Wengi mmeguswa mkanuka

Wengi mmeguswa mkanuka

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
245
Reaction score
314
Ukisoma posts nyingi za wapenzi wa CCM utaona jinsi wanavyoshiriki kutimiza mipango ya wahuni wachache bila wao kujitambua. Ni hivi: toka 2015 kuna kikundi kiliamua namna nzuri kwao kufikia Ikulu ni kuichafua taswira ya Tanzania, viongozi wake na chama tawala nje ya nchi.

Mara tu baada ya uchaguzi mkuu zilizuka jitihada za kuishitaki nchi jumuia ya ulaya, UN na ICC. Kikundi hicho kilifikia hadi kutangaza kimewasilisha mashtaka ICC. Katika kufanya hivyo kilichagizwa na kesi ya viongozi wa Kenya pale ICC. Wakadhani kufungua kesi ICC ni jambo rahisi kama kufungua kesi Kisutu. Bahati mbaya kwao kikundi hiki kilikwama kote huko.

Kikundi hiki kikabadili mbinu. Kikaanza kupeleka hoja zao kwa kina BBC, DW, AI, HRW. Nia ilikuwa ileile. Kuichafua taswira ya nchi kimataifa. Nako huko hakukuzaa matunda tarajiwa japo mbinu hii bado inatumika na hiki kikundi.

Ikaanzishwa mbinu mpya. Kuipaka nchi sifa ya kukiuka haki za binadamu na mauaji ya raia. Yakazuka mauaji mkuranga, kibiti, arusha, na kwingineko. Hata bila uchunguzi wahusika haraka wakadai ni Serikali inahusika. Washauri wao waliwashauri kuwa mauaji ya raia husababisha nchi za nje kuingilia kati. Nalo hili likabuma.

Kikundi hiki kikaanzisha mbinu nyingine.

Kuhakikisha wanazalishwa wakimbizi bandia. Wakimbizi hawa bandia wako nje ambako kazi yao kubwa ni kuisema nchi yao vibaya. Walidhani wataweza kushawishi jumuia ya kimataifa. Mfano, licha ya kujua watanzania hawakubali ushoga kikundi hiki kikajinasibu kuwa kikitawala kitawapa mashoga. Nafsi zilikuwa zinawasuta ila tamaa ya Ikulu ikazidi imani. Mbinu hii nayo imebuma. Wakimbizi bandia wamejikuta hawana mvuto ugenini.

Sasa janga la corona limewapa fursa mpya ya kuendeleza azma yao ya kuchafua taswira ya nchi.

Ndio maana mmoja wao juzijuzi kadai diplomasia ya Tanzania imeharibika tena eti mno! Yeye na kikundi chake ndio wanaotaka kuzalisha picha hii: Tanzania inagombana na jamii ya kimataifa na jirani zake! Ndiye anaoongoza mkakati unaotaka kuonyesha kuwa Tanzania na JPM wana ugomvi na WHO, IMF, Kenya, Zambia, n k. !!!

Kwa bahati mbaya na kwa kutokujua baadhi ya wana CCM mtandaoni wameingia kichwakichwa! Utawasikia nao wanatukana WHO, wanamtukana Rais wa Kenya, Uganda, Zambia na Rwanda! Nao wanaonyesha eti hawa ni maadui wa Tanzania na wanamchukia JPM! Wameguswa wakanuka haswaaa!

Wengi hata hawaelewi kuwa Tanzania ni mwanachama hai wa WHO, WB, IMF na mashirika mengi ya kimataifa! Yaani kudai WHO ina ugomvi na Tanzania ni sawa na kudai Tanzania ina ugomvi yenyewe kwa yenyewe! Hawajui Serikali zina Balozi maalum pale Geneva Kwa ajili ya K na WHO! Serikali yoyote ikiwa na sintofahamu na taasisi ya kimataifa ambayo ni mwanachama kuna taratibu zake. Tanzania wala WHO hazifanya utaratibu wowote wa kusuluhisha "mgogoro"! Wapanga mkakati huu wanatumia uelewa mdogo wa baadhi ya wana CCM kufanikisha azma yao!

Ukweli ni kwamba Tanzania haina mahusiano mabovu na kina WHO, Kenya, Zambia, Uganda, EU, US, etc. Ukweli ni kwamba raisi JPM hajatamka popote kuwa ana ugomvi na kina WHO, Odinga, Uhuru, M7 na wengineo!

Mpanga mkakati huu na kundi lake wanafurahii! Wana CCM wenyewe ndio wanasaidia kudhoofisha taswira ya nchi kimataifa!

Kabla hujaamua kuzusha ugomvi ambao haupo tafakari sana! Uccm wako hauwezi kuboreka kwa kuizulia nchi maadui au migogoro hewa!

Diplomasia yaTanzania nje ya nchi ni imara mno. Taswira ya Tanzania kwenye jumuia ya kimataifa ni nzuri mno. Magufuli hana ugomvi na WHO. Magufuli hana ugomvi wowote na Kenya, Uganda wala Zambia.

