GE2025 Wenje: Lissu alinufaika na falsafa ya 4R za Rais Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Wenje ameendelea kujimaliza, mwenyewe na kujiona mjanja

Tumika baba!
====================
Mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ezekiah Wenje, amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, jumla ya kesi 417 zilifutwa, ikiwemo kesi sita zilizokuwa zikimkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kama sehemu ya utekelezaji wa falsafa ya 4R iliyoanzishwa na Dkt. Samia.

Wenje ametoa kauli hiyo leo Oktoba 18, 2025, alipohutubia mkutano wa kampeni wa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Amesema anashangazwa na baadhi ya watu wanaomshambulia Rais Samia wakidai serikali yake imeminya demokrasia, ilhali ni yeye aliyefungua ukurasa mpya wa siasa za maridhiano nchini.

Ameeleza pia kuwa wakati CHADEMA iliposusia ruzuku ya serikali na kukumbwa na changamoto za kifedha, ni uamuzi wa Dkt. Samia uliowezesha chama hicho kuendelea tena kupokea ruzuku, hatua iliyochangia kununuliwa kwa majengo yanayotumika kama Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Mikocheni, Dar es Salaam.
 
Huu ni ukweli mtupu, hakuna kosa lolote mtu kuhama chama na hakuna ubaya wowote aliyehama kusifia chama chake kipya, ila asifanye makosa mawili
1. Asitoe siri za kambi wakati alipokuwa Chadema
2. Asiwe mtovu wa shukrani kwa kuisema vibaya Chadema, kuiponda, kuikandia na kuibagaza!
Karma itamhusu! Thread 'Angalizo kwa Wanasiasa hamahama; Japo ni haki yenu lakini msisahau fadhila. Kuweni watu wa shukrani, mtabarikiwa sana, vinginevyo karma Itawahusu!' Angalizo kwa Wanasiasa hamahama; Japo ni haki yenu lakini msisahau fadhila. Kuweni watu wa shukrani, mtabarikiwa sana, vinginevyo karma Itawahusu!
 
Huyu naye wenzake wanatangaza Ilani, watawafanyia ni

Huyu naye wenzake wanatangaza Ilani kwamba watawafanyia nini watanzania wakishachaguliwa yeye anaongelea habari za Lissu ambaye hata kwenye uchaguzi hayupo. Wanakuwa kama njiwa pori wimbo uleule kila siku "Chadema Lissu, Chadema Lissu" yaani wamekariri tu kwamba ukiwaongelea hasi chadema na Lissu basi vyeo vinakuja tu.
 
Huu ni ukweli mtupu, hakuna kosa lolote mtu kuhama chama na hakuna ubaya wowote aliyehama kusifia chama chake kipya, ila asifanye makosa mawili
1. Asitoe siri za kambi wakati alipokuwa Chadema
2. Asiwe mtovu wa shukrani kwa kuisema vibaya Chadema, kuiponda, kuikandia na kuibagaza!
Karma itamhusu! Thread 'Angalizo kwa Wanasiasa hamahama; Japo ni haki yenu lakini msisahau fadhila. Kuweni watu wa shukrani, mtabarikiwa sana, vinginevyo karma Itawahusu!' Angalizo kwa Wanasiasa hamahama; Japo ni haki yenu lakini msisahau fadhila. Kuweni watu wa shukrani, mtabarikiwa sana, vinginevyo karma Itawahusu!
Ndugu tuombe tuamke salama 29, naimani atahutubia kupitia Facebook kama ilivyo Madagascar....

Hasta la Victoria simpre " polepole "
 
Back
Top Bottom