Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,969
Baada ya Tanroads kuweka X nyumba zilizo ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro kuanzia Kimara Stop over baadhi ya watu wenye akili na waelewa wameanza kuondoka ili kupisha upanuzi wa barabara na ili kuokoa baadhi ya mali zao kabla tinga tinga halijafika.
Kwa maoni yangu nafikiri huu ni uamuzi mzuri kwani unasaidia kuokoa zaidi ya asilimia 80 ya mali badala ya kusubiri mpaka dakika ya mwisho kama ilivyowatokea baadhi ya wananchi wabishi kule Mbezi mwisho. Nawashauri wakaazi na wafanyabiashara waliomo kwenye nyumba zenye X waanze kufungasha virago kabla tinga tinga halijafika. Nawashauri wajiepushe ba wenzao wachache wanaowadanganya kwa maelezo kuwa wamezuia kwani hiyo haiondoi ukweli kuwa wataondoka hivyo ni vema wakaondoka taratibu na kuokoa mali zao. Mfano kuna mmiliki wa bar moja maarufu hapa Kimara Suka karibu na kituo cha mafuta yeye kaona isiwe shida kaamua kuondoka badala ya kusubiri vunja vunja ambayo inaweza kuathiri mali zake.
Mimi nimeona niwashauri kwa nia nzuri wananchi hao waondoke mapema badala ya kusubiri gharika kama ile ya Mbezi watafute maeneo mengine wakajipange upya. Ardhi haijaisha katika nchi hii.