Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

The Haves and The Have Nots.

"Nadya harusi lini?" Jamani hili swali silipendi hiliii. Na waulizeee watu wote dunianiiii nitalivumilia ila sio Vivi jamani. Akiuliza Vivi kama nachomwa kristapen, na anavopenda sasa kuniuliza hilo swali kutwa mara 890920000. Asinione lazima aniulize, na akishaniuliza mtasema labda imetosha akimuona mtu tu lazima aianzishe tena hii topic. Wakutane n Dr Square Stella sasa, utachoka wewe msomaji. Huyu muhenga Dr. Stella anavojishaua na hio ndoa utasema kaolewa na miaka 15 vile kumbe kaolewa kizee mpaka makeup ilidundaaa sura ilivomkomaaa. Kwanza Dr gani shangingi shangngi hio PHD yake naitilia mashka makubwa na hio Medicine ndo na mashaka ni Dr. Mwaka. No offense waliosoma nae wanasema Stella kichwaaa hatariii. Balaa lingine lile. Ila ndo shangingi kashindikana. Mtu ana miaka 48 afu kazaa kweli jamani kama sio ushangingi nini huo?

Vivi ndo anani nyongonyezaaa maini yoteeee. Yaani ananimalizaa. Kwanza kadogo kadogooo, afu kameolewa kadogo kadogo na kijana mdogo mdogo mwenye pesa zake, na anampenda ni balaaaa! Full package. Wakati anamuoa walisema kafata pesa ya baba mkwe, maana ana kisuuu mzeee wa Vivi sio cha mchezo mchezo. Manake alimuoa mdogo kama sio 22 basi 23 kijana alikuwa kama 27 afu hana kitu. Mzee mwenyewe hakufurahia ila Vivi akabeba mimba kukomeshaaa mzee ikabidi tu apokee mahari fastaaa.

Ever since their life has been everything i wished for and dont have. Stella nam mudu maana kazi ndogo sana kumnyamazisha namuuliza tu wewe uliolewa na miaka mingapi? Atajikanyaga kanyaga hapo Vivi atamjibia 38. Na mwambi i am 30 bado miaka 7 so nipumzishe kidogo, rekodi yako bado sijaifikia. Vivian namwambia tu nitafutie shoga angu mume, nahaadhirikaaa mwenziooo. Basi nikimwambia hivo ndo anajiona ana bahati duniani hakunaaaa

Honestly ndugu msomaji niko kwenye kona, tena kona hio ya kitongaaa. Raia zimenikalia kooni kuhusu ndoa kama sijui wana hisa kwenye hili papa langu. I just dont believe in marriage. Ukichangia sina bahati kabisaaaa niwe tu muwazi ndugu msomaji. Nikimpenda mimi mwanaume mjue ana watu maana sio mtu. Na mimi ushindani siweziii. Yaani nina nuksiii tu, wanaume naowapata mimi wa hvyo hovyo tu afu broke ass. Balaaaa tupu. Wenzangu wanaweza hata kukaa wakajivuna wanaume wa maana nimewapata ila bahati nimechezea mimi niwe tu muwazi sijawahi kubahatika zaidi ya majaribuuu tu.

Unlike Stella the Genius, and Vivi the spoiled brat, mimi nimetokea familia ya kimaskini, ya mama na wadogo zangu wa 3 wanao nitegemea mimi kila kitu. Nime fight sanaaa, nimetumika sio kidogo na hao hao wanaume kufika hii level ya maisha niliofika kukaa meza moja na kina Stella na Vivian, nime hustle sanaa mwenzenu. Navosema sio genius unaweza kudhania labda napata divsion 1, mimi ni division 3 form 4, na 2 form 5, chuo nimepiga pass tu mwanzo mwisho ndo mumini kwamba bila kufosi kingi nisingetokaaa kimaishaaa.

Baba angu yupo sanaaa, ila nae maisha ya kuunga unga tu, ana mke mwingine, na watoto wengine atajijua na balaaa lake. Mkosi juu ya mkosi wa wanaume kukanifanya niamua sasa kuwa single kwanza mpaka atakapotokea Mr. extra ordinary ambae ataushika mtima wanguuu. Low key nishafanya umalaya sanaaa, nimenufaikaaa, sahivi nimepewa kitengo marketing manager, nakula kiulaniiii, nawapa mama na wadogo zangu maishaaa. Mdogo wangu wa kike ashaolewa, wa kiume ana kazi yake, mama nae eti kaolewa tena kapata mzee mwenzie wa kumliwazaa, nae ana watoto wakubwa kama sisi wanaliwazana.

Kama kuolewa mama angeolewa mda sanaa, sababu katulia afu mzuriii sanaa, nasikitika kufnana na baba yangu sanaaa, sema hakutaka kuolewa sababu ana amini baba wa kambo si baba. Akaamua kulea wanae kiugumu ugumu maana anasema wanaume hawaaminiki kabisaaa. Kukimbilia ndoa mara wanao wana bakwa na huyo mume wanafanyiwa vitu vya ajabu akasema ataolewa wote tukiwa na maisha kama hio riziki itajitokeza. Na kweli ikajitokeza kwa huyo mzee aliefiwa na mkewe.

Navosema sina bahati mnaweza jua labda nina kiburi au nachagua sanaa, ofcourse nachagua kidogo lakini. Mwanaume wa kwanza mimi kumpenda alikuwa jirani yetu mmoja wa kishua flani, nilimpenda mpaka nikimuona naishiwa nguvuuu kwa furaha ya kumuona tu. Nakaa dirishani ili apite nimuone. Siku nzima mpaka mama ananitukana wewe vipi kama msengery aliekosa soko kwenye hilo dirisha. Nili sali, niliomba Mungu mimi, nilifanya yoteeee, ila nasikitika kuwataarifu ndugu wasomaji THEE GUY NEVER NOTICED ME TO THIS DATE. Nikaja kupotezana nae na kuja kusikia kawa mvuta bangi sijui sina uhakika

The second guy i loved, was stingy, afu ananiomba pesa. Tuko chuo wote mi pesa natoa wapi? Plus macho juu juu kwa wasichana wenye pesa. Nilijitahidi sanaaa ndugu msomaji ila nasikitika i was too broke for the relation to work. Alini stress sanaa mnoo mnooo. Msengery mnyamwezi yulee simtakiii simtakiii mpaka kesho. Sikuwahi kula hata 100 yake. Aende tu salamaaa. Kama sio mkosi nini?

Nikaja kumpenda boya mwingine, malaya malaya tu, uhusiano uligubikwa na fumanizi za kutoshaaa, nikajikongoja hivo hivo tu, akaja kuoa mtu mwingine. Nilimfanyia matukioa lakini, hio story ya siku ingine tena. Ila inshort sikuambulia kitu napo. Sio kulogwa huku jamaniiii?

Nikaja kumenda kaka mwingine nae choko tu, malaya malaya, macho juu juu tu. Afu mi akili zadarasani sina ila kumsoma mwanaume na kumfumadakika tu. Nikaona foleni kubwa, kutiana janaba tu nikajiweka pembeni kwanza nijitafakari hili gundu mbona zitooo hivi. Wanaume 4 in a row na wote sio riziki kweli jamani ndugu msomaji? Sio kulogwa huku kweli?

