Wema,Lemutuz na Mange. Je, wataingia serikalini?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,619
21,363
Katika hali isiyo ya kawaida, mkuu wa kaya amewaacha makada motomoto wa ccm mitandaoni ktk baraza lake la mawaziri ndg Lemutuz,dada Mange na mnyange Wema.Katika nyakati tofauti makada hao walionesha interest za kuingia bungeni ambapo lemutuz alitoswa bunge la Afrika mashariki baada ya kushindwa kujibu maswali,huku Mange akiishia mikononi mwa polisi baada ya kuchukua fomu ya kugombea Kinondoni wakati Wema akiwa wa mwisho huko Singida kwenye kura za maoni.Watatu hao walipambana sana mitandaoni kuhakikisha Magufuli anaenda ikulu hili na wao wapate nafasi serikalini in return.

Gazeti ili lilipojaribu kuuliza kwanini hawa watu hawakupata uwaziri mtu muhimu kutoka ikulu alisema kwa kifupi kabisa "these people they dont fit anywhere na hawawezi kuwa viongozi maana hawana sifa ya uongozi in every aspect"

Kwa hali hiyo inabidi Lemutuz aendelee sana kupost matangazo ya maziwa ya ASAS, huku Wema akishauriwa akomae sana kuuza lipstick na Mange aendelee sana kuchafua watu mitandaoni maana maisha sio rahiisi kama walivyodhania.
source Harambee newspaper
 
Last edited by a moderator:
Mange Ana deserve pongezi sio ubunge wa kuteuliwa,
Labda akpambane jimboni labda wananchi wanaweza mpa ridhaa
 
Huyo MTU muhimu kutoka ikulu anamaanisha wanasifa ya kutumika tu??? Haki ya shetani hii ndo CCM, wakisha kutumia huna thamani tena
 
Waendelee kupost shudu mitandaoni wapate hits nyingi kwenye blogs zao ili kina Dr Mwaka na Delina Group waendelee kuwadhamini.
 
"These people they don't fit anywhere" kiingereza cha Shigongo bhana. Sasa tabu yote ya nini na wasomaji wenyewe wa magazeti hayo Ni mahausi gero
 
Kwa mujibu wa "@kichwapanzii" wa instagram,Mange kesha pigwa talaka hivyo alikuwa anatafuta pa kutokea
 
Si vibaya wakawa mawazi wa JF maana idadi yetu huku ni kubwa tupo 350 elfu .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom