Weledi wa maprofesa wetu na maisha halisi.

Weledi wa maprofesa wetu na maisha halisi.

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
8,122
Reaction score
7,525
Nimeshtushwa na habari iliyomo kwenye gazeti moja la kila siku hapa nchini kuwa peofesa mmoja wa kitivo cha uchumi kasema eti ujio wa ndege zile mbili utasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa kasi kubwa.
Nimeshindwa kumwelewa katika maana hii, hivi ni kweli mikoa na wilaya zote zina viwanja vya ndege? Gharama zake yaani nauli ni rafiki wa watu maskini wa nchi hii? Zawezaje kusaidia kuinua uchumi kwa kasi kama niliyoyauliza hapo juu hayawezi kujibiwa na huyo prof.?
Prof, hivi ndege moja inabeba abiria 80 zidisha kwa 2 ni 160. Je, uwiano huo wa 160: 51, 000, 000 kwako wewe ni akisi la maendeleo ya kasi?
Maprof mmepotea na chanzo mnakifahamu, kutoka kisiasa siyo? Njaa za uteuzi zinawasumbua hadi mnatoa maoni yanayodhalilisha taaluma zenu.
 
Ni vyema ukaliweka wazi jina la huyo Prof, ili tufupishe mjadala. Au ni Prof. BB?
 
asiee maprofesa watanzani wachunguzwe na veti vyao pia vikaguliwe

'kupatwa kwa maprofesa"
 
Back
Top Bottom