Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,615
- 40,162
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ezekiah Wenje, amesema Serikali ya Tanzania ina wajibu na nafasi ya kikatiba kulinda maisha ya wananchi wake na mali zao, hasa wakati wa matukio yenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
Akizungumza katika mahojiano na Citizen TV ya Kenya siku ya Alhamisi, Wenje alisema matukio yaliyojitokeza Oktoba 29, 2025 yalikuwa ya kusikitisha, lakini hatua zilizochukuliwa na Serikali zinalenga kuzuia madhara makubwa zaidi dhidi ya umma.
Wenje alisisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru linaloamua mambo yake kwa kuzingatia maslahi ya wananchi wake zaidi ya milioni 60. Alisema haiwezekani kuruhusu kundi la “watu 5,000” kutikisa amani ya nchi nzima.
Wenje alikiri kuwa maandamano ni haki ya kikatiba, lakini akabainisha kuwa taratibu za Tanzania zinataka waandamanaji kutoa taarifa kwa polisi ili kupata kibali na ulinzi. Alisema kilichotokea Oktoba 29 hakikufuata taratibu hizo na matokeo yake ni vifo vya raia, askari na uharibifu wa miundombinu muhimu ya umma kama mabasi ya mwendokasi.
Aidha, alieleza kuwa Serikali imeunda tume ya uchunguzi ili kubaini ukweli kamili kuhusu chanzo cha maandamano, idadi ya vifo, kiwango cha uharibifu wa miundombinu na mali za binafsi, na hatua za kulinda taifa dhidi ya matukio kama hayo siku zijazo. Akisema hadi sasa hakuna takwimu rasmi za vifo zilizotolewa na Serikali, Wenje alionya dhidi ya takwimu za kupotosha zinazozagaa mtandaoni.
N.B Huyu Wenje 2020 Kaka yake aliuliwa kwenye harakati zza Uchaguzi wake Jimbo la Rorya