Hao ni watu nilio wapenda mimi, kuna walio nipenda wao, nikabanana tu hapo hapo na kujinufaisha kidogo tu ndugu msomaji sio snaaa. Kati ya wote kuna mmoja mpaka kesho ni best wangu. Alikuwa ananihitaji mda nikawa simtaki hana kitu mie wa kazi gani. Ile misenge mingine yote nimeambulia kunyosolewa tu. Hamna hamna mara ikawemo akaja kutoka kimaisha katika dili dili zake anazozijua yeye mwenyewe akaja kunitafuta na nilikuwa nimechokaaa sio kidogooo. Akaniweka kwenye ramanani. Nikasema huyu naolewa nae.

Siku napiga simu akapokea mwanamke, na mtoto analia akasema anaoga. Kumbana mbanaa sanaa ndo kusema oooh sijaoa ila na mtoto. Muongo muongo nae, nikapeleleza nikajua ana mwanamke ana kaa nae na wamezaa mtoto ndio. Akajisemesha hampendi sijui nini ilitokea ndo maana kaja kunisaka after so many years. Nikalainika tukawa na mahusiano kabisaa na jua siku yoyote yule mwanamke atatimuliwa niolewe mimi. Subhna Allah!

Kila siku anaomba mda zaidi a solve hio issue, kuja kustuka yule mwanamke kazaa mtoto mwingine wake tena. Nikajua hapa changu sinaaa, natumika. Sio haba hapa sikutumika bureee, huyu kaka anajua kuhudumia mnooo. Alinipa kiwanja nashukuru Mungu akanitafutia hii kazi, akanifungulia miradi kama mi 4. Kweli ananipenda toka moyoni sema ndo hatukuonanan mapemaa. Akanitibua vuziii zote kuongeza mtoto na mkewe, yani alinitibua kwa kimbungaaa cha katrina.

We parted ways but we are still friends ila hamu ya kupenda imekula kwangu, wanaume siwaamini hata kwa kuwatania kabisaaaa. Sahivi nikipiga mechi nipewe changuuu kabisaaaa ndo mengine yafuate. Na mechi zenyewe kupiga mara chache sanaaa. Nimekuwa kama hanisiii. Sio mtu wa pombe, sio mtu wa sigara, sio mtu wa vi ben10. Nipo nipo tu hata sijielewi. Na hata sio mtu wa wanawake vile vilekama sio hanisi ndugu msomaji mi mtu wa aina gani? Vuzi unaweza isha mwaka sija nyoa namnyolea nani?


Nikimpenda mwanaume siku 2, ya 3 lazima aje kunitibua vuzi zoteee. Hawa short time nimepita nao si kimasihara, Naumia kweli maana sio maagizo ya Mwenyezi Mungu kuishi hivi ila nifanyaje ndugu msomaji??????????? Watu wananichukuliaje sijui, maana sionekani na mwanaume, wala mwanamke mwenzangu basi ijulikane moja kwamba flani yule msagaji, niko niko peke yangu kama jizi vile hahahaaaaa sieleweki sielewekiiii.

Wenzangu wana stress wapate mume, sjui mtu awape jina lake, sijui mambo kibao. Mi natafuta something very simple nipate tu mtu tunae elewana baaaaaaaaaaaa! Anijue mimi Nadya nataka nini na mimi nimue anahitaji nini, tuwe tu soul mates baaaaaaaaaaasssssss. Hilo karatasi wala sinahaja nalo, huko mbali sanaaa, hizo level za juu sithubutuuu wala kuchungulia humo.

Nikiona mtu anapata mtu wanaelewana ana break up kisa harusi hamna, najisikitikia, laiti mimi ningepata hata kile kidogo asichokitaka mwenzangu mbona ningekuwa mwenye furaha sanaa. Kupata tu hata bwanaaa, ana jali Nadya kala nini, wapi, kalala wapi, awe mwaminifuuu na ametuliza akili kwangu mbona ningesoma misa ya shukraniii.

Wapiiiiiiiii! Imefika stage naongea mwenyewe kwangu upweke. natizama movie najisimulia mwenyewe. Yani kuongea mwenyewe tena sio kitu cha kujishangaaa. Sijibaniii naongea hatalisaa lizima. Nifanyaje sasa. Nawaza kama nisingekuwa mtu wa morals na virtues ila siwezi kudanganya mwenzenuuu. I just cant be selfish enough to play with some ones emotions just like that.

Zamani kina vivi wakinitania roho inaniumaaaa ila sahivi nishakuwa sugu, mda mwingine utani naanzisha mwenyewe, msejaaaa.

ITAENDELEA KESHO SAA 4
nisifikie stage ya Nadya jameni ...i feel her...
 
Uliposhikwa shikilia mama, ukiringa yatakufika ya Nadya
umesema kweli kabisa,tatizo sio kuringa,inakua ngum kama hakuna hisia za kumkubali mwanaume.waeza hisi kero zaidi ya mapenzi ukiamua kujikaza kushikilia uliposhikwa.
[HASHTAG]#reality[/HASHTAG].
 
Living to the expectation. Queen V.

I am queen V. The queen herself, the legend, the real life barbie. Sio kazi ndogo kabisaaa kuwa mimi. It is more than anyone can manage. I am full package. People wish to be me, but they dont know what they are wishing for. Nawaaambiaaa.

You might think i live this life cause my pops is loaded ila hapana. I always wanted to marry a proper guy, who can give me a proper life, and i can enjoy the rest of my life properly. Being my pops daughter it was supposed to be piece of cake, cause a lot of family friends live proper lives, and i am a beutiful girl so money was supposed to follow money blah blah but it didnt.

I was raised to be a wife and a mother nothing more, Daddy princess nothing more. People were always nice to me, or us with my sisters and brothers, matter of fact they were more nice to my dady's money. I dated couple of guys from the clans you and i know are loaded. It was always either the guy comes from London or New York and his pops is involved with pops either way. The guys were extra nice, nikienda ma kwao mama zao ndo extra extra nice kwangu mpaka naona wazi wazi hapa pesa ya mzee inaabudiwa.

Kosa nikifanya mimi naombwa msamaha. And it was always speak to your pops about this for me, talk to your dad about this, always using me as laverage ina a baragain to get on the better side of pops. Watu wanasema bwana wewe hupendwi inapendwa pesa ya mzee wako. Acha simu za malalamiko umenichukulia bwana angu sababu ya pesa ya mzee wako, Mungu atakuulani nakwambia, si mnatumia pesa zenu kutuonea maskini. Utalaaniwa Vivi na uzao wako wote. Mapicha picha sasa wakati the guy swore he was single on his dads grave. The hustle is real.

Nikaacha kudate and i really wanted to marry young sababu home, gate kaliii sanaa, na dada alizalia home, so dad was super disapointed akaongeza ulinzi, i just wanted to do dad proud. Ushaona mtu anataka harusi na hataki kudate. Vikaanza vita vya kutolewa barua na watu wa ajabu ajabu wanaotaka favors na mzee.

