Wekeza sasa kwa Scandinavia Express ijayo | Biashara ya Mabus

Kuna suala la breakdowns kwenye mabus ni kitu cha kawaida sana kipindi kile Scandinavia walikuwa wapo sharp sana kwenye kufaulisha abiria kwenye gari zao.
Kwa gari sita hakikisheni service za gari ziwe za uhakika sio za mashaka
Shukrani

4 zitakuwa barabarani Dar - Dodoma

2 zifuatazo zitakuwa special pia kufanikisha kufaulisha pale itakapohitajika

1 itakuwa inasubiri kubadilishana kwa safari ya siku inayofuatia Dodoma, ambayo tunaweza ipa ruti fupi pia maybe Dodoma - Kondoa/Arusha/Singida au Iringa then likageuza Mchana

1 Italala Scania kwa Check-Up Saa 4 itaondoka pamoja na gari la Dodoma lenyewe likiishia Morogoro,
na jioni litarudi na Gari la kutoka Dodoma, lenyewe likigeuza tokea Morogoro kuja Dar.

Kupokezana huku ni kuzipa gari mapumziko na muda mzuri wa check-up
 
🙏
 
Start small grow with experience.
 
Mtaji unaweza usirudi milele.

1. Kuna mkopo wa mabasi inabidi kampuni ilipe.

2. Kwa model ya hiyo biashara manake revenue kubwa itatumika kwenye operation costs mwishowe mnaweza mkatengeneza 0 economical returns.

3. Scandnavia walikuwa wanamilikiwa na wanasiasa. Asilimia kubwa ya mafuta waliyokuwa wanatumia walichukua kwenye yard za serikali. Ndo ilikuwa rahisi kwa wao kuvimba vile barabarani.

4. Nakushauri, anza kwanza wewe, fanya kwa miaka kama mitatu, pata uzoefu. Badae weka kampuni yako kwenye soko la mitaji kama DSE. Watu watawekeza wengi kwa urahisi wakishaelewa business model yako kwa vitendo.
 
Biashara ya Mabasi ni moja ya boashara ngumu kama tu ya usafiri wa anga, na ukiangalia staffu ndio shida na hiu ni nature, ulimsikiliza yule tajiri wa Summury kitu alicho elezeaga kuhusu Biashara ya Mabasi?

Unawekeza pesa nyingi sana lakini mwisho wa siku kuba uzembe mkubwa sana hasa kwa Madereva.

Biashara ya mabasi ni sawa na biashara ya ndege,

Ila ni wazo jema
 
Kwenye Chakula cha abiria tumia mfumo wa wanao tumia Mahoteli ya kitalii polini wa Lunch box

Ni kwamba usiku kabla ya safari unawauliza abiri wote kama kuna wale asii kula nyama, kama wapo wao wanakuwa na menu tofauti baada ya hapo Lunch box zinaandaliwa na asubuhi zinakuwa tiyali zinapakiwa kwenye basi, mnaqeza pata Lunch sehemu yoyote pembeni ya barabara au mkajenga kabisa kituo cha Lunch na mkaweka vyoo pale
 
Zinachangamsha safari ndio mizuka ya kibongo bongo
 
Hayo maelezo hayawezi kumshawishi mtu kuwekeza.
Kwanza lazima wenyewe wenye wazo muwe na kianzio au muoneshe taaluma yenu na uzoefu. Halafu muweke mpango wa biashara 'business plan'
Halafu muangalie sheria zinasemaje kuhusu kuitisha hisa au kuuza hisa bila kupitia soko la hisa.
Biashara ya usafiri ni rahisi kuanzisha ukiwa na mtaji ila ngumu kuifanya idumu.
 
Kitu ambacho wengi Wetu hatukifahamu ni kuwa kampuni hiyo ilianza miaka ya 1972 na kukuza jina hadi miaka ya 2000,

Siasa ama wanasiasa sio walioijenga kampuni, maana baada ya wao kuanza kuingia miaka ya 2002 ndiyo ilikuwa mwanzo la anguko

Hivyo basi ukirudia kupitia bandiko juu utagundua cost nyingi ni mficho kwenye bei ya nauli ikiwa na maana kila biashara uionayo hapo inajitegemea na inafaida yake ila as long zimeunganishwa kuleta better experience zinaonekana moja
Lengo ni kuhakikisha hatupotezi senti kwenda nje yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…