Nchi kufunga mpaka ni jambo la kawaida mno na NI haki yake. Mmesahau tuliwahi kupiga kiberiti kuku ambao tuliona watatuletea mafua ya ndege? Tulikuja kuwa maadui? Walipouliza walielezwa na yakaisha.

Hata Tanzania ikihisi wazambia wanaokuja na TAZARA wanaweza kutuletea virusi itakuwa huru kuzuia safari za TAZARA! Kuna ubaya?

Tusikuze mambo kijinga!
Wenye akili wataelewa!
Lakini uko huru kuzulia nchi yako maadui hewa na magomvi yasiyokuwepo. Si ndio uelewa wako!
Tusisaidie kikundi kile! Msikubali kunuka mkiguswa!
 
MATAGA, haikusaidii kusema 1+1=4.. haikusaidii mbele ya wanahesabu wezako, sana sana watakuona kituko!
 
Wahenga walinena,.. "Mchelea mwana kulia hulia yeye".
 
Nahisi wewe Calvinkimaro ni Mchaga. Kama kweli wewe ni mchana anasema: sijawahi kuona au kusoma ujinga kama huu wako ukiandikwa na mchana sina yako. Wachaga Wendi wanajitambua. Siku nyingine Fuchs utambulisho wako


Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sio Calvinkimaro na wala sio mchaga una jingine la nyongeza?
 
Hiki Kiki si cha wahuni kimeharibu hata utaratibu wa vipimo maabara kuu ya taifa.
 
Jifunze kuandika kwanza mwandiko Kama wa mchattle au ulibashite masomo yako.
 
Mkuu kuhusu Tundu lissu kuna mbunge wa Chadema alisema ile ilikuwa ni inside job yani chama kilitaka kimpoteze

Huyo ben mimi simfahamu

Kuhusu aqwilina jiulize km Mbowe asingeandamana bila kibali huyo Mtoto angekufa?

Mtueleze yuko wapi Ben Rabiu Saanane,nani alimpiga risasi Tundu Lissu,kwanini watu wanatekwa na kupotea kwenye utawala huu?
Shutuma za Makonda zilizotolewa na Wamarekani kwanini hamkuzijibu?

Uchumi umeshuka,ajira hakuna,sukari imepanda bei,mnanunua wanasiasa wa upinzani,mlihusika kwenye kifo cha Aquellina bado mnataka watu wakae kimya!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuhusu Tundu lissu kuna mbunge wa Chadema alisema ile ilikuwa ni inside job yani chama kilitaka kimpoteze
Huyo aliyehongwa uwaziri kwanini Polisi wasianze kumhoji ili waanzie hapo na huyo mroto mwenye sura kama ya shetani aanzie hapo
 
Mkuu kuhusu Tundu lissu kuna mbunge wa Chadema alisema ile ilikuwa ni inside job yani chama kilitaka kimpoteze

Huyo ben mimi simfahamu

Kuhusu aqwilina jiulize km Mbowe asingeandamana bila kibali huyo Mtoto angekufa?
Mkuu; Hepuka kuweka hisia kwny mambo ya msingi mkuu

Mbowe ndiyo aliyeandamana..sasa kwanini mwanafunzi asiyehusika apigwe risasi!?

Kwanini ufyatue silaha za moto kwny maandamano ambayo sio threat!?(kwa waandamanaji hawana silaha za moto)

Tunachukulia simple kwa 7bu haya mambo hayajatukuta lkn km huyo binti angekuwa ni dada/ndugu yako ndo ungejua uchungu upo kwa kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijibu swali Chadema walikuwa na kibali cha kuandamana ?

Tambua kuwa sheria haina huruma
Mkuu; Hepuka kuweka hisia kwny mambo ya msingi mkuu

Mbowe ndiyo aliyeandamana..sasa kwanini mwanafunzi asiyehusika apigwe risasi!?

Kwanini ufyatue silaha za moto kwny maandamano ambayo sio threat!?(kwa waandamanaji hawana silaha za moto)

Tunachukulia simple kwa 7bu haya mambo hayajatukuta lkn km huyo binti angekuwa ni dada/ndugu yako ndo ungejua uchungu upo kwa kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtueleze yuko wapi Ben Rabiu Saanane,nani alimpiga risasi Tundu Lissu,kwanini watu wanatekwa na kupotea kwenye utawala huu?
Shutuma za Makonda zilizotolewa na Wamarekani kwanini hamkuzijibu?

Uchumi umeshuka,ajira hakuna,sukari imepanda bei,mnanunua wanasiasa wa upinzani,mlihusika kwenye kifo cha Aquellina bado mnataka watu wakae kimya!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbowe anayo majibu yako na hata kuhusu chacha wangwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaangalie neno la Kaisari vizuri, tumeagiza sukari kutoka Uganda, nyingine imepitia Bandari ya Mwanza na nyingine Bandari ya DSM kontena 20.
Logistics ngumu aiseee hapo kwenye zigo la pili
Waziri wake alisema iko kasumulo inatoka Malawi yeye anasema inatoka jinja sasa sijui tumuamini nani
 
Back
Top Bottom