Hakuna mtu alieniumaaa sanaaa kama Side. Nilimpenda sanaaa, na alikuja na gia anataka kunioa. Na side mdigo wa Tanga anajua mapenzi, kubembeleza, kudekeza, aliniganda kama luba. Side was young but he had already washed his hands so he dined with the kings. Alikuwa anapiga kazi na zmee sanaa na anaaminika. Na kilichonitia utambi, hakuwa mtu naemjua maisha yangu yote. Design aliibuka tu. Siku ya kwanza ameniona akaniambia nakupenda nataka nikuoe.

Hakutaka dating wala nini, akaleta barua. Mzee alimkataa akasema Side kijana wa mjini, level zake mishangingi ya mjini kama Nadya ila sio mimi. Mi nikangangania posa ipokelewe. Mzee akaipokea kwa roho safii tu mtoto akililia wembe mpeee. Nikawa obssesed na harusi hakuna mfanowe.

Kumbe Side kutoa ile pesa akawa anaitumia kama laverage kukopa pesa kwa mzee kila siku. Anadai kayumba. Mzee anachukulia kama mkwe wake kayumba anampa tu pesa. Na Side anazidi kuyumba. Akampa full bail out. Sasa kuna Mzee Issa ni right hand man wa mzee tangu tunazaliwa. Akawa design kamstukia Side. Akapeleleza na kujua Side ana mke wa kiarabu yuko Oman na anawapururaaa hao waarabu sio kitoto. Ndo maisha yake hayo. Kuoa au kuposa kwa matajiri aanze kuwachuna mapesa.

Wakawa wanataka kuizima hii ishu kimya kimya nisijue. Wakamuweka wanted, wachaga nyoko wale, wakamfata na bunduki akarudisha baadhi ya pesa na zingine analipa kidogo kidogo mpaka kesho. Mi sikujua chochote nikipiga namba ya Side haipatikani. Nikaanza kupata hofu.

Siku niko mjini nakula restaurant tena peke yangu, mara wanaongelea kuhsu Mzee wangu. Mzee mwenye ma bus flani,bintie yake si aliposwa na Side huyu mwarabu wa kariakoo. Oooohhh, kamchunaa sio kidogo. Kaja kustuka kampa zaidi ya million 300. Juzi wamemfata na bunduki kumtikisa karudisha 100 tu, zingine wameandikishana. Yule Side falasi sanaa, angeendelea kuwapurura waarabu tu, kavamia wachaga wale pesa zao yenyewe chimbuko lake ujambazi atawaweza.

Kidogo nizimie. I felt so much shame kumuingiza baba kwenye upuuzi kama huo. Nikasema sitaki tenaaa mwanaume anaenijua mimi nani wala natokea wapi. Ulipita mda sanaaa. Tatizo chuo wanajua mimi nani kila sehemu nayojulikana wanajua mimi nani.

Siku mtu dada yake akawa anaumwa tuko chuo mwaka wa 3. Akaniomba lift nimepeleke. Nikampeleka sasa uswazi gari haifiki. Mnapaki mnatembea. Nikaenda mpaka hapo. ukamuona mgonjwa na nini, hali yake ikawa sio nzuri. Akasema kuna jirani yake alimkopesha alfu 20, tusiondoke hatumpatia hio pesa. Tukakaa kidogo ni nyumba ya kupanga wana share upande, huyo muhusika yuko uani..

Tukaenda kupeleka hio pesa, kwa nje kaanika sare za jeshi, tukaingia tukamuona kijana almost makamo yetu. Tukataka kumpatia akagomaaa. Akaomba namba zetu maana mgonjwa ikiwa vovoteatujulishe. Shosti akamptia ya kwake, mimi nikanunda. Sio type zangu kwanza, kabisaaa. Mambo ya kurushana vichura chura sio.

Akaanza kusumbua apewe namba yangu. Shosti akataka kumwambia mimi ni nani na achukue time. Nikamwambia wewe usimwambie mpe, afu mi najua nitamfukuza vipi, kumbuka anakuuguzia dada yako, shemejio mlevi mbwa. Sasa ukimtibua vuzi ataeteseka mgonjwa. We nachie mimi nimlainishe.

Akaanza hi, sijui nini. Nikamwambia mimi sina pesa, kwanza sina wa kunisomesha kwetu kijijini na mambo kama hayo mradi tu kumkatisha tamaa, na mwambia vile vitu vinavokata nyege kwa speed ya 4G. Hahahaaaa! Nitumie 20,000. Anatuma kama jinga. Namwambia sasa suala la mimi kusoma, ananipa moyo atanisomesha.

Mwanzo nilianza kama mchezo tu, sasa baadae the lies were too deep, it was too late kumwambia all these were lies. Na uzuri hakuwa kwenye cycle yangu kabisaaa. Akitaka kuniona niko busy nasomaaa, nimesafiri hivo. Pesa yetu 20k nakula kama Hamisa mobeto kila baada ya siku 4. Akaanza kuwa anakuja chuo kuniona na nini.

Ballaa likaanza siku kanikomalia namba uje home, ni muhimu muhimu. Mmmmhhh! Nikatumia kikata nyege level one na shida ya 50,000 fasta. Akatuma akasema naomba uje seriously. Nikaanza mambo ya ada, mradi tu nisiende. Akasema suluhisho ya hilo ndo leo nimepata we njoo utajua huku. Hutahangaika tena ada.

Nikamwambia shosti ampeleleze dada yake kuna nini huko, akasema hadhani kama kuna issue serious, shoga akaniambia wewe neda. Kataa maneno usikate wito. Nikamwambia nisindikize. Akakubali. Tukapaki gari letu huku CCM, na kuchapa lapa mpaka huko uchochoroni. Ye akaingia kwa dada yake, mi nikawa najizoa zoa kuingia kwa kijana sababu nyumba za uswazi kila mtu anakukazia jicho unavojipeleka machinjioni.

Alifurahi kuniona nyie kama kaona keki sijuiii. Nikakuta form ziko pale juu. Akaniambia jaza kwanza hizi form. Nikawa nazisoma. Inshort ni form za mimi kuingiziwa mshahara wake kila mwezi. Nikauliza vipiii? Akasema kwa furaha i wish you could see him how happy he was, anaenda program ya UN Sudan 3 years. Kwa hio ananiandikisha mimi kama mwenza wake huko jeshini kwao. Mmmmmmhhhhh! Nikasema uongo wangu leooo uta ni Ufoo Saro mchana kweupeeee.

Nikiwaza nimwambie ukweli nawaza huyu mjeda mguu wa kuku anaweza hata kuwa nao hapo chini ya kitanda, akanimaliza na kunipiga muhuri wa gaidi la kibiti. Jesuuuuuuuuuus! In Nigerian voice. Nikawa nimepigwa bumbuwazi. Ananiambia utalipa ada, utasoma kwa raha you dont have to worry. Chupi niliovaaa nikahisi inanibanaa na kunikata mapajaaa, nikahisi K imekuwa kubwa chupi imekuwa ndogo ghaflaaa.

I felt bad about myself, really bad. How selfish. Kaka wa watu ashajaza form zake, ahaamua hatma ya maisha yake based on my silly lies. Nikaanza kuamini kweli nimelewa vibayaaa. Nikakata shauri nitamwambia akiwa Sudan huko, sahivi anaweza kuniua mimi, mgonjwa, shosti ikawa mambo ya Ufoo Saro bureee. Nikajikazaaa, nina roho ngumu nikijipangaaa. Nikaamua nimpe na mchezo ili asistuke kabisaa, wala asihisi kuna tatizo lolote. Nikaja zile form kw bashasha najiliza kwa uchungu huku nadai furaha.


