- Wakati tukisubiri SMZ ilipe madeni nusu nusu huko SMT basi ni vyema Taasisi hizi zinazodaiwa na serikali zikalilipa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) ili Shirika liweze kuwalipa TANESCO. Deni hili ni kubwa ni mzigo kwa ZECO. Dawa ya deni ni kulipa SMZ lipeni.
- 1) Mamlaka ya Maji inadaiwa Shs. 16,016,312,000/= mpaka Septemba
2) Wizara ya Afya Shs. 500,000,000/= mpaka Septemba
3) Manispaa Shs. 881,000,000/= mpaka Septemba...
4) Idara ya Anga Shs. 883,000,000/= mpaka Septemba, Sijui Oktoba na Novemba.
5) Sauti ya Tanzania Zanzibar Shs. 717,000,000/=
6) Wizara ya Kilimo Shs. 410,000,000/= mpaka Septemba hiyo
7) Chuo cha Mafunzo Shs. 69,261,000= haijambo kidogo
8) KMKM Shs. 127,000,000/= mpaka Septemba
9) Afisi ya Rais Ikulu Shs. 313,000,000/= mpaka Septemba hiyo, Hansard zikae sawa
10) Afisi ya Baraza la Wawakilishi Shs. 19,000,000/= pesa ndogo sana hiyo, nalipongeza Baraza la Wawakilishi.
11) Uwanja wa Amaan Shs. 103,000,000/= mpaka Septemba inadaiwa.
12) ZBC TV Shs. 191,000,000/= mpaka Septemba
13) Idara ya UUB Shs. 27,000,000/= Haijambo kidogo
14) Bandari Huru Shs. 9,000,000/= Haijambo kidogo - Hawa viongozi wengine siwezi kutaja wa Serikali nitaona haya kidogo, lakini mpaka Marais wastaafu wamo humu, hili nitalifunika mpaka Mawaziri wastaafu siwezi kuwataja.
15) Afisi ya Makamu wa Pili Shs. 16,000,000/= Hongereni sana,
17) Chuo cha Utalii Shs. 8,000,000/=
18) Idara ya uchapaji Shs. 39,000,000/=
19) Mrajis Mahakama Kuu Shs. 8,000,000/= haijambo kidogo
20) Chuo cha Ufundi Karume Shs. 80,000,000/=
21) Chuo cha Afya Mbweni Shs. 23,000,000/=
22) Benki ya Damu Shs. 118,000,000/=
23) Bohari Kuu ya Dawa Shs. 97,000,000/=
Narudia tena Hansard zikae sawa, mpaka Septemba pengine wamekwenda kulipa Oktoba/Novemba sijui, lakini si rahisi hicho kitu.
24) Wizara ya Uvuvi na Mifugo Shs. 7,000,000/=
25) Wizara ya Elimu Shs. 17,000,000/=