Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

Me Vs The Privileged.

I hate my life, i always hated my life as far as i can remember. It was one failure after another. One disappointed after another. Mpaka mda mwingine nikawa nakufuru huenda Mungu ni Mungu wa wachache. Dont get into thinking myabe i am just lazy and complaining and shit, hapana nafanya kazi sanaaa, najitumaaa mnooo, na fight balaaaa.

First and foremost i am a Dr. medicine by profession nimepata university of Mosscow, nina masters ya epidemiology from London school of tropical medicines, nina PHD in Epidemiology from University of Pittsbrugh. I am educated and i am proud to say expensively educated. Sio elimu ya mchezo mchezo. Dont get mad, at least not yet.

Hizi research institutes hapa bongo nimeingia sanaaa na kutoka kama choni kwangu vile, kuanzia Ifakara, ICAP, Jpiegho, taka taka gani za mradi ya Malaria, Nimevuruga mnooo, si ndo tropical medicines sasa. Wazungu watasha wenyewe nikieka tu magamba mezani wana shake hands na mimi fastaaaa na kunikabidhi mradi. Hio london school of tropical medicines ndo kila kituuuuu kwenye miradi ya hii ya malaria.

I thank my pops, he was not rich, ila alikuwa ni Dr tu wa kawaida mvaa kipima joto, sema aliusoma mchezo kwamba wodini hamnaa ishu akaamua kuwekeza kwenye watoto tufike kule ambako yeye hakufika. Nakumbuka nilitaka ku major in pediatrics cause napenda sanaa watoto, i was young and naive and honored to save lives. Almanusuraaa aniachie laana, kakomaa soma epidemiology. Sikujibana kukupeleka Moscow uje uishie kuwa common pediatrician. Nimekuanzia misingi imara, naomba twende sawa hapa ni epidemiology tu. Na london school alinitafutia yeye mwenyewe. Alikuwa anaifatilia online kama sijui nini, na scholarship juu. Hapo mwanangu ana miaka 2 sitakiii shule mie, tukaparanganyanaaa shika nikushike nikasema tu niende nisije laaniwa. Miezi 18 sio mingi nikarudi kwa furaha.

Akanitafutia na PHD mwenyewe mzee maskini. It is sad i disappointed him either way. Nadiriki kusema dunia hii ni ya wanaume, laiti ningejua hilo mapemaaa nisingehangaikaaa sanaaaa. Ningecheza kama pele. Ila nimekosea hesabu na sio mara moja.

I was raised kwenye familia mama hajasoma ila ali manuver manuver na alikuwa extremely beautiful akapata u secretary kwa mzungu akawa analipwa vizuri sanaa, kuliko hata baba. She was over protective of us, anataka tuwe wazungu. Tumesoma st constantine Arusha, shule wazungu na foreigners tupu, it was all about grades, about europe pass mark from Africa, hivo. So mpaka naenda Moscow mimi bado bikra, sijui wanaume na hila zao sijuiiii.

Nimefika Moscow ndo naanza kujifunza funza sasa, na nilivo na mkosi kutua tu Moscow nakutana na mbabuuuu, well mbaba same age like my dad maybe older.Nikawa simtakiii simtakiii. Alinigandaaaa ruba nyumaa. Akaanza kwanza kunipa offer ya appartment uzunguni Moscow, nikahisi drug dealer baadae nikajua mtu wa Embassy wa Africa kusini huko. Baba anapenda yule balaaa. Miaka 7 tukapendana mnoooo. Nikasema nisirudi hivi hivi atanisahau nirudi na mimba. Mmmmh!

Akaniambia atakuja na nini. It took me 5 years to realise he is never comming back. Kila siku ananipa sound sound mpaka aka staafu. Uzuri i had a daughter, nakapendaaa sanaa japo kananipasua kichwa, katoto ka uschana wangu. Siku practise sanaa, nikaunga masters, nikarudi sasa nakuwa hot cake kwenye career industry yangu. Nikikaa kidogo nahama, mradi ukiishanahama.

Zikaanza stress za reja reja oooh ana hela ila mume hana. Kazalishwa tu kaachwa. Wajinga hawakosi pa kukushikia. Nikaanza kusaka mume sasa. Kama bahati Nikampata Dr. mmoja nae tulikuwa wote Moscow Dr Jovin. Tukapendana sanaaa, nikajihakikishia naolewa 200%. Miaka inaenda ha propose wala nini. Nikaamua kumuuliza muhenga mwenzangu vipi? I am 35, you are 36 vipiii?

Akasema mimi nina mchumba yuko Moscow, akirudi nitamuoa huyooo, asiporudi nitakuoa wewe. Khaaaa! I was desparate i took the offer, nakesha na kusali asirudiiii, nafungaaa, mpaka nikawa mkangafu kila navofunga naona haitoshiii. Dogo nae kaanza maswali baba angu nani? Shubhamit yule baba ake anaendekeza zinaa Moscow tu.