Mjeda hataki niondokee, shoga ananitumia sms twende we shangingi utaombwa mambo sasa hivi sio kaka yako huyo. Kila nikisoma mazingira naona sio shirikishi kabisaa. Nikabadili gia angani na kuanza kujiseksisha, lengo nimpe kimoja tu cha fastaa nipate kujiokoa na nafsi yasi. Mjeda alikuwa na ugwadu kama Papii Kocha, na hivi pesa zake nimekula sanaa hizi buku 20.

Msitake niandike mengi ila mkae mkijua ATAKE KUIOKOA NAFSI YAKE ATAIANGAMIZA NA MIMI NDO NILIPOANGAMIA kujitia kupima kina cha bahari na mguu. Cha fastaa kikaishia kulala hapo hapo. Shoga anatuma sms mpaka saa 7 we malaya gari iko ccm kule shoga angu uswazi huku tutakuta balaa. Mda huo napigwa tu runguuu la kipepe mfululizo. Mjeda na hivi mtu wa mazoezi rungu la kipepe ni under estimation ya masacre ilionikuta siku hio. Kuondoka asubuhi na sikuagaaaa. Nilimwambia nachukua maji bombani, tena nimevaa bukta yake ya adidas na tshirt lake, sina sidiria sina chupi. Nina funguo tu na simu. Pochi niliacha.

Nikampigia shoga twende. Kufika wameiba power window, wamechomoa taa zote, wamechomoa tairi na rim zake. The hunger is real. Shosti tumwambie mjedaa, nikamwambia haina hajaaa. Tuokoe nafsi zetu, namtwangia Issa atajua la kufanya. Nikamsomesha tu Mzee Issa nilifata dudu sehemu sasa wamekomba power window, wamekomba tairi wamekomba kila kitu. Akauliza wapi temeke. Akasema zinakuja sasa hivi. Najua ananunua. Akaja kijana. Wewe kumbe mwanetu, samahani bwana hatukujua wa nyumbani. Wakaanza kufunga vile vifaaa. Mjeda anapiga simuu kwa fujo. Nikajificha kwanza.

Wakarudisha kila kitu, akampigia Mzee Iss bwana ishamalizwa issue yote. Akaanzakushoboka kati yenu nani mtoto wa mzee? Nikamkazia sisi wanawake wa Issa tu. Akatukana Mzee yule atafia kwenye nyuchi yule, haya shemeji zangu samahanini kwa usumbufu. Siku ingine mkipaki semeni tunaenda kwa Cobra. Tukaondokaaa. Namsimulia sasa shoga kuhusu form na rungu la comrade mjeda lilivonipata jana.

Akasema umeliwa kizamani sanaa shoga angu. Umekopwa kwa karatasi tu. Haendi UN wala vuzi la UN hilo chezo tu upagawe umpe uchi wa bureee. Utanambiaaa. Hamna kusmeshwa wala nini, ndo usha kopwa mchana kweupeee. Mi najua unamchezea mijokeri huko ndani kumbe unapigwa last card afu ukajaa manina zako. Huo uongos hoga angu, huku uswazi mwanaume akikwambia kitu jua tu anataka uchi waaaaa usikiwekee akilini. On the bright side uchi wako hajauchukua bado unao mwenyewe. Nyie mbwa kala mbwa. Alietoa pesa katoa pesa bandia, alietoa noti katoa noti bandia. Ngomaa droo hio.

Niliborekaaaa! How could he? Japo nimemchota akili sawa sio kunila kingi kizembe namna ile. Na nimempa mambo ya 3D nikijipa moyo he is different kumbe he is the biggest scammer of the all. Basi tu bahati yake, tena bahati yake anajua kufanya ila vinginevo ingekuwa hasara kamili. Haaaaaaaaa. Mpaka form zina mihuri ya jeshiii kabisa kmanina kweli kweli. Haaaaaaa.

Nikaanza kuchat nae kiugumu sasa. Ananiambi baby njoo please naondoka kesho, leo tulale wote, mafaaan kweli tena shubhamit mshenzi wahid anatumia karata ya jana kupata uchi leo. Mmmmhhh! Nikampa jokeri la bibi niko mwezini baby wangu. Nilitaka ajikoroge tu next time, wakati anadai anaondoka wiki hilo hilo kwenda Sudan. Akaniuliza siku ngapi nikajibu mi mgonjwa mgonjwa siku 10 zote niko mwezini. Akaniambia basi njoo tu.

Kilichonifanya niende ni lengo moja just to rub to his fase kwamba he is the jack ass nimejua kwamba kanitapeli uchi. Nimbananishe mpaka aseme ukweli kwamba yeye looser hamna UN wala nini. Nikajiandaa na mission ya Mr and Mrs Smith. Nimefika pale jioni sikwenda na gari wala nini, napakti zangu 4 za pad utanitaka tena yale makubwaa kabisa Free Style sitaki ujinga.

Balaa likaanza kaleta ndizi nipike kwenye mkaaa. Mmmmmmh1 Kucha yangu ya 70k naanzaje kuimenyea ndizi. American nails wanayoijua ile kucha watanielewa. Akasema natoka kidogo naja. Nikamuuliza dada, wapi kuna mama nitilie mzuri, akanielekeza. Nikaenda fastaa na hot pot nikarudi na ndzi zangu sahani tatu. Zimetiwa nazi shata shata huwezi kudhania.

Nikampa dada ile nyama, na minyanya na kila kitu nikamwambia mkaa wako weka humu. Nikabandika maji yanachemkaaa, yanakaukia najaza. Karudi usiku, hapo nimesogoa na dada mpaka basi, dada pia hajui mimi nani na kama niko vipi. Mda wa kula napakua tabasamu kubwaaa sanaaa. Kukiona chakula kile akastukaa kitu. Nikajuchuuza mzima mzima baby najua kupika nazi shata shata.

Akauliza umepika wewe, niko ndiooo. Mi mchagaaaa. Akawa anakula kimya kimya tu. Na mimi nakula mkavuuu. Akasema hujpika wewe. Nikamkazia nimepika mimi, tena nakuwa offended kabisaaa alaaa. Akasema hujapika wewe na hujui kupika kabisaaa. Nikasusa na kuacha kula nikanunaaa. Akasema mimi nimenunua ndizi bukoba, wewe hizi ni ndizi malindi za msohi hakuan upichi wala chemical equation upike malindi ziwe bukoba. Umenidanganya, na mimi sipendi KUDANGANYWA.

Roho ikafanya paaaaaaaaaaaaaaaaaaah! Nikasema nikitoka salama sirudiiii tena huu ujinga. Nikasema kweli sijapika na sijui kupika. Akaniambia kwenu hamna shida, ingekuwa kuna shida usingekuwa hujui kupika umri huo, na mimi nilikuona tu there was something about you. Chupi nikahisi inaweka nyufaaaa. Uzuri mama ntilie nawaamnia akashikwa tumbo la kuhara choo kipo ndani. Kaingia tu chooni, nikanyakua pochi moto. Najiambia wakitaka kunibaka namtaja tu Cobra. Saa 5 afu chocho za hajaaa. Niko speed ya 4g.

