinafsishaji wa mabenki ulipoanzishwa nchini, wataalamu wa benki ya Dunia waliishauri serikali ya Tanzania, kwamba zoezi la ubinafsishaji kwa Tanzania, haliwezekani kwa sababu li benki la NBC ni kubwa mno na limetapakaa Tanzania nzima, hivyo ndilo lenye kuhodhi monopoly ya sekata ya mabenki nchini, hivyo hakuna benki nyingine yoyote inaweza kuja na kustawi Tanzania!. Hivyo wakashauri ili kuleta ushindani halali wa mabenki nchini, hili Li benki likubwa la NBC, kwanza lazima livunjwe, ligawanywe kwenye vibenki vidogo vidogo, na rasilimali zake ziuzwe ili benki za nje zije zilinunue ziweze kushindana, Mzee Ruksa alikuwa hana hiyana, akakubali, hivyo NBC ikavunjwa, na kuundwa NBC, NMB na CHC. Mwalimu Nyerere alishangaa na kukasirika sana na kiukweli hatua ilimtoa machozi, akaiandikia kitabu cha "Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania".

CCM ni Chama Dola, Utenganishaji wa Kofia Mbili ni Kiini Macho!
Tulivyoanzisha vyama vingi nchini, CCM kilikuwa chama Dola, ndicho kilichokuwa kimeshika hatamu za uongozi wa nchi, viongozi wote wa serikali walikuwa na kofia mbili za chama na serikali. Tulivyoanzisha vyama vingi, tukaondoa kofia mbili kule chini kote, kofia mbili zikabaki kwa Mwenyekiti tuu wa CCM, ndie rais wa nchi, lakini kwenye nafasi nyingine zote, watendaji wa CCM walivuliwa kofia moja, watu wakidhani huku ni kuwapunguzia mamlaka makada wa CCM serikalini, kumbe hawakujua, wateule wote walioteuliwa kwenye nyadhifa serikali ni makada wa CCM!. Hivyo CCM kuwa na nguvu zaidi, badala ya mtu mmoja kuwa na kofia mbili, sasa ni watu wawili!, ma RC, Ma DC, Spika, na watendaji wengine wote wakubwa wa serikalini ni makada!

Mali na Rasilimali za CCM ni Mali ya Umma, na Rasilimali za Umma
Wakati wote wa Chama kimoja, wafanyakazi wote wa nchi hii walikatwa michango ya lazima kukichangia Chama kana tunavyokatwa kodi kwa lazima. na kwa vile CCM ni chama dola, majengo, viwanja na maeneo inayomiliki na rasilimali mali ni mali za serikali ambazo ilijigawia kwa sababu CCM ilikuwa ndio serikali, huwezi kujiibia mwenwenyewe, mali ya serikali ni mali yako, hivyo CCM ilikuwa inajichukulia tuu mali zake.

Kama Ilivyo kwa NBC, Ilibidi Kwanza CCM Ivunjwe Ndipo Tuanze Mfumo wa Vyama Vingi
Ili kuleta ushindani halali wa vyama vyote, CCM ilibidi ivunjwe, rasilimali zake zichurudishwe serikalini, vyama vyote vianze moja from the scratch, lakini CCM kilianza hivyo hivyo na mali zake zote ilizo loot toka kwa Watanzania, hivyo kuwa ni chama kubwa tajiri, chenye nguvu ya pesa na rasilimali!, kuvishindanisha na vyama vidogo masikini, sio ushindani halali!. Niliwahi kushauri, siku ikitokea upinzani kuchukua nchi, kazi ya kwanza ni kuipurura CCM mali zote ilizo loot toka kwa Watanzania!.

Lengo la CCM Kujitegemea!

Uamuzi wa CCM kuamua kujitegemea, ukiuchukulia juu juu, ni jambo zuri!, lakini ukizama ndani deep inside, utagundua kuhusu the motive behind uamuzi huu!, utakubalia na mimi just to "fear the Greeks especially when they bring gifts!"

"ulterior motive behind" ya hatua hiyo, kwa CCM kuamua kujitegemea, could be, imegundua ruzuku ndio roho ya vyama vyote vya siasa vyenye nguvu!, kuna uwezekano mkubwa CCM ikapoteza wabunge wengi kwenye bunge lijalo, hivyo kupoteza kiwango kikubwa cha ruzuku!, hivyo sasa CCM inajiandaa kunyolewa!, wapinzani makini wote, watakapoliona hili dubwana kubwa lenye mali na lenye nguvi hivi kama CCM, tajiri kama CCM na rasilimali kama CCM, anajianda kunyolewa!, what about hivi vyama sisimizi?!.

Utegemezi wa Ruzuku!
Mpango wa kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa, ulibuniwa ili kuinufaisha CCM!. CCM ndie mnufaika na mfaidika mkuu wa ruzuku, CCM ndie mtegemezi mkuu wa ruzuku, lakini vyama vingine vyote ni totally dependant on ruzuku!. Sasa inapotokea chama cha kijamaa kinachofaidi ruzuku, kujipanga kutotegemea tena ruzuku, hili likifanikiwa, kwa CCM kweli kujitegemea, na kuweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku!, amini msiamini, huo ndio utakuwa mwisho wa ruzuku!. Nahisi kuna jambo la siri limejificha, usikute wamepanga CCM ikiisha jitegemea, then, zoezi ugawaji ruzuku kwa vyama vya siasa ndio litafikia mwisho, kwa vyama vyote sasa kutakiwa kujitegemea, na kwa vile vingi ya vyama vya upinzani ni vyama ruzuku, ruzuku ikikatwa, huenda huo ndio ukawa mwisho rasmi wa upinzani nchini!, hivyo hili nililowahi kulisema hapa chini kwenye rejea, huenda sasa ndilo linakwenda kutimizwa!.

Ushauri na Hitimisho
Kwa vile Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na vyama hivyo vipo kwa mujibu wa katiba, then, uongozi wa chama chochote kilicho madarakani, una wajibu wa kuvilea vyama vingine na sio kuviangamiza.

Hivyo basi, Wale wote wenzangu na mimi, wenye matumaini na upinzani kuja kushika dola!, hii jamani kwa Tanzania ni ndoto ya mchana kweupe, ni bora muendelee kutumaini kwa kanuni ya "hope for the best!" but get prepared for the worst!".

Siku hizi, jambo likipangwa lisipotimia, linatimilizwa, na ili litimie kama kuna kitu kinapaswa kufanywa ili kitoshe, kisipotosha kinatosheshwa!. Kwa sasa tumshukuru sana Kikwete, ni mtu mwenye utu na aibu ya kuua upinzani wasiwazi, lakini siku za mbele, anaweza kutokea mtu katili asiye na huruma, akauua upinzani wazi wazi huku tukishuhudia.

CCM Hoyee!

NB. Hii ni opinion yangu!. Everybody has the right to his or her own opinion, wengine sisi tuoneni hivi hivi, tunaona mbali!, hivyo bandiko hili nitalitunza as a reference materials, siku ya siku likitimia, nitakumbusha.

Wasalaam

Paskali
PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!
CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?
Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?
Watch TBC Live!. " William Malecela na Ndoto ya CCM Kutawala Miaka 50!.
 
Preamble!.

"Ukiona mwenzako ananyolewa!,...."


Tatizo lako unataka kupingana na historia. Njia ya CCM kuendelea kutawala ni moja tu: KUWATUMIKIA WATANZANIA KWA HAKI NA KUWAPATIA MAISHA BORA. Kinyume cha hapo WATAONDOLEWA iwe na upinzani au wananchi wenyewe bila kujali mambo ya vyama... (na wana CCM ndani). Lakini sikulaumu sana kwani jinsi CCM walivyolewa madaraka ndivyo wanavyofikiri itakuwa.
 
Ulichosema ni 100% correct! Lkn malengo yao haya si rahisi kuya-achieve. Ili waya-achieve inabidi viongozi na wanachama kwa jumla waache ufisadi ambao sasa umekuwa moja ya itikadi za CCM (CHUKUA CHAKO MAPEMA).

Sasa hivi ni vigumu sana kuanzisha viable business kuliko ilivyokuwa zamani walipokuwa na kila opportunity. Nini kilififisha au kuua miradi yao ya awali kama vile SUKITA? Je sababu hazipo tena?

Kumbuka wa-NEC wa CCM ni viongozi ambao ndiyo waliyoua miradi ya nyuma. Ile miradi haikuuawa na wanachama wa kawaida wa chama.

Motive ya hawa viongozi wa CCM kutaka kufanya biashara sasa ni ile ile, yaani wapate nafasi ya kuchukua chao mapema kabla ya mwisho wa 2015. Usitegemee ghafla wataacha ufisadi. IMPOSSIBLE, I DECLARE!!
 
By the way, mbavu za kutekeleza jambo hilo CCM watalitoa wapi? Ruzuku kwa vyama vya siasa ni mojawapo ya masharti ya IMF na World Bank (Economic and political Reforms). Hebu waanze tuone hiyo ngonjera ya kunyimwa nyongeza kwenye bajeti wataichezaje!
 
Ni ndoto za mchana kila kiongozi anaiba mali ya chama iliyokuwa iko chini ya mamlaka yake, kwa hiyo kujitegemea na wizi wao huo ni ndoto, halafu mwekiti wao huyo ni afadhari nyani akamalizia wakati uliobaki wa uenyekiti wake wa chama, nyani huyo ataweza kufanya la maana , huyo mwenyekiti wao ni masihala tupu.
 
being optimistic is the best way that can push you forward...even if it would take 5yrs..20yrs or 50yrs from now.....''THE POWER OF POSITIVE THINKING''...
WHEN SOUTH AFRICA DECLARED''FREEDOM IS COMING TOMORROW''...YOU SAW HOW LONG THAT ''TOMMORROW'' TOOK...
 