One unlucky gloomy day the girl from Moscow came back, in town for the marriage. Niliumia sanaaa, mnooo mnoooo, still i was hoping something will happen, just something, God was not gonna stand by and watch me be cast aside afu mtu mwingine aolewe, after so much i put in, so many prayers, so many fastings, so much everything. Nilijitoa kwa yule mwanaume acheni tuuu. Sitaki kuanidka sanaaa.

Nikawa nishasikia mwenye mali karudi ila nikaamua kukomaaa na mimi singoki. Natuma text kama kawaida, care kama kawaida, kama kuamua aamue yeye mwanaume sio mimi nijiweke pembeni. Text zikaanza kupungua, simu zikaisha kabisaaaa kila dalili ilionesha kwamba yule ashaamua na ameamua ku base kule kwa bibie alietoka moscow, ila bado nikawa in denial naona kabisaa chance ipo. Chance gani labda wewe msomaji umeelewa.

Mafungo kama kawaida, sadaka za kuteketeza kama kawaidaaa. Napambana mpaka dakika za mwisho. Na dakika ya 90 ilifika kwa text yake kwamba jmosi mimi nao kutoka kwa Jovin, na kwa text hio it was obvious anae olewa tena sio mie tena ndugu msomaji. Sikukata tamaa naamini kabisaa bado hio sio fainalii kabisaa, ni distraction tu. Jumamosi ikafika akaoa kweli ndugu msomaji amini usiamini the wedding went down. Everybody in our cycle was there except me. I was 36 and my girl was 8. Ndipo nilipo conclude kwamba Mungu ni Mungu wa wachache, na kati ya hao wachache mie simooo kabisaa na wala hata nifanyaje siwezi kuingia.

Several years later nakanusha kabisaaa kwamba Mungu si Mungu wa wachache, ni Mungu wetu sote, na hakuna asilo liweza. I was married nikiwa 38, tena na researcher mwenzangu na tuna watoto wa 2 tumezaa wote na kila mmoja alikuwa na mtoto kabla.

Was the struggle worth it? Hell no! Ndo maana nawaambia nilikosea hesabu. Nilikosea vipi that is a story for another day. I envey Vivian. I envy her everybit.

She is young, married at 23, waliwahi mapemaa, katoka tu chuo wakaweka ndani. Enterpreneurial bad ass mom, ana watoto wa 2, married her best firend, ukikaa na na mumewe watakukeraaaa sio kwa kupendana kule jamaniiii. Siooo. His pops is rich, wote tulijua mume anamuoa for the pops money kumbe walaaa, the guy can make and is making his own money plus vivian ndo balaaaa zaidi. Anafanya projects na kina Melinda Gates na Laura Bush yaani ni next level kabisaaaa.

On the mean time, i am still a reseacher niko Ifakara, mradi wangu uko kijijini huko, nafuga na kuku zangu za mayai, na za kienyeji na kulima mboga everything i vowed never to become, in short ican admit i am reduced to nothing. Watasha nikaa nao mezani wananiambiaaa Stella you are too old, too committed to your family and kids, this project is too big for you. We are looking for someone like you but so much younger, without commitment, without responsibilities who can execute nimble. You can not hold a baby in one hand and a project this big on the other hand. It is just a polite way to say my days are over in the research world.

ITAENDELEA KESHO SAA 4
 
The Haves and The Have Nots.

"Nadya harusi lini?" Jamani hili swali silipendi hiliii. Na waulizeee watu wote dunianiiii nitalivumilia ila sio Vivi jamani. Akiuliza Vivi kama nachomwa kristapen, na anavopenda sasa kuniuliza hilo swali kutwa mara 890920000. Asinione lazima aniulize, na akishaniuliza mtasema labda imetosha akimuona mtu tu lazima aianzishe tena hii topic. Wakutane n Dr Square Stella sasa, utachoka wewe msomaji. Huyu muhenga Dr. Stella anavojishaua na hio ndoa utasema kaolewa na miaka 15 vile kumbe kaolewa kizee mpaka makeup ilidundaaa sura ilivomkomaaa. Kwanza Dr gani shangingi shangngi hio PHD yake naitilia mashka makubwa na hio Medicine ndo na mashaka ni Dr. Mwaka. No offense waliosoma nae wanasema Stella kichwaaa hatariii. Balaa lingine lile. Ila ndo shangingi kashindikana. Mtu ana miaka 48 afu kazaa kweli jamani kama sio ushangingi nini huo?