Kona ya kwanza, ya pili wana hawa hapaaaa wakani tight wakachukua simu, wakachukua hereni na cheni. Wakaanz akujadili tumbake au tumuavhe. Nikawaambia mimi mwanamke wa Cobra nibakeni tu ndo mtamjua. Wakastukaaa. Umemtaja nani? Cobra. Wakampigia simu, akasema mwanamke ananitwa nani? Nikawaambia mchepuko wa mzee Issa. Cobra akaongea naooo mda mrefu sanaa, wanalalamika wabakie hata na simuuu tu kwa usumbufu. Hmad mjeda huyu hapa. Sasa pozi alilotukuta sio la kukabana ila ni majadiliano.

Cobra yuko loudspeaker analalamika mi mwenye mwaamke namtaka huyoo sio kwamba simtamani ila babu Issa sio mtu wa kumchukulia mwanamke, bora umminye pumbu atakusamehe sio kumegeamwanamke, haina jisni hio penalty na vitu wanipe vyote, anawaambia huyu ndo demu wa juzi wa gari. Nikawa wa kwanza kumuona mjeda nikawaambia mjeda huyoooo. Wakasepa nikaokota vitu. Akauliza ulikuwa unongea nao nini na unajiamini nini kuondoka namna ile. Kafuraaa, nusu anichape makofiii. Anafsi kijeshi jeshi.

Nikakaza siendi naenda hostel. Anatumia ubabe twende nyumbani. Watakurudia tena wale wakubake na safari hii sitokei. Nikamjibu tu jeusir mimi nawamudu wale. Kama kunibaka ungekuta washamaliza. Anazidi kuvimba wewe mwanamke jeuri sanaa wewe, unanijibu mimi? unajua mimi nani? Kidogooo, kidogooo nimwambie wewe msengery tu utaniambia nini kwa taarifa yako mi flani. Ila nikakaa kimya. Akaanza kushuka sasa anabembeleza twende tukazungumze. Yale ya ndizi yameisha. Nikawaza huku cobra kanilinda mbele huko je? Cobra atanichokaaa. Nikarudiiii.


Njia nzima anjiongelesha kiupolee sanaa kama mtu. Kufika ndani kajaza maji kafunga mlango, afu kanikalisha face to face aka mana to man hio, ananiambia SIPENDI KUDANGANYWA. NASISITIZA SIPENDI KUDANGANYWA! MWANAMKE MUONGO SIMPENDI KABISAA KABISAAA. hYA UNA BLEED UKO PERIOD AU UONGO? Mmmmmmmmhhhhhhhhhh! Hahahaaaaa! Ukisikia k kukushuka ikaburuta chini na kuwa nzito ndo mda huo. Nikajibu ndio na bleed. Nimemtulizia jicho. Akasema nauliza mara ya 2 na ya mwisho. Nikajilaza nimesema ndio niko period. Akaanza kuchekaaaaa! Mwanamke mkavuuu wewe, bahati yako, nimekupiga mikwaraaa umekunya kunyaaaa. Usingekuwa period ungejisalimisaje fastaaa. Nikasonya tu kimya kimya.


Nikaamua na mimi kumtikisa Sudan unaenda mkoa gani? Akanitega Sudan unakujua wewe? Akanipata. Nikamuuliza safari lini? Akajibu umenichoka kiasi hiko? Nikapanda kitandani na kugeukia ukutani kulala. Nasema nikitoka leo sirudiiiii kutembea na hawa mbwa kachokaaa. Sirudiii. Nimekomaaa. Asubuhi nimeamka akaniwahi na mabusu tele tela kama sio yeye wa jana. Na mimi nikajikaushaaa. Nikaoga fastaaa, na kuaga. Akaniambia no tunaenda mahali. Nikamkazia naenda lecture. Akaanza kuomba unajua zile form nimemwambia mama sasa kasema anataka kukuona. Nikamkazia naenda lecture. Akaanza kupanic we huna shida ya ada, nendaa, na usirudi hapa. Nikajibu sawa. Nikachukua vitu vyangu na kutoka. Nikamuaga dada, alikuwa malangoni, na mjeda yuko mlangoni, akaniuliza lini tena mdogo wangu? Nikamjibu kwaheri hii ya kuonana dear, ndo nishapewa notice nisionekane tena hapa. Mungu atakujalia upone. Nitakuwa nakupigia simu. Mjeda kuona naharisha nje mambo yetu akazama ndani kwa aibu.

Alikuwa kanifika hapaaaa kooni. Afu design nishaanza kumpendaaa ile mechi ya juzi ilileta balaa kubwaa sana moyoni kwangu. Nae analeta mambo ya kisengery hasomekiii. Njiani nikasimama kwanza nikaliaaaa na mengi, afu nikaendelea na safari. Nimefika ccm nikakumbuka sikuja na gari. Nikaanza kutafuta bajaza, Porte ikawa inanipigia horn kwa nguvu inanifata nyuma, moyoni nikasema huyu choko angejua mzee wangu ana ma bus ya mkoani, Yutong tena nyingiii na gari naloendesha mimi angejipanga upya. Akaja kunisimamia miguuni. Nikawa namtazama tuuuu, uswazi porte ndo kila kituuu. Akashusha kioo, kumbe mjedaaa bwana ndo ana ki porte. Mmmmmh!

Nikamuuliza unasemaje, oooh ingiaaa bwana. Nikaingia cause sikutaka anijazie watu na kubwa sikutaka cobra anione nae. Alivokuwa proud na hio Porte hahahaaaa, ungemuhurumia. Anawasha full Ac. Nikamwambia naenda lecture kwa kumkazia so kama nishuke nishuke tu mapemaaa. Akawa ashabadilika kawa mwema tenaaa. Anajielezea ni muhimu kwenda kwa mama yake, sababu kaanda sherehe ndogo sasa nisipoenda itakuwaje. Nikamhurumia.

Kufika huko kwa mama mtu, hamna sherehe wala nini mjeda ni chronic lier. Nilichukiaaa sio kidogo. mama wa watua najitahidi kuwa polite, kachinja kuku na wali mweupe tukala, nikawa nimemuweka mjeda kiporo. Njiani akasema nakupeleka hostel kuna nyaraka muhimu sanaa za nchi hiiziko kwangu zinatakiwa na boss wake. Tunachukua tunaondoka. Hatukai. Nikawa nasema tukifika sishiukii maana nimeaga kwa matarumbeta hata siku haijapita narudi kulala kwa bwana si kujiaibisha huko.

Kaingia ndani kakaa kaaa, kakaaa. Nikazima gari, nikaipaki ccm n kumfata huko ndani. Akasema kumbe unajua ku drive, nilikutega tu. Nilikasirikaa mara 2000. Nikajua hamna cha nyraka wala nini alitaka tu kunirudisha nyumbani ki silencer. Akaanza kujisemesha mi naondoka jmosi, we still fighting mambo ya kijinga, leo tukae basi bila kugombana, mi hizo nyaraka sipeleki kama jeshi kuniukuza wanifukuzeee tu, i jsut want nikae na wewe, tu hug na kukisss bila kugombana. Akanionesha simu imeandikwa boss inapigaaa. Sipokei wala siendii, tukae tu the 2 of us. Aaiweka chini akenda kwenye friji, anastukia mi nishaipokea nasema haloo!

