Wema wa mtu haulipwi

Wema wa mtu haulipwi

Bonge La Afya

Member
Joined
Dec 19, 2016
Posts
35
Reaction score
83
Leo nilikuwa nafatilia moja ya kituo cha television huko marekani tajiri nambari moja duniani Bilionea Bill Gates aliulizwa na mwandishi mmoja wa habari kuwa anajisikiaje kuwa tajiri mkubwa zaidi duniani. Akajibu kuwa hadhani kama yeye ni tajiri namba moja. Akaulizwa anadhani kuna mtu anamzidi? Akajibu "Nadhani yupo mmoja" Akaulizwa ni nani?

Akasema "Nilipokuwa shuleni sikuwa na fedha. Kuna wakati nilienda kwenye "vijiwe" vya kuuza magazeti ili nisome tu japo vichwa vya habari. Kijana mmoja mweusi (black American) ambaye alikua ombaomba eneo lile aliniona Alijua nilihitaji gazeti lakini sikuwa na uwezo wa kununua. Akatoa kiasi cha pesa katika zile alizokuwa akiombaomba akaninunulia gazeti. Nilijaribu kukataa kwa sababu nilijua anaweza kulala njaa kwa sababu yangu, lakini alinisihi nichukue...

...Siku nyingine tena nilienda kijiwe kile na sikuwa na fedha. Sikutaka mtu yule anione. Hivyo nikapitia vichwa vya habari kimyakimya, na wakati naondoka nikaletewa gazeti, nimelipiwa na yule ombaomba. Akanitizama, akafurahi. Nikamtazama. Nikalia. Nikaondoka"

Mwandishi akamuuliza sasa huyo awezaye kuwa tajiri kuliko wewe wakati umesema ni ombaomba? Bill Gates akasema "mtu yule alitoa hata kile kidogo alichokuwa nacho ili kunisaidia. Hakujali kuwa anaweza kulala njaa, kukosa malazi, kukosa mavazi, hakujali kupoteza akiba yake yote ndogo aliyokuwa nayo ili kunisaidia. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi."

Mwandishi akamuuliza, kwanini usimtafute umlipe? Bill akajibu. Nimeshamtafuta, nimemnunulia nyumba, na kumpa dola milioni moja (kama bilioni mbili za kibongo), lakini sijaweza kulipa hata robo ya alichonipa. Mwandishi akamuuliza kwanini? Bill akajibu "kwa sababu mimi nimetoa sehemu ndogo katika kikubwa nilichonacho, lakini yeye alitoa sehemu yote katika kidogo alichokuwa nacho. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi"

Umejifunza nini?me nimejifunza wema wa mtu haulipwi.

#festongadaya
 
Usiseme Leo ulikuwa unasikiliza mkuu maana hii stori ya jamaa ina zaidi ya miaka 3 humu ndani.

Ila inafundisha.
 
Nimejifunza kuwa vitu vidogo vidogo vikifanywa kwa moyo wote bila kuangalia utalipwa nini baadaye huwa ana athari kubwa sana katika maisha.

Kutoa ni moyo si utajiri.
Na kutoa si lazima kutoka kwa tajiri kwenda kwa masikini, ila inawezekana kabisa kukawa kutoka kwa masikini kwenda kwa tajiri.
 
Kutoa kidogo kwa nia na moyo safi kuna athali kubwa kuliko Kutoa millioni ili utokee kwenye magazeti.
 
Leo nilikuwa nafatilia moja ya kituo cha television huko marekani tajiri nambari moja duniani Bilionea Bill Gates aliulizwa na mwandishi mmoja wa habari kuwa anajisikiaje kuwa tajiri mkubwa zaidi duniani. Akajibu kuwa hadhani kama yeye ni tajiri namba moja. Akaulizwa anadhani kuna mtu anamzidi? Akajibu "Nadhani yupo mmoja" Akaulizwa ni nani?

Akasema "Nilipokuwa shuleni sikuwa na fedha. Kuna wakati nilienda kwenye "vijiwe" vya kuuza magazeti ili nisome tu japo vichwa vya habari. Kijana mmoja mweusi (black American) ambaye alikua ombaomba eneo lile aliniona Alijua nilihitaji gazeti lakini sikuwa na uwezo wa kununua. Akatoa kiasi cha pesa katika zile alizokuwa akiombaomba akaninunulia gazeti. Nilijaribu kukataa kwa sababu nilijua anaweza kulala njaa kwa sababu yangu, lakini alinisihi nichukue...

...Siku nyingine tena nilienda kijiwe kile na sikuwa na fedha. Sikutaka mtu yule anione. Hivyo nikapitia vichwa vya habari kimyakimya, na wakati naondoka nikaletewa gazeti, nimelipiwa na yule ombaomba. Akanitizama, akafurahi. Nikamtazama. Nikalia. Nikaondoka"

Mwandishi akamuuliza sasa huyo awezaye kuwa tajiri kuliko wewe wakati umesema ni ombaomba? Bill Gates akasema "mtu yule alitoa hata kile kidogo alichokuwa nacho ili kunisaidia. Hakujali kuwa anaweza kulala njaa, kukosa malazi, kukosa mavazi, hakujali kupoteza akiba yake yote ndogo aliyokuwa nayo ili kunisaidia. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi."

Mwandishi akamuuliza, kwanini usimtafute umlipe? Bill akajibu. Nimeshamtafuta, nimemnunulia nyumba, na kumpa dola milioni moja (kama bilioni mbili za kibongo), lakini sijaweza kulipa hata robo ya alichonipa. Mwandishi akamuuliza kwanini? Bill akajibu "kwa sababu mimi nimetoa sehemu ndogo katika kikubwa nilichonacho, lakini yeye alitoa sehemu yote katika kidogo alichokuwa nacho. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi"

Umejifunza nini?me nimejifunza wema wa mtu haulipwi.

#festongadaya
Upuuzi mtupu! Ni yale yale ya "Toa ndugu ulichonacho" Ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom