Wenye majina ya watu walioweka fedha uswisi wawataje - Mkuchika!

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,597
1,005
waziri mkuchika amewataka wale wote wenye majina ya watu walioficha fedha uswisi wawataje ili washughulikiwe.

Itv habari
 
Mie, siwajui! Uswizi wametoa masharti magumu ili kushilikiana na selikari dhaifu kuwabaini hao watu.
 
waziri mkuchika amewataka wale wote wenye majina ya watu walioficha fedha uswisi wawataje ili washughulikiwe.

Itv habari

Wewe hebu elezea vizuri, ebo!

Anayeshughulikiwa nani, ANAYETAJA au ANAYETAJWA? Manake hii serikali yetu imegeuzwa betri usije ukatuponza bure
 
Kweli Tanzania tuna viongozi wendawazimu kabisa badala ya kutupa matokeo ya uchunguzi wao wa zaidi ya miezi mitatu sasa kuhusu suala hilo, wao wanakuja leo wanataka tuwatajie majina!!!

Kesho nitawatumia majina ya watu wanaotuhumiwa kuficha pesa Uswis ili tuone kama watawachukulia hatua.
 
Hosea amesema wanataka watu woote wenye majina yao wampelekee ili waanze kuyashuhulikia, na hatua zichukuliwe.

Hapa naona wameanza kuweka vizuizi!
 
Kama serikali ya ccm haiwajui hao mafisadi haina haja ya kuendelea kukaa madarakani kwani wameshimdwa hata kuwakamata wahujumu uchumi wa nchi yetu.Ni wanafiki wakubwa.Hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole kwani wote ni wachafu.
 
Mie, siwajui! Uswizi wametoa masharti magumu ili kushilikiana na selikari dhaifu kuwabaini hao watu.

wala siyo magumu hiyo ndiyo itifaki yenyewe...benki haziendeshi kwa majungu na umbea..hizo ni akaunti na fedha halali mpaka sasa unless proven otherwise na tz kuwa kuna tatizo na umiliki wa hizo akaunti pamoja na hela zake. kwa vile wanaomiliki hizo akaunti wamewahi kuwa wafanyakazi wa serikali na walijaza fomu za mali na fedha walizonazo na wanavyozipata itakuwa rahisi kama tz wana takwimu zao na kuiambia uswisi kuwa takwimu zetu hazionyeshi watu hao kuwa na kiasi hicho cha fedha.
 
...vyombo vilivyopewa kazi ya kuchunguza kazi imewashinda...eti wamekaa wanataka wapelekewe majina na...hahaa...eti na ushahidi...
 
Hosea amesema wanataka watu woote wenye majina yao wampelekee ili waanze kuyashuhulikia, na hatua zichukuliwe.

Hapa naona wameanza kuweka vizuizi!

Hosea alishindwa richmond ya lowasa itakuwa mihela ya nje kabisa uswiss?
 
wala siyo magumu hiyo ndiyo itifaki yenyewe...benki haziendeshi kwa majungu na umbea..hizo ni akaunti na fedha halali mpaka sasa unless proven otherwise na tz kuwa kuna tatizo na umiliki wa hizo akaunti pamoja na hela zake. kwa vile wanaomiliki hizo akaunti wamewahi kuwa wafanyakazi wa serikali na walijaza fomu za mali na fedha walizonazo na wanavyozipata itakuwa rahisi kama tz wana takwimu zao na kuiambia uswisi kuwa takwimu zetu hazionyeshi watu hao kuwa na kiasi hicho cha fedha.

Wewe unategemea salikari hii ifate hayo masharti? hao aw kuyafata ndio wahusika ... Baba tumeliwa tufanya mabadiliko kwanza
 
waache ubabaishaji kama hakuna kitu kama hicho si waseme kwa uhakika! waache longolongo la kutaka wapelekewe majina. hivi taasisi za dola haziwezi kupata majina mpaka watajiwe? basi hatuna nchi kana vyombo vyetu ni hivo vinavotegemea upelelezi wa zito
 
Mimi binafsi sioni sababu ya kuendelea kuwa na TAKUKURU wala waajiriwa wake maana ni kupoteza bure kodi za watanzania. Tangu iamzishwe, pamoja na kupewa uwezo mkubwa zaidi kisheria na kubadilishwa jina toka TAKURU kuwa TAKUKURU, taasisi hii imekosa tija kwa taifa, haijaweza kudhibiti rushwa wala kuipunguza. Siwashangai wanaoibeza kuwa ni yafaa kirefu chake kuwa ni "Taasisi ya Kuruhusu na Kupamba Rushwa". Sasa hebu sikia hiki kituko kingine, eti TAKUKURU badala ya kufanya uchunguzi wake kugundua viongozi wa serikali walioiba na walioficha fedha Uswisi, leo Dr. Hosea anasema eti wenye majina wampelekee. Hivi TAKUKURU japokuwa ina watumishi wengi wanaolipwa fedha nyingi inakaa ofisini na kuwataka watu wenye taarifa za rushwa na walioficha fedha Uswisi kuna haja gani ya kuendelea kuihudumia taasisi hii isiyokuwa natija kwa taifa? Lakini wiki kadhaa zilizopita wakati vuguvugu la walioficha fedaha lilipokuwa hot, Dr. Hosea alisema anafanya uchunguzi. Je ni nini Dr. Hosea amekifahamu kupitia uchunguzi wake, kama kweli aliufanya?
 
Huu msimamo wa serikali kutaka majina ya walioficha pesa Uswisi au popote pale nje ya nchi yatajwe, ni janja ya serikali kuipotezea/kuiua hoja ya Zitto Kabwe kisanii. Kwa sababu kama kutajwa kwa majina ya hao mafisadi ndiyo kutaifanya serikali ichukue hatua , basi chenge na mwezake idrisa Rashid ambao walitajwa na SFO ya Uingereza kwenye sakata la rada, walitakwa wawe wameishashitakiwa au wangekuwa jela miaka mingi iliyopita.
 
TAKUKURU, Usalama wa Taifa vyote hivi viko chini ya wizara anayoongoza Mkuchika. Kama Mkuchika anashindwa kuchunguza taarifa za hela huko Uswis basi hana sifa ya kuwepo kwenye hiyo nafasi. Anategemea wauza korosho wa Newala wawe na taarifa za watanzania wanaoficha hela Uswis? Kwanini tuendelee kugaramia ofisi yake kama hana uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom