real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,303
Biashara ya fremu inatajwa kuwa ndiyo iliyokuwa inawalipa zaidi wenye nyumba kuliko kupangisha vyumba vya kuishi.
Katika nyumba nyingi za jiji la Dar es Salaam, ni nadra kukuta iliyojengwa bila kuwa na maduka ya biashara, maarufu kwa jina la fremu.

Ndiyo maana nyumba nyingi ama zina fremu tayari au zimejengwa kwa ramani ya kuwa nazo siku za baadaye.
Khalfani Kizungu anayeishi Mtoni Mtongani, anasema mwaka 2005 aliibadili nyumba yake ya vyumba sita alivyokuwa akipangisha na kulipwa kodi ya Sh 20,000 kila chumba na kuizungusha fremu za maduka.
Baada ya kujenga fremu anasema akaanza kujipatia Sh 50,000 kwa kila fremu. Baadaye alipandisha bei hadi kufikia Sh70,000 mwanzoni mwa mwaka 2016.
Wakati miaka ya nyuma biashara hii ikionekana kuwa na kipato kikubwa kiasi cha kuwavutia watu wengi kama ilivyo kwa Kizungu, hivi sasa wamiliki wa fremu wanalia njaa.
Mwanzoni Kizungu alifikiri kuna mkono wa mtu baada ya fremu zake kuanza kudoda, lakini ukweli ni kuwa wafanyabiashara wengi wanalalamika kukosa wateja wa bidhaa zao.
“Hawa wapangaji watatu waliomaliza mkataba wao mwishoni mwa mwaka jana, ni kama waliniwangia kwa sababu fremu zimekuwa zikikaa hadi miezi mitatu bila mpangaji ilihali hapa ni barabarani na hapo kabla zilikuwa zinagombewa,’’ anasema na kuongeza:
“Mpangaji akija anataka kulipa miezi sita, nimekataa hadi nimekubali, lakini hali ilivyo hawa waliobaki wakimaliza mkataba wao sidhani kama wataongeza kwa sababu wanalalamika hakuna biashara.’’
Kauli ya Kizugu inaoana na ya Halima Yunus, mkazi wa Buza wilayani Temeke. Anasema kuwa anataka kubadili fremu zake kuwa vyumba vya kupangisha kwa sababu anakufa njaa.
Anasema alipoachishwa kazi katika benki moja, fedha zake aliamua kujenga nyumba na kuweka vitega uchumi ikiwamo kuchimba kisima cha maji kwa ajili ya kuuza na kujenga fremu nne za biashara.Alianza biashara hiyo mwaka 1995 huku ikiwa inafanya vizuri.
“Kwa mara ya kwanza nimekaa na fremu ikiwa haina mpangaji mwaka juzi, kuanzia hapo kadri siku zinavyokwenda hali ndiyo kama hiyo, tatu hazina watu nimeweka maji ya kandoro nauza na barafu na moja ina mpangaji anayelipa kwa miezi mitatu,’’ anasema na kuongeza:
“Nilikuwa nina uhakika wa kupata zaidi ya milioni nne kila mwaka, ikiwa ni kodi ya pango ambayo hupanda na kushuka kulingana na makubaliano kati yangu na mpangaji.’’
Yunus anaeleza kuwa baada ya kusikia msisitizo wa kulipa kodi ya majengo, alifurahi akidhani hali ya biashara ingebadilika, matokeo yake anasema wapangaji wanabanwa kodi huku wakikosa wateja..
Mpangaji pekee aliyebaki katika fremu za nyumba ya Yunus, ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, anasema akimaliza mkataba wake wa miezi mitatu aliolipa Desemba mwaka jana, atabadili eneo la biashara.
“Eneo kwa mwonekano ni zuri, limechangamka, lakini halina biashara kabisa, kodi ni kama nimetupa haijarudisha hata nusu hasara zaidi vitu vinaharibika,’’ anaeleza.
Pamoja na bidhaa za nyumbani kama vile mchele, unga, mafuta kwa mitaani kufanya vizuri, anashangaa kuwa kwa mtaani hapo biashara hiyo kwake imegoma.
“Nikikuonyesha daftari la madeni unaweza kuniona sina akili, kwa sababu watu wanasema ukimkopesha mteja umemfukuza, lakini mimi nimeona bora nitumie njia hiyo ili angalau nipate nusu hasara wakati natafuta eneo zuri zaidi, kwa hapa imeshindikana, ”anasema.
