Weka order yako sasa

Weka order yako sasa

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,109
Reaction score
53,632
ImageUploadedByJamiiForums1430901095.425907.jpg
 
Daa!!hii nimeipenda.Watu wmedhamiria kweli na hiki chama mwaka huu.
 




Ongeza Ubunifu.

Tengeneza
Aina fuatazo

1.Moja kama hiyo
2.Moja yenye Bendera ya Tanganyika
3.Yenye Bendera ya Tanzania.
4.Mchanganyiko wa Bendera ya Tanzania na Tanganyika kutegemea wapi unataka kuiweka kwenye nguo.

Ila Ubunifu umeenda shule hongera!

Mwisho usisahau mchango kwa Chama.

 
Safiiiiiii. Weka bei. Oda hafanywi bila kujua bei.

Elfu hsmsini seti nzima. Kuanzia mtandio, hilo gauni hapo, kikoi chake, kilemba.

Mnunulie FaizaFoxy anahitaji sana
 
Last edited by a moderator:
Ongeza Ubunifu.

Tengeneza
Aina fuatazo

1.Moja kama hiyo
2.Moja yenye Bendera ya Tanganyika
3.Yenye Bendera ya Tanzania.
4.Mchanganyiko wa Bendera ya Tanzania na Tanganyika kutegemea wapi unataka kuiweka kwenye nguo.

Ila Ubunifu umeenda shule hongera!

Mwisho usisahau mchango kwa Chama.


Ya tanzania inakuja mkuu??
 
Hivi Limumba wanaweza kutengeneza nguo nzuri kwa ile rangi yao ilivyo mbaya???
 
Rangi za CCM ni mbaya sijawahi kuona, hata nguo ishonwe vipi bado haiwezi kumpendeza mvaaji....

Wengi hawapendi rangi zilizokolea sana kama kijani njano nyekundu. Kidogo wangezichanganya kiustadi
 
