Wema Sepetu kapatikana na bangi

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,654
6,277
Kamanda Sirro kasema baada ya kumuhoji walifanya upekuzi nyumbani kwake na kukuta kuna msokoto wa bangi na kifungio.

=========

Mrembo Wema Sepetu anatarajiwa kupandishwa kizimbani kufuatia tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi katika nyumba anayoishi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amesema kuwa Wema na mwenzake watapandishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na wa bangi kwenye nyumba zao.

Kamanda Sirro alisema kuwa upekuzi uliofanywa katika nyumba ya Wema Sepetu alikutwa na msokoto mmoja wa bangi pamoja na karatasi maalum za kuvutia bangi zijulikanazo kama ‘Rizla’.

Pamoja na Wema Sepetu, mwingine atakayepandishwa kizimbani ni pamoja Bakari Mcheni ambaye yeye katika upekuzi huo alikutwa na misoko mitatu ya bangi.

Kamanda Sirro alisema watu 10 watapelekwa mahakamani kwa ajili ya kula kiapo juu ya mwenendo wa kimaadili kutokana kutumia dawa za kulevya ambapo kwa ndani ya miaka miwili wasihusike na kutumia dawa hizo pamoja na kuripoti Polisi mara mbili kwa mwezi. Watu hao wataokula kiapo hicho ni Hamidu Chambuso, Rumeo George, Sideo Mwandigo, Khalidi Mohamed ‘TID’, Johanes Mansen, Said Masoud ‘PTT MAN,’ Rajab Salum, Lulu Chelangwa, Nasoro, pamoja na Bakari Kierefu.

Katika operesheni hiyo ya kusaka watu wanaojihusisha na dawa za kulevya walikamatwa watu 112 ambapo kati ya hao 12 ni wasanii Bongo fleva na Bongo Muvi.

Aidha katika operesheni inayoendelea, dawa za kulevya 299 na Puli 104 vilikamatwa.

Akizungumzia madai kuwa kuna baadhi ya watu wameonewa, Kamanda Sirro amesema kuwa watu wote waliokamatwa hakuna mtu aliyeonewa katika hilo na walikuwa wazi katika mahojiano

Chanzo: SwahiliTimes

=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
Yaliyojiri katikati ya mchakato wa upelelezi wa kesi ya wema
Wema kukutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini
 
Yaani mfanyabiashara wa madawa ya kulevya aliyetangazwa kwa swagger zote utadhani Pablo Escobar afu anakutwa na kamsokoto kamoja..??????
Afu wamejuaje ni ka kwake?
Hii ndio Tanzania.

Usipokutwa na kosa polisi utatafutiwa kosa, na mara nyingi watampa mtu kesi ya kukutwa na bangi, silaha au madawa ya kulevya ili tu wasionekane wameshindwa.
 
Back
Top Bottom