Mtu wa upande wa pili akasema /makibuyu huyu choko najua labda kapata matatizo haleti document kumbe anatomba mwanamke mda huu na kampa simu yangu mimi apokeee. Akafululizaaa matusiiiii ya nguoniiii. Nikastukaa na yeye kastukaaaa. Nikajizoa zoa na kusema samahani hapa chrage kibandani, kaiacha mda umeme hamna achajiwe nimeona unapiga sanaa. Simu ikakatwa. Nishajiaandaa na vitasaaa, nikajua iwavo iwavo nachezea vitasa.

Akasema you know what kesho kutwa naondoka and i said leo sitaki ugomvi, nataka tu , tukiss na ku hug tutagombana siku ingine, nakuweka kiporo. Hili soo nalia hirisha kwa siku hizi 2 kwanza. Ila ujifunze usishike simu yangu utaongea na raisi uzimie. Nikawa kimyaa nimevurugwaa. Akja kuni hug its okay. Mabusu moto moto hasiraa ikashukaa kidogoooo.

Nikaanza kumuuliza unamjua mimi nani? Anajibu nachojua wewe mwanamke wangu, japo muongo muongo nakupenda hivo hivo na shangingi shangingi pia maana mpaka gari unajua kuendesha na ada sina, hata kama ulikuwa mdangaji haijalishi ila kuanzia sasa ni mwanamke wangu ole wakeeee basha ataeshoboka hapo yaaani yaaani sitaki kusema sanaaa. Nikakaa kimya.

Shoga angu akapiga, wewe malaya mjeda kakumalizaaa, unajua kulikuwa na test ya ghafla nimekufanyia msengery wewe, umepakatwa kwa bwana huko mi nafanya test mbili mbili kubabake. Roho ikafanya paaaaaaah! Nikawaza mambo mengi sanaaa. Hili picha la mjeda sijui linakotoka wala linakoenda shule nimeitelekezaaa. Nikawa sielweiii yaani sielewi.

Nikasimulia uongo wa mjeda kwao kuna shreheee afu hamna lolote. Akauliza walipika wali kuku? Nikasema ndio. Akaniambia kiuswaziii shere hio kubwa sanaaa. Mmmmmmhhhh! Nikashangaaa sanaaaa. Sikutia neno wala nini. Huku mjedaa cassanova akajivunze mapenzi upyaaa. Mpaka maji kwenye friji ananifatia. Chakula anagizia tu. Mda aliotoka ni kwenda kupaki gari na alinifungia kwa nje.

Mi najua mda wowote najua anasema haendi kokote tuendelee na maisha mengine. Ikafika jmosi asubuhi anapaki kabisaa. Moyoni nasema kwa fix huyu ukute anaenda Arusha. Hahahaaaa! Namchora tu. Akaniachia crad ya bank na pass word nisingeshangaa codes za uongo. Nikapokea kimasihara. Ananiambia hizo hela zitazoingia tumia usijibane ila fanya ufanyavo mama umpeleke laki 3 kila mwezi zinazobaki fanya mambo yako, pendeza na nini lipia ada.

Ananiambia geto langu litunze, ikiwezekana hamia hapa achana na hostel, nishalipia kodi miaka mi 2. Najua mjeda anaenda arusha ananizingua tu. Nisindikize kazini naondokea kazini. Hapo ndo nilihakikisha mshenzi anaenda Arusha hana lolote. We sudan uondokee kazini sio airport kweli? Nikamsindikizaa. Nishaanza kumpenda so hata akinidanganya vingine nacheka tu moyoni.

Tumefika ananikabidhi porte uitunze naipendaa sanaa hiii gari yangu, gari ya ujana wangu. namba ya fundi wangu wa service hii. Uzuri kuendesha unajua so utaifaidi, haili mafutaa kabisaaa. Yaani ukinisalitiii, nimeweka ulinzi wa pentagon sitaki kusema sanaaaa. Ma kiss saa zima. Akasema nashukuru tumjuana kabla sijaondoka japo hatujawa na mda sana ila wewe ni mtu sahihi kwangu. Mmmmmmhhhhh! Nawaza kwa mikwara huyu kaenda tu hapo Arusha ananichagizaaa.


Nikarudi pale geto ndani ya porte, nikapafunga fresh na kusepa na porte ya mjeda. Nikawa na gari 2. Ila porte nilitokea kuipenda sanaaa, bai tu kuliko Rav 4 langu. Kilichokuja kufanya nijinyeee ni picha alizonitumia akiwa Sudan kweliii, kwenye combat, mbele ya vifaruuuu, serioulyyy!!!!!!!!!!!!!!!! Kumbe kaenda kweli Sudan and everything was real! Haaaaaaaaa!

ITAENDELEA KESHO
 
The Beauty and the beast! Mommy JJ.

Hello ndugu wasomaji! My name is Gift and i am a gift from God to this ungrateful world. You can call me Mom JJ. I am a proud mom, single mom or not, i am proud of my son. And he was not a mistake but a decision i made, correct or not it doesnt matter. My son my world.

Unlike other single moms, i am a rich single mom. I live in the west sides, i drive latest cars, mwanangu anasoma shule nzuri sanaaa. I am a lawayer and i have my own law firm. I make my own clean money. Huge money if i may stress. Which i splash all over, and it can buy me seat next to Stella and Vivian, baddest beaches in town. The platinum lifestyle.

I must confess i sleep around a little cause i love life, and i am enjoying life. Sina mibwana mingiiii. Na mabwana wawili tuuuu jamani hata ile level tu ya bibi zetu atleast mabwana wa 3 sijafikia. Nina bwana wangu mmoja aka bonge la bwana waziri ambae tunakutana mara chache ila hizo chache ni za msingi hatariiii kwenye uchumi wangu. Ananilipia ada ya mwanangu, huu mgari wa million 100 kanipa yeye, ofisi ile mjini kanipangia yeye na ana spend kwanguuuu sio masiharaaa kabisaaa.

Niliendaga nae Dubai kabla sijamjua mzungu wa roho, mpaka nikaanza kuhisi au free mason. Maana natoa macho kutamani ma designer staff anasema chukuaaa, chukua tu usijibaneeee. We chukuaaa, hivi vimewekwa kwa ajili yenu. Nilichukua shades za MK, $460 ananiambia chukua na za brown chukua na hizo Gucci. Nikasema mbona hatukukutana mapema, ningelalal na waganga wote Unguja mpaka Sumbawanga mpaka niipate pete. Bahati yake tena bahati ya mtende kuota jangwani.

Watu wangu wa karibuuu wanaomjua huyu bwana wanahisi labda ndo baba mtoto wangu, na wakiniuliza uliza navunga wanahisi katoto ka mheshimiwa so inawekwa under cover. Kumbe wangejua alienizalia ni mshenzilingi mmoja hana mbele wala nyumaaa. Nawaza siku ya kumpeleka mwanangu kwa baba ake mzazi naanzia wapi? Na nilivo mlea hovyo hovyo sasa. Mbona takondaaa. Ila baba ni baba ukifika mda ataisoma namba.

