Mimi binafsi sioni sababu ya kuendelea kuwa na TAKUKURU wala waajiriwa wake maana ni kupoteza bure kodi za watanzania. Tangu iamzishwe, pamoja na kupewa uwezo mkubwa zaidi kisheria na kubadilishwa jina toka TAKURU kuwa TAKUKURU, taasisi hii imekosa tija kwa taifa, haijaweza kudhibiti rushwa wala kuipunguza. Siwashangai wanaoibeza kuwa ni yafaa kirefu chake kuwa ni "Taasisi ya Kuruhusu na Kupamba Rushwa". Sasa hebu sikia hiki kituko kingine, eti TAKUKURU badala ya kufanya uchunguzi wake kugundua viongozi wa serikali walioiba na walioficha fedha Uswisi, leo Dr. Hosea anasema eti wenye majina wampelekee. Hivi TAKUKURU japokuwa ina watumishi wengi wanaolipwa fedha nyingi inakaa ofisini na kuwataka watu wenye taarifa za rushwa na walioficha fedha Uswisi kuna haja gani ya kuendelea kuihudumia taasisi hii isiyokuwa natija kwa taifa? Lakini wiki kadhaa zilizopita wakati vuguvugu la walioficha fedaha lilipokuwa hot, Dr. Hosea alisema anafanya uchunguzi. Je ni nini Dr. Hosea amekifahamu kupitia uchunguzi wake, kama kweli aliufanya?