Naye Haji Omari ambaye ni mfanyabiashara wa nguo katika soko la Tandika shuleni, anasema mwaka juzi na mwaka jana biashara imekuwa mbaya na amekuwa ananunua nguo kwa kuvizia.
“Ona hizo zilivyopauka, mstari wa juu wote hizo zimekufa siwezi kumuuzia mtu, hakuna biashara ndiyo maana nimechanganya na madera ya dukani ambayo angalau yana wateja kutokana na bei yake kuwa chini,’’ anaeleza.
Anasema siku zote amekuwa akiuza nguo za mitumba na anapata wateja na kulipa kodi ya fremu kwa miezi sita kama walivyokubaliana na mwenye nayo, lakini sasa wana mgogoro kwa sababu hajamlipa.
“Nilimuomba achukue kodi ya miezi mitatu kwanza nyingine nimpe baada ya mwezi nikipokea mchezo (upatu), huwezi kuamini huo mchezo wenyewe umevurugika watu hawana fedha na sijamlipa,’’anasema.
“Muda wowote atanifukuza kwa hasira kwa sababu hatuelewani lugha, nikimwambia sijapata ananiona jeuri, ona wenzangu hao wamefunga siyo kwa kupenda wamekimbia madeni ya waleta mzigo na mwenye fremu anawadai, ” anasema Omari huku akionyesha fremu mbili ambazo zimefungwa.
Profesa wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Humphrey Moshi, anasema ni wazi kuwa biashara imebadilika kama wanavyolalama wenye fremu na wafanyabiashara.
Anasema wakati huu kuna mabadiliko ya uchumi na watu wameshindwa kwenda na mabadiliko hayo, badala yake wanataka hali iwe kama zamani.
Kuna mambo kadhaa anayosema yamesababisha hali hiyo kutokea, ikiwamo vita dhidi ya rushwa ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza fedha iliyokuwa inapatikana katika mianya isiyo rasmi.
“Umakini katika ukusanyaji kodi pia umesababisha fedha kuadimika, kuna mtu alikuwa anapata faida asilimia 60 na alikuwa halipi kodi,’’ anasema na kuongeza:
“Wakati huu anaolazimishwa kulipa kodi kwa kila anachofanya ni lazima atapata asilimia 20 ambayo kwake itakuwa ni sawa na bure, lakini katika nchi zenye uchumi wa ushindani, faida katika biashara hushuka na kufikia hadi asilimia 10.’’
Profesa Moshi anaitaja sababu nyingine ya wafanyabiashara wa kawaida kulalamikia biashara kuwa mbaya kuwa, ni fedha ya bajeti ya Serikali kuu kutotumika katika matumizi ya kawaida, badala yake kutumika katika masuala makubwa ikiwamo ujenzi wa miundombinu.
Aidha, anasema fedha zimekuwa zikipelekwa Benki Kuu ambako hawazifanyii biashara, hali inayochangia kukosekana kwa fedha kwa walio wengi.
“Kosa lilifanyika huko nyuma ambapo tulikubali kubinafsisha hadi benki za biashara. Zingekuwepo fedha zingepelekwa huko zingeendelea kuwepo kwenye mzunguko na hali ingekuwa na nafuu kiasi.
“Huko nyuma uchumi haukuwa asilia, kipindi hiki ni cha mpito cha kuufanya uchumi uwe halisi, zamani walikuwa wanauza au kupangisha viwanja na fremu kwa bei mbaya, lakini sasa kila mmoja analipa kulingana na anachokipata, ”anasema Profesa Moshi.
Mtaalamu mwingine wa uchumi, Dk Godwin Maimu anasema Serikali inafanya mabadiliko ya kiuchumi ili kutengeneza uchumi ulio rasmi.
Mabadiliko hayo yanaweza kusababisha hiki kinachotokea sasa kwa sababu inadhibiti matumizi ya fedha na kuipandisha thamani.
Anasema kutokana na hali hiyo hakuna fedha inayotumika kununua vitu vya kawaida, kila aliyonayo ananunua vitu vya maana na kuachana na uwekezaji usio na tija.
“Kwa sababu fedha ilikuwa nyingi, hakuna kubanwa kulipa kodi kila mmoja alitamani kuwa mfanyabiashara na alifanikiwa kwa sababu kulikuwa na mzunguko wa fedha usio rasmi. Baada ya muda hali itakuwa nzuri na wananchi watakuwa wamejifunza nidhamu ya fedha,”anasema Dk Maimu.
Chanzo: Mwananchi