Ndugu msomaji sikufichi ila umbea sikati kwenye comments, na ole wako ujicomentishe mzazi mwenzie mama JJJJ weeeeee shika adabu yako ikushikeee na mshikamane wewe na adabu yako, ila mzazi mwenzangu ni ........................ nimeghairiiiiii kuwasimuliaaa mmzezidi umbea, labda mbele mbele huko kwa sasa tuongee mambo ya maana tupu. Bwana wa kwanza ndo huyo bonge la bwana Waziri.

Mwanaume anajua kufanya na kuspend mpaka unapatwa na uchiziiiii. Wanaume hawa hawafaiii kabisaaaa. Huyu waziri sikumpata zali la metali, nilikuwa single mother, nime choka chokaaa sina mbele wa nyumaaa. Kipindi hiko nina shoga angu ananisimulia mambo ya Mh jinsi anavompeleka shoga ake mwingine Dubai, kampangia aprtment mi naponda atakuwa anamlaaa Tigoooo lazimaaa. Anasema hapanaaa, Waziri Mzungu wa roho sanaa niamini mimi, hana michezo hio kabisaaaa.

Sasa mwanangu kaanza kuumwa moyo anatakiwa kwenda India, sina mavi ya India yaaani sianaaa. Baba ake mzazi hata msimuulizie atawatibua tu mavuziiii kama alivonitibua mimi miaka mingi iliopita. Nikamwambia shoga angu Monica nikutanishe na yule waziri bwana wa shoga akao, anaweza kunisaidia, ki JJ kitakufa Monica. Monica hatakiii na anakapenda ka JJ vile baba ake mbwa kachoka namlea mwenyewe kwa shida shida akaona katakufa kweli.

Akamwambia shoga akae, akagomaaaa. Kama chale zilimchezaaa. Nikakata shauri niende ofisini wizarani. Sikufanikuingia. Nikamzoa zoa Monica kesho yake twende wote, maana secretary anamjua Monica so tukaingiaaa. Nimefika najielezaaa, najimalizaaa sio kidogo. Yule baba yuko kimya. Nimemaliza akapiga simu moja tu Muhimbilia akaniambia nenda kule watakupa taratibu za kwenda India nishawapa maelekezo wamuweke kwenye list. Kuwa na amani tu. Tukaaga tukaondoka.

Nikaenda kweli nikakuta kapewa ufadhili mpaka wa mimi kwenda kukaa hotel, akatibiwa, haikuwa serious kama nilivohofia. So akapona haikutakiwa kurudi tena. Sio siri ule msaada wa yule baba ukanikaa rohoni vibaya mno. Baadae nikaenda tena safari hii secretary akaniacha nimuone. Kwanza akawa hanikumbuki kabisaa. Nikamkumbusha akasema aaaaaah, dogo anaendeleaje nilifatilia nikajiridhisha mmekwenda na mmepewa huduma nilio agiza hawajafanya uchachuaji. Nikashukuru na kujimalizaa hatariii. Baba mkavuu hajaomba namba wala nini. Nikaondoka mkavuuuu. Ananiambi ukihitaji msaada wowote as long as rafiki wa Monica njoo nitakusaidia.

Ukapita mda kama miezi 6 bado ule wema wake nasikia design sio vizuri kusahau wema mkubwa vileeee, roho inaniambi hujatoa kitu umefanyiwa hayooo, ukitoa je? Acha uzembe wewe. Nikaanza kumsumbua Monica namba ya mheshimiwa. Monica mgumuuu, akachoka na kelele za namba namba akaamua kuiiba kwa shoga ake akanirushia. Akaniambia wamekosana shoga alifumaniwaaa. Hio hapo ushindwe wewe kuilalia bahati ya mwenzio mlango wazi.

Nikawa namtext mheshimiwa kama utanihitaji kwa shughuli yoyote ile mi niko tayari. Hahahaaaaa! Shughuli gani yeye mtu mzimaaa. Akaniambia sawa, kwani una ujuzi gani? Nikamwambia mimi mwanasheria ila bado sijapata mahala pa kueleweka. Akasema kesho neda kwa MASHA ujishikize, uanze na kufanya bar exams nikiwa nakutafutia postion nyingine. Mmmmmmhhh. Asubuhi nikaenda kwa Masha nikajua najitoleaaa, naambiwa nitalipwa allowance sio za kitoto. Mheshimiwa akazidi kunivurugaaa. Ikapita miezi 6 niko kwa Masha nakula maisha tu.

Siku akatuma meseji mlete mtoto anisaimie sijakaona toka karudi India. Mlete huku Double Tree. Nikawaza sanaaa, kama anataka kunitumia kwanini aniambie niende na mwanangu? Sikuelewa kabisaa. Ila sikuataka kumkaidi boss wetu. Nikaknunulia nguo mpya, na mimi allowance za Kazini naweza kununua japo cream, nishaanza kungaa, suti zangu za gharama, vigauni sexy, lace wig kidogo naonekanaaa.

Kufika kule yuko na wanae design kama brunch hivi. Nikasema nikae pembeni nisipaparike. Akatuma muhudumu atuite. Tukaenda, nakunya kunya sio kidogo. Akawaambia tu wanae huyu rafiki yangu yuko kwa uncle Masha kule, mwanae ndo alienda India kipindi kile nilichowasimulia. Akaja mkewe sasa Mh. Akamwamba mimi nani, mwanamke ana roho nzuri yuleee hakuna mfanoweeee. Unaweza jua mke wa waziri nyodooo kibaoooo, walaaa, anambeba mwanangu na mnajua watoto wasivojua nafasi zao. Ikaisha ile brunch.

Ikapitamiezi 6 tenaaa akawa kaja tu pale alikuwa kaja kuzungumza na boss Masha, sasa wakati ashamaliza akaagiza niitwe, nikaenda, akasema vipi kazi nikashukuru, akasema Lau kaniambia mitihani umefanya poa sanaa, na anaona utaweza law firm yako. Najichekesha chekesha hapo sio kitotoo, yeye mtu mzima atamalizaa kila kituuu. Akazidi kunivuruga.

Nikarudi kwa Monica kumwambia bwana kama kuna mganga, mtaalamu, mchawi, mwanga, mshirikina, kigagula, mzee wa busara yoyote yule wa kuniweka kwa Mh, niko tayari kuwanga kutoka Tanga mpaka Pemba nikae kwa waziri. Monica kanitazaamaaaa. Akaniambia unapoteaaaa. Namwambia Monica atanichokaaaa atanishauuuu, nakuwa mzembeee, sijiongeziii mimi Monnny, najibwetekaaa, waziri kajiongezaaa sanaaa, tena mnooo mimi ndo namfelishaaa.

Akanitizamaa, unawaza shirki tuuu mda wote, kwa hio umeona kujiongeza ndo kuwanga, wale wenzio wazitoooo ndo utaharibuuu jumla jumlaaa. Jiongezeee kikubwaa. MWAMBIE. Mmmmmmmmhhhh! Ndo manake, yule waziri wa nchi hawezi kukuanza wewe mavi yako, umkatae ili iweje, wewe ndo wa kujiongeza ugange njaa yako, mtumikie kafiri upate mtaji wako. Nikamuuliza najiongeza vipi, namwambia vipi shoga angu? Akajibu wewe mtu mzimaunajua kila kituuu jiongozeeee. Mhhhhhhh! Acha tu ndugu msomajiii haikuwa kazi ndogo.