Mkuu Pasco

Hili nimelipokea kama kengere ya hatari kichwani mwangu tangu nilipoliata humu jamvini na kunamahali nimeonyesha wasiwasi wangu juu ya wazo hili walilokuja nalo hawa Ccm. Kiukweli ni hakika kabisa vyama vya Upinzani ni lazima kabisa waanze kufikilia vyanzo mbadala vya kuwaingizia mapato vinginevyo Vinakwenda kufutika mithiri ya chaki ubaoni.

Chama hiki kimefanya mengi maovu ktk taifa hili hakiko tayari kuachia madaraka katika kipindi hiki kwasababu kufanya hivyo ni sawa na kujipeleka mwenyewe Police ilhali unajua anatafutwa mwizi na wewe ndiwe uliyeiba!!!

Vyama vya upinzani ni lazima viboreshe vyanzo vyake vya mapato viache kutegemea ruzuku, Ikumbukwe ni hawa ccm baada ya Chadema kuchanja mbuga nchi nzima na wananchi kujipanga barabarani kuitikia maandamano na mikutano ya Chedema kwa maelfu ccm kupitia serikali walichimba mkwara kwamba wataacha mara moja kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa kwa kuwa eti vinatumia hela nyingi bila tija!!!

Kiukweli ingawaje walikuwa wakitishia nyau kwa wakati ule, ila mwitikio na presha ya vyama vya siasa hususani vya upinzani, ndio uliowafanya kuliboresha wazo lile "kimkakati" ili kuviteketeza kabisa vyama hivyi "Vichanga" Wapinzani walipokee hili kama ni kengere ya alarm iwakumbushe yale yaliyowahi kufanywa na chama hiki na serikali yake huko nyuma na Vijipange

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Mpaka Leo CCM haijiendeshi kwa ruzuku ya Chama bali mikataba ya ajabuajabu inayoingiwa na wawekezaji.

Kuna mikataba mingi inayofumbiwa macho kirahisi tu, kiasi hata wananchi mkihoji hamuwezi kupewa jibu la maana zaidi ya blabla.

Mkuu Pasco amini kwamba kwa jinsi dunia ya utandawazi inavyokwenda kasi watanzania itafika mahali hatutahitaji Chama cha siasa kutukomboa na makucha ya CCM.

Rejea ya Misri, vile CCM inavyojitengenezea mazingira ya kudumu madarakani ndivyo inavyozidi kuwaamusha Watanzania.


CCM inaweza kutawala Muda mrefu ila sio milele,acha waendelee kutukusanyia hasira mioyoni mwetu.!!
 
Last edited by a moderator:
Kwa uzi huu inaonekana wapinzani wamefanikiwa sana kuwaelemisha watanzania kiasi cha CCM kuona madhara waziwazi.

Hongereni vyama vya upinzani msikate tamaa watanzania tunaelewa mnachotufanyia ila sio vile vyama pendwa kwa CCM kama UDP,NCCR, ACT na vingonevyo.
 


Historia ya Ubinafsishaji!
Ubinafsishaji wa mabenki ulipoanzishwa nchini, wataamu wa benki ya Dunia waliishauri serikali ya Tanzania, kwamba zoezi la ubinafsishaji kwa Tanzania, haliwezekani kwa sababu li bemki la NBC ni kubwa mon na limetapakaa Tanzania nzima, hivyo ndilo lenye monopoly ya mabenki, hivyo hakuna benki nyingine yoyote inaweza kuja na kustawi Tanzania!. Hivyo wakashauri ili kuleta ushindani halali wa mabenki, Li NBC kwanza livunjwe, ligawanywe kwenye vibenki vidogo vidogo, na rasilimali zake ziuzwe ili benki za nje zije ziweze kushindana, hivyo NBC ikavunjwa, na kuundwa NBC, NMB na CHC. Mwalimu Nyerere alishangaa na kukasirika sana!.

Pasco.
Pasco

na hapo ndipo mzee wetu wa Lushoto alipoona Uzia na kuona jamaa atamkwamisha kwenye mipango yake ya kuendelea kuuza mashirika mengine , na ndipo wakamuambia Mzee unaumwaa wewe, twende ukatibiwe, inasemkena mzee aligoma, sijuhi ni nani alimshawishi akakubali kwenda kule Uingereza, Kilichobaki ni Historia.
 
Upuuzi mwingine kutokana na kibahasha...!

KWA MIAKA TAKRIBANI 50 CCM IMESHINDWA KUIFANYA NCHI YETU IJITEGEMEE BADALA YAKE TUNATEGEMEA BAKULI.

ENDELEENI KUJITEKENYA NA KUCHEKA WENYEWE.
 
Ni kweli kuwa katika uchaguzi ujao (serikali za mitaa na serikali kuu) CCM ina hali mbaya sana na wazo hilo ndiyo njia pekee ya kujinusuru kwa CCM.
 
Back
Top Bottom