Wekeza kwenye malengo yako

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
156
168
Kuzipata pesa na kuzitumia nje ya malengo yako hii hukutengenezea majuto baadae kipindi ambacho unakuwa huna nguvu wala uwezo wa kuzitengeneza pesa kama zile za mwanzo.

Wengi hufeli katika kutimiza malengo yao lakini hufaulu starehe za maisha ambazo mbeleni huwaacha katika kilio kikubwa na kujuta.

Wengine husahau kabisa maumivu waliyoyapata kipindi wanatafuta pesa, husahau jinsi walivyoshindia mlo mmoja, walivyojiweka mbali na pombe sigara starehe za gharama punde tu wanapopata hela hutumbukia ndani ya starehe hizo na mbaya zaidi huaribu mwenendo wao wa maisha kabisa..

Tujifunze kitu kwa mtu mmoja aliejulikana zamani kama IRON MAN, THE BADDEST MAN ON THE PLANET hapa namzungumzia MICHAEL TYSON.. Akiwa na umri wa miaka 20 miezi 4 na siku 22 Tyson alishachukua mataji makubwa matatu duniani WBA, WBC, na IBF yote haya aliyabeba ulingoni tena kwa kuwashinda wapinzani kwa kichapo kikali.. Kipindi hicho Tyson alikua analipwa hela nyingi sana mpaka kufikia mwaka 2003 inasemekana kuwa pambano moja la Tyson alikua akipigana ashinde au apigwe anaweka kibindoni dola za kimarekani milioni 30 ambazo kwa hela ya kitanzania ni kama bilioni 65 na milioni 800 hvi, huo ulikua ni usiku mmoja wa Tyson alikua anaingiza hela hizo zote, na kwa maisha yake yote ya ulingoni amefanikiwa kujikusanyia dola za kimarekani milioni 300 sitaki uzibadilishe kwa hela za Tanzania maana utapata tabu sana kumfikiria Tyson huyu, ww jifunze tu kupitia yeye, maisha yake yake yalikua kama vijana wa leo tu, maana na yeye kipindi hicho alikua kijana kama sisi alutumia pesa zake kwenye kila aina ya starehe alipata anachotaka na kutumia anavyoweza hakujiwekeza kwa maisha ya baadae na familia yake maana aliona kama atapambana ulingoni maisha yake yote lakini haikuwa hivyo mwisho wake aliishiwa nguvu za kupambana akawa hana hela tena akaandamwa na madeni hadi akawa anaandaa mapambano kwaajili ya kumchangia alipe madeni.. Maisha yake yakawa ya kujificha kwa aibu
Tyson huyu alijitokeza mwezi wa 6 mwaka 2005 alinukuliwa akisema " Maisha yangu nimepoteza kila kitu, nmeshindwa maisha, natamani kuishi peke yangu mbali kabisa na maisha yangu"
Maisha ya Tyson yameharibika alipata pesa akashindwa kutengeneza pesa..

Iheshimu pesa nayo itakuheshimu zaidi.. Tyson hakuiheshimu alitumia vibaya anakiri alipata pesa na kutamani kila starehe lakini starehe zake zimemfanya abaki jina Tyson basi..
Vijana tujifunze kupitia makosa ya wenzetu ili tuweze kufanikiwa...

Siku zote pesa inatakiwa kutengeneza pesa
Iwekeze pesa kwenye malengo yako hata kama itakuchukua muda mrefu kuzalisha pesa lakini kuwa mvumilivu mbeleni utakula matunda ya pesa zako
Unapopata pesa kitu cha kufanya ni kutimiza ndoto zako na sio kutimiza matamanio yako.

By Jay Speed
 
nimependa naanza sasa na kuendelea tena na tena
 
Back
Top Bottom