Nikajikakamuaaaa nikaandika sms moja, japo unaweza kunielewa vibaya au usinielewe kabisaa ila jua wewe ni mtu muhimu sanaa kwangu, na umeugusa moyo wangu kwa namna ya kipekeee. Sijui nikurudishie kitu gani kwa wema wako. Hakuna kinachofaaa. Laiti tungekutana mapema nikauchomekea huu mstari wa kiutu uzimaaa ningekuwa mwanamke mwenye furaha sanaa duniani. KUBWA LA MAADUI. Nikajua itachukua mwaka kujibiwa.

Ikajibiwa hapo hapo, naenda Dubai next week, i can use your company. Sikutaka kusema kazini sijui ushuzi ganiii, nikasema tu sina passport. Akaniambia nenda uhamiaji muone huyu atamaliza kila kitu. Hizi ni level za kiutu uzimaaa. Tukaenda Dubai mojaaaa. Sasa yeye ni envoy, akaja kupokelewa na nini mi nikaenda hotelini moja kwa moja. Nikaja kujua tunalala hotel tofauti. Nilisonyajeee kimyaaa kimyaaaa. Sikukubali nikasema kingi lazima lifosiweee wima wima.

Nikamuuliza umelala wapi? Akaniambia katika convo za kawaida, akasema sisi mawaziri ni popular snaaa sonisingeweza kulala hotel moja na wewe ningejikuta kwa shigongo. Mmmmmhhhh! Mradi analeta ugumu tu usio na ula zimaaa. Tukaagana good night good night. Nikawazaaa, nikasema maisha sio lele mama. Nikamtumia sms moja fupi sasa ila very effective. Nina nyege sanaa na wewe. Afu basi.

Nusu saaa kubwa nasikia mlango unagongwaaa. Kichoendelea msiulizeee nyie watu wazima jiongeziiii. Ila mkae kujua sikufanya makosaaa hata kidogoooo. Hata kidogooo. Nasemajeeeee, nasema hiviiiiiiiii, hata angesema naomba makalio ningempaaaa, kwani kitu gani bwanaaaa? Na siku ya pili sasa alivonifanyia ma shopping ya hatariii, nusraa nusraaa nimuulize mwenyewe Mh hutumiii kiboga? Hujiskiiii hata kujaribu maybe kujifunza, maana uwanja wa kujifunzia nipo hapa. Basi tu Monica aliniambia sio mdau wa hayo mambooo kabisaaa

Japo nae yumooo mzoefuuu wa haya mambo si mnajua mu mkubwaa anafanya sanaa, anafanya na wengiiii na mimi i managed na ku manuver to put a mark kwenye hii tasnia ya umaluuni. Katika malaya wake woote nikaweza kuji brand na kujitofautishaaa, nikamkamataaa haswaaa. Mwanzo ilikuwa kuganga njaa mimi, yeye tamaa zake, ila mpaka tunarudi wote tunahisiaaa. Tunapendanaaaa. Na tume zoeanaaaa kabisaaa mpaka nasahau kama mtu mkubwa nchini.

Kurudi cha kwanza akanihamishia uzunguni awe anakuja kwa raha zake anitafune vizuriiii na mimi nimchune vizuriii. Nikaja kugundua mheshimiwa sio malaya, sioooo hata kidogooo. Niko mimi na mkewe tuuu hamuwezi amini ndugu wasomaji. And he was spending on me like crazy. Nilitoka from 0 to hero in a flash. Nikaanza kumpenda ile ilee sasa mahaba niueee. Akiwa kwa mkewe roho kama inachomokaaa. Mpaka nikapata Alcers.

Baada ya kukaa mda kama miaka mi 4 nikamjaribu tu tuzae, akafurahiii sanaaa. Na mimi nikafurahi sanaaa. Jaribuuu, jaribuuu na wewe, wapiiii. Bila bila tu. Nikahangaika sanaaaa. Failure ya kumzalia na mawivu yanguuu mwenyewe tukaanza kuyumba, akapunguza upendo asilimi 60%. Sio kama hanijui anakaa miezi mi 3 ndo anitafute tupige game moja. Stress zikanizidiaa. Nikaanza kuwa mlevi wa pombeee

Nikishauriwa na Nadya nikaamua kutafuta Serengeti Boy, Toy Boy kiben ten 2 cha kuniliwaza na kunipunguza ashki. Miezi mi 3 mingi jamaniii sio masihara. Ki ben changu kisaniii, hakiiimbi kama Dimond ni ki Dj. Na mwenyewe alinitongoza mtoto mkavu yule ana roho ngumuuu sanaaa. Ilikuwa kwenye harusi akanitongozaaa, nikamtimuaa. Nadya badala ampe namba yake yeye akampa namba yangu.

Kilipokuja kunipata ni kunilete mkufu wa dhahabu, kwa kzi yake alikunya kunya sio kidogokuupata hapo almost 6 month i am curving the shit out of him. Nikapunguzaa na kuwa normal atleast. Nadya yake yanamshinda yule mtoto ila anangangania sio mdogo sanaa mimi 35, yule 30 ana udogo gani? Mtume na Bi Khadija walipishana miaka mingapi bwanaaa? Mmmmmhhhhh!

Mwanaume msaniii yule muoneni vile vile, nikajua vile mie mkubwaa, mzee, afu nishazaa atakuwa antaka kunichuna labdaa, Nadya anasema whats wrong throwing him some few changes, you can afford it. Nikasema maybe. Ngoja nijaribu tu nikifeli kwani kitu ganiii? Kwani shingi ngapi? Ila sikuwa na expectation hizooo, kind nilijua nitakuwa mwanamke wa shadows, wa kufichwa, natambulishwa dada yangu, nilijiandaaa kisaikolojia.

Cha kushangaza first date ilikuwa concert, alikuwa anapiga siku hio nikaenda, alifurahiaaa kama nini sijui, he better show me a smile, i am paying for it. Asiweke wimbo na kuanza kuchagiza special for my lady sijui nini na kunivuta mbele za watu nicheze nae. Moyoni najisemea vijana wenzie wanasema hili mbuzi zeee na huyu HB vipi tenaaa? Hahahaaa! He is like that. Always proud of me. Na hajawahi kuniomba hata shingi 10.

Nimemwambia nataka kuinvest kwenye hio business basi niwe partner hatakiiii. Anasema mimi ni mwanamke wake tu, its not about the money. Nadya ananiambia hapo anakupanga kwanzaaa, kukuondoa shaka atakupiga nyingi zaidi maana plan la mda mrefu. Tatizo siku hizi nacho kimeanza kunipanda kichwaniii. Kinataka kwanza kabisaa nimtambulishe kwa mwanangu kama baba! Khaaaaaaaaaaaaaaaaa! Bila hivo sipo serious nae. Mmmmmmmhhh! Na mimi mpaka kesho siku waziri akinitafuta tufanye matusi furaha yangu sio ya nchi hiii. Roho yangu bado iko kwa waziriii nzima nzimaaa. Huyu DJ anajua nina pesa ya mbogaa ila hajajua how deep m money is cause sikutaka kumuonesha hivo.

ITAENDELEA.
 
Back
Top Bottom