Haya wabongo,
Hii ndiyo hofu yangu kubwa ya Wabongo na swala hili!
Nimeacha kuandika kwa muda ili nipate kidogo kusikia mawazo ya wengine na mmekuja na lenu sasa…Tunaounga mkono swala hili na sisi tunavyo vyeti feki!... jamani, kortini kisheria tayari mmeshindwa kesi kwa sababu hii ni dhana isiyokuwa na ukweli na upumbavu mkubwa kwa sababu hapa tunajadiliana hakuna aliyesema kiwango cha elimu yake. Kwanza mtu kama mimi Bongo sii chaguo langu kuishi kama nitakuwa na elimu ya juu kwa sababu hizi hizi - watu kukisia vitu na kuvifanya kweli kisha wanategemea kuwa msomi ndiye Mungu mdogo wa duniani..
Jamani, swala ambalo lipo ubaoni na mahakamani ni kuhusu viongozi ambao wanavyo vyeti toka shule zinazojulikana hali viongozi hawa hawakuwahi kusoma pale!. Mathlan kuna mbunge inasemekana ana digrii nne na moja kaipata toka Havard lakini ukweli ni kwamba kiongozi huyo hakuwahi kusoma chuoni hapo wala kwa kupitia elimu ya Mtandao. Kwa hiyo cheti chake kanunua toka mtaani.. Hii ndio kesi ambayo mimi nakubaliana nayo na huyo Sitta lakini sio kesi yenu nyie.
Kesi yenu ni kuhusu Chuo fulani kutokuwa cha kweli na mifano ndio hiyo ya Washington na Commonwelth. Ajabu mnatumia mifano ya vyeti vinavyozungumziwa kuhalalisha dhana yenu ya vyuo!. Hakuna kesi hata moja inayohusu chuo fulani kuwa ni feki isipokuwa kinachozungumziwa ni KUGUSHI vyeti vya elimu.
Matata,
Unaongopa unapozidi kudai kwamba Commonworth haikusajiliwa Virgin Island. Sababu yako kubwa eti hawana ofisi pale wanapodai kwamba ipo. Huu ni upuuzi kwa sababu usajili wa shule hizi nchi kama Virgin Island ni njia mojawapo ya kuepa kodi kubwa za Corp. Hawa jamaa wapo Florida na wanatoa masomo kwa njia ya Mtandao. Ni kweli kabisa inawezekana elimu wanayoitoa ni ya undanganyifu lakini hatuwezi kusema kwamba mtu aliyesoma kupitia mtandao wao, kagushi cheti. Marekani leo hii kuna shule za mtandao nyingi sana hata kushinda shule za madarasa na zote zimesajiliwa na zinatoa vyeti kama maji, hizo shule za madarasa juu magorofani ndio usiseme kabisa ziko kibao na zote zinatoa vyeti. Kuna vyuo vya madarasa unaweza kusoma kwa dollar 600 kwa semister nzima elimu ya juu na Wabongo wengi wamekwenda vyuo hivi hali chuo cha kawaida Marekani huwezi kukubaliwa hata kusajiliwa kwa hizo dollar 600. Na vyuo hivi vinatambuliwa kisheria na vyeti vyao sio feki isipokuwa ni jukumu letu sisi waajiri kuvikataa vyeti hivyo kama havitoshelezi elimu tunayoihitaji kwa msomi lakini msinambie eti msomi huyo ana cheti feki.
Kuwa na ofisi sio swala lako wewe kwani hata meli za mabaharia zimesajiliwa Liberia, Ghana na Virgin Island wakati havina ofisi za kufanyia kazi huko isipokuwa Athens, Greece. Hii haifanyi mashirika hayo kuwa ni feki.
Kyoma,
Labda hapa lugha zetu zinagongana na nitakwambia nachosema mimi. Kwanza kabisa -Tofutisha kati ya CHUO na CHETI.
Swala la usajili wa chuo ambacho kitatambuliwa na Department ya Education huko Mareakani ni swala la State. Kila department ya education toka state moja hadi nyingine zinatofautiana kisheria hii amini. Ndio maana Washington University wamekuwa wakihama state hadi state na pamoja na kuwa ni matapeli. Kuna shule ambazo zimesajiliwa Florida au,Oregan ambazo haziwezi kusajiliwa DC, NY ama Texas. Na sababu zake za kutosajiliwa zinatofautiana kwa kila hali toka mifano yako huko nyuma hadi ile ambayo inahusu national security na safety issue. Kwa hiyo lazima tuwe na tahadhali hata kuamini kwamba kila chuo kilichosajiliwa Marekani ama nchi ya nje lazima CHETI chake kitambulike Tanzania ama nchi nyingine wakitambue cha Tanzania. Hakuna sheria hiyo Kyoma na wala haitakuwa sheria kabisa kwani nafahamu VYETI vya vyuo kibao toka Ulaya havitambuliwi hapa hali vyuo hivyo vimesajiliwa kihalali na vinajulikana.
Kutambua chuo uhalali haufanyi cheti kuwa na uzito haya ndio makosa tuliyokuwa nayo Tanzania. Asilimia tisini na tisa ya VYETI toka vyuo vyetu nchini havitambuliki Marekani, Canada, Uingereza na nchi kibao Lakini kutokubalika kwa vyeti vya shule hizi za Tanzania haina maana shule hizo hazitambuliwi na National Accreditation Council ya Tanzania.
Na kama mimi leo hii ningekuwa ktk usajili wa shule Tanzania, labda robo tat ya shule zote mpya zisingepata kibali kwani ni wizi mtupu, hatuna vyuo isipokuwa namba kubwa ya kufurahisha IMF na World bank..
Mwisho Kyoma, Kuna zaidi ya vyuo millioni dunia nzima hatuwezi kutambua kila chuo na vyeti vyake kwa kupitia mfano wako isipokuwa tunatakiwa kuwa na chombo ambacho kinawatihani wasomi wote wa nje kwa fani zao pindi wanapotaka kufanya kazi ama kushika madaraka fulani nchini. Nilikupa mfano wa Uhasibu kwa sababu bila kupita mtihani wa Shaban, cheti chako cha Uhsasibu ni ganda tu ukutani. Na ukifika kwenye CGA watihaniwa wote duniani hufanya mtihani mmoja.. credit zako toka chuo kinachotambulika mathalan IFM ukitoka na NAD zote mbili hukubaliwa na board ya watihani. Kwa hiyo hapa wameondoa kabisa mpango wa kuwepo chuo feki. Tatizo la profession nyingine ni kwamba:- Board za mitihani zipo nyingi na zote tofauti. Mwanafunzi aliyesoma law Havard anakaa mtihani wa mwisho tofauti na yule aliyesoma Yale au UDSM kwa wakati mmoja. Phd ndio kabisa kwa sababu kila mmoja atachukua kile alichotaka kiwe mkondo wa elimu yake. Na mitihani inatofautiana kati ya mtu na mtu, chuo kwa chuo hadi nchi kwa nchi. Bahati nzuri Tanzania tunao utaratibu wa mitihani kutoka sehemu moja. Utaratibu wetu Tanzania tofauti sana na nchi nyingine, nchi za wenzetu hata shule za msingi tu mitihani yao haitoki sehemu moja ama shule zote kufanya mtihani mmoja, kwa hiyo hapa vigumu kusema unaweza kupima uzito wa elimu ya mtu toka chuo fulani. Pia labda ndio maana wenzetu hawana mpango wa kugushi mitihani - Hii ni advantage ya elimu yao.
"Yes, we can"
 

Attachments

  • 1430943935106.jpg
    1430943935106.jpg
    30.5 KB · Views: 191
Back
Top Bottom