Aishi na risasi 3 mwilini kwa miaka 11 baada Muhimbili na Bugando kutomfanyia upasuaji

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
1667370322893.png

Julai 6 mwaka 2011 ni siku ambayo hatoisahaulika kwa Kulwa Makasi (32) baada ya kupigwa risasi tatu, moja kichwani, mgongoni na kwenye paja la kulia anazoishi nazo kwa miaka 11 sasa.

Mkazi huyo wa Shibula jijini Mwanza kwa sasa anatembea kwa kiti maalum kutokana na ulemavu alioupata baada ya kupigwa risasi na askari polisi wakati wa operesheni ya kuwaondoa wamachinga katikati ya mji mwaka huo. Kwa ulemavu alionao, familia yake sasa inatunzwa na mkewe, Salome Peter.

Siku ya tukio, polisi kwa kushirikiana na mgambo walikuwa wanawaondoa wamachinga katika Mtaa wa Makoroboi na Kulwa anasema alitoka nyumbani kwake Mtaa wa Mabatini kwenda kwenye biashara zake ndipo alikuta watu wakikimbizana.

“Nilipofika Makoroboi nilikuta taharuki ya Jeshi la Polisi, mgambo na wamachinga. Nikauliza kuna nini, wakaniambia wamesema tusifanye biashara eneo hili, nikasikia sauti ya askari akisema wenye mizigo eneo hili waje waitoe,” anakumbuka Makasi.

Baada ya kusikia kauli ya askari huyo, akiwa na wenzake watatu, anasema waliingia stoo na ndani ya dakika tatu walisikia mabomu ya machozi yakipigwa nje.

“Tulitaharuki, tukaamua kutoka na tukaona watu wanakimbia, nasi tukakimbia kuelekea lilipokuwa Soko Kuu la Mwanza. Tukiwa tunakimbia tulisikia askari akitoa amri kwamba ‘piga risasi.’ Zikanipiga tatu,” anasema.

Kutokana na kutokwa damu nyingi, anasema alipoteza fahamu na alipozinduka alijikuta katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) cha Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando alikokaa kwa mwezi mzima lakini hakufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi hizo kutokana na ubovu wa mashine hivyo akapewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alikaa kwa mwaka mmoja bila kufanyiwa upasuaji, sababu ikiwa ni hitilafu za mashine.

“Vipimo vya Muhimbili walisema matibabu yangu kwa wakati huo hayakuwepo nchini hivyo nilihitajika kusafirishwa kwenda India kufanyiwa upasuaji huo,” anasema Makasi.

Matumaini yaligonga mwamba baada ya familia yake kushindwa kumudu gharama za usafiri na matibabu ambazo hazikumbuki kutokana na kupoteza karatasi yenye taarifa hizo.

“Baada ya kukaa muda mrefu hospitalini bila matibabu madaktari walishauri nirudishwe nyumbani,” anasema.

Kutokana na risasi zilizo mwilini mwake, Makasi anasema kuna wakati humsababishia hasira jambo linalomfanya aonekane mwenye tabia tofauti kwenye familia na kipindi cha baridi anahisi maumivu na vichomi jambo linalomkosesha usingizi.

Huku akibubujikwa machozi, Salome, mke wa Makasi anasema hakutarajia mume wake angekuwa mlemavu.

“Wakati mwingine nakata tamaa kwa sababu mambo yameniwia magumu mno, nawaomba mtusaidie. Naamini akiondolewa risasi mwilini anaweza kurejea kwenye utimamu wa afya ili tusaidiane kulea hii familia,” anasema.

Kauli ya Muhimbili, MOI

Alipoulizwa kutaka kufahamu kama Makasi alipokelewa, Msemaji wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema taarifa za mgonjwa huyo hazionekani.

“Nimeangalia kwenye mfumo sijaona kama alitibiwa hapa Muhimbili, nadhani alipofikishwa hapa alielekezwa kwenda MOI,” alisema Aligaesha

Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi naye alisema taarifa za mgonjwa huyo hazioni ingawa suala hilo halizuii mgonjwa kutibiwa.

MWANANCHI
 
LMAAOO! Jeshi lipi? hili linaloua watu bila sababu za msingi?
Ya kale yamepita, tugange yajayo, huko zamani yalikuwepo lakini toka rais wetu wa awamu ya sita aingie rais wa watu kipenzi cha watanzania hakuna tena uonevu hakuna viloba baharini yaliyobaki ni madogomadogo ya kinidhamu yanayofanyiwa kazi polepole hatimaye Tanzania yetu itakuwa swafi kabisaa.
 
Angekuwa ni mtoto wa kibopa wa serikalini Muhimbili na Bugando wasingetoa excuse ya kitoto kama hiyo
Sasa mkurugenzi, huyo mtoto wa kibopa wa serikalini anapata wapi huo muda wa kukimbizana na polisi kwa sababu ya umachinga!

Hao watoto utawakuta kwenye ofisi zenye viyoyozi, na siyo kule makoroboi Mwanza! Hao wanaokimbizwa na kupigwa risasi na polisi ni watoto wa maskimi!
 
Sasa mkurugenzi, huyo mtoto wa kibopa wa serikalini anapata wapi huo muda wa kukimbizana na polisi kwa sababu ya umachinga!

Hao watoto utawakuta kwenye ifisi zenye viyoyozi! Hao wanaokimbizwa na kupigwa risasi na pokisi ni watoto wa maskimi!
This could happen at any circumstances, unakumbuka yule Dada Akwilina aliyepigwa risasi katika vurugu za kisiasa?

Alikuwa ni mpita njia tu wala hakuhusika kivyovyote na mvutano wa CCM na CHADEMA lakini alikuwa mhanga.
 
Maskini wanajifanyia biashara kutafuta riziki hawana ata siraha mkononi lakini, biashara yake na familia yake kuitafutia ndo vimemfanya kafiks hapo, pole brother maisha tu huwa hayakai daima milele,utatoka hapo
 
Back
Top Bottom