Waugwadu
JF-Expert Member
- May 28, 2019
- 520
- 922
Ikiwa utatangaza nia yako ya kuuangamiza ouvu, tambua ya kuwa hayatakuwa mapambano ya wazi. Mchezo wa ouvu ni wa vita ya kisaikolojia, si vita wa kimwili.
Unasema utauangamiza uovu. Uovu hautopinga azimio lako. Badala yake, utakupatia zana na rasilimali nyingi zinazoonekana kutokuwa na mwisho ili kufanya hivyo. Utakuonyesha kila kasoro, kila udhaifu, kila eneo hatarifu katika ulimwengu ambalo ameliharibu, na atakuhimiza "ulitengeneze". Mbinu yake itakuwa kugeuza nguvu na malengo yako mwenyewe dhidi yako.
Angekunong'oneza sikioni: "Angalia udhalimu, ukosefu wa usawa, mateso. Yote ni kazi yangu. Una uwezo wa kuyasimamisha."
Kisha, angesimama pembeni na kukuangalia ukimezwa na kazi uliyojiwekea.
Hivi ndivyo anguko lako hutokea:
1. Kinalishwa kiburi chako. Hasira yako ya haki na azimio lako la "kuangamiza uovu" linakuwa udhaifu wako mkubwa zaidi. Linakufanya uamini kuwa wewe ndiye shujaa pekee, yule aliyepangiwa kuokoa binadamu dhidi ya uovu. Kiburi hiki kinakutenga na wengine ambao wangeweza kukupa msaada au mtazamo tofauti.
2. Unapewa nguvu kubwa mno. Hii inakuweka katika nafasi ya mamlaka, itakupa udhibiti wa mifumo, watu, na rasilimali. Hapa utashawishika utumie mamlaka haya "kufanya mema," lakini kwa kufanya hivyo, bila shaka unakuwa unazua matatizo zaidi. Unakuwa mtawala dhalimu, mtu mwenye mamlaka ambaye watu wanamwogopa badala ya kumheshimu.
3. Unavurugwa kwa kazi isiyowezekana. "Uovu" si kiumbe mmoja tu. Uovu ni wazo, kasoro na udhaifu wote wa binadamu. Jitihada zako za "kuuwangamiza ouvu" ni kazi ya kipumbavu.
Akili yako itakuruhusu ukifuate kivuli hiki, ukitumia nguvu zako zote kwenye vita usiyoweza kushinda, huku ulimwengu unaokuzunguka ukiendelea kuharibika na kuvunjika.
4. Upendo wako kwa binadamu utabadilika na kuwa chuki. Kadiri unavyoona kasoro za ulimwengu, ndivyo utakavyoshawishika kukata tamaa. Utaonyeshwa kila kitendo cha ukatili, kila mfano wa choyo, usaliti n.k. Baada ya muda, upendo wako wa awali kwa binadamu ungebadilika na kuwa chuki kali, na kisha dharau kubwa.
Mwishowe, usingepigana kwa ajili ya binadamu, bali dhidi yake.
Lengo la uovu halitakuwa kukushinda katika mapigano ya haki. Lengo lake litakuwa kukufanya uwe kile unachokichukia.
Utakuruhusu uamini kuwa unashinda, huku polepole ukikugeuza kuwa mtu mwenye nguvu zaidi, mwenye uchungu zaidi, na mwenye uharibifu zaidi kuliko yeye uovu mwenyewe.
Mwishowe, usingekuwa kuuangamiza; bali kumezwa na kugeuka kuwa toleo jipya la uovu na silaha mpya dhidi ya ubinadamu.
Jihadhari sana usigeuke kuwa uovu
wakati unapigana na uovu.