Vivi ndo anani nyongonyezaaa maini yoteeee. Yaani ananimalizaa. Kwanza kadogo kadogooo, afu kameolewa kadogo kadogo na kijana mdogo mdogo mwenye pesa zake, na anampenda ni balaaaa! Full package. Wakati anamuoa walisema kafata pesa ya baba mkwe, maana ana kisuuu mzeee wa Vivi sio cha mchezo mchezo. Manake alimuoa mdogo kama sio 22 basi 23 kijana alikuwa kama 27 afu hana kitu. Mzee mwenyewe hakufurahia ila Vivi akabeba mimba kukomeshaaa mzee ikabidi tu apokee mahari fastaaa.

Ever since their life has been everything i wished for and dont have. Stella nam mudu maana kazi ndogo sana kumnyamazisha namuuliza tu wewe uliolewa na miaka mingapi? Atajikanyaga kanyaga hapo Vivi atamjibia 38. Na mwambi i am 30 bado miaka 7 so nipumzishe kidogo, rekodi yako bado sijaifikia. Vivian namwambia tu nitafutie shoga angu mume, nahaadhirikaaa mwenziooo. Basi nikimwambia hivo ndo anajiona ana bahati duniani hakunaaaa

Honestly ndugu msomaji niko kwenye kona, tena kona hio ya kitongaaa. Raia zimenikalia kooni kuhusu ndoa kama sijui wana hisa kwenye hili papa langu. I just dont believe in marriage. Ukichangia sina bahati kabisaaaa niwe tu muwazi ndugu msomaji. Nikimpenda mimi mwanaume mjue ana watu maana sio mtu. Na mimi ushindani siweziii. Yaani nina nuksiii tu, wanaume naowapata mimi wa hvyo hovyo tu afu broke ass. Balaaaa tupu. Wenzangu wanaweza hata kukaa wakajivuna wanaume wa maana nimewapata ila bahati nimechezea mimi niwe tu muwazi sijawahi kubahatika zaidi ya majaribuuu tu.

Unlike Stella the Genius, and Vivi the spoiled brat, mimi nimetokea familia ya kimaskini, ya mama na wadogo zangu wa 3 wanao nitegemea mimi kila kitu. Nime fight sanaaa, nimetumika sio kidogo na hao hao wanaume kufika hii level ya maisha niliofika kukaa meza moja na kina Stella na Vivian, nime hustle sanaa mwenzenu. Navosema sio genius unaweza kudhania labda napata divsion 1, mimi ni division 3 form 4, na 2 form 5, chuo nimepiga pass tu mwanzo mwisho ndo mumini kwamba bila kufosi kingi nisingetokaaa kimaishaaa.

Baba angu yupo sanaaa, ila nae maisha ya kuunga unga tu, ana mke mwingine, na watoto wengine atajijua na balaaa lake. Mkosi juu ya mkosi wa wanaume kukanifanya niamua sasa kuwa single kwanza mpaka atakapotokea Mr. extra ordinary ambae ataushika mtima wanguuu. Low key nishafanya umalaya sanaaa, nimenufaikaaa, sahivi nimepewa kitengo marketing manager, nakula kiulaniiii, nawapa mama na wadogo zangu maishaaa. Mdogo wangu wa kike ashaolewa, wa kiume ana kazi yake, mama nae eti kaolewa tena kapata mzee mwenzie wa kumliwazaa, nae ana watoto wakubwa kama sisi wanaliwazana.

Kama kuolewa mama angeolewa mda sanaa, sababu katulia afu mzuriii sanaa, nasikitika kufnana na baba yangu sanaaa, sema hakutaka kuolewa sababu ana amini baba wa kambo si baba. Akaamua kulea wanae kiugumu ugumu maana anasema wanaume hawaaminiki kabisaaa. Kukimbilia ndoa mara wanao wana bakwa na huyo mume wanafanyiwa vitu vya ajabu akasema ataolewa wote tukiwa na maisha kama hio riziki itajitokeza. Na kweli ikajitokeza kwa huyo mzee aliefiwa na mkewe.

Navosema sina bahati mnaweza jua labda nina kiburi au nachagua sanaa, ofcourse nachagua kidogo lakini. Mwanaume wa kwanza mimi kumpenda alikuwa jirani yetu mmoja wa kishua flani, nilimpenda mpaka nikimuona naishiwa nguvuuu kwa furaha ya kumuona tu. Nakaa dirishani ili apite nimuone. Siku nzima mpaka mama ananitukana wewe vipi kama msengery aliekosa soko kwenye hilo dirisha. Nili sali, niliomba Mungu mimi, nilifanya yoteeee, ila nasikitika kuwataarifu ndugu wasomaji THEE GUY NEVER NOTICED ME TO THIS DATE. Nikaja kupotezana nae na kuja kusikia kawa mvuta bangi sijui sina uhakika

The second guy i loved, was stingy, afu ananiomba pesa. Tuko chuo wote mi pesa natoa wapi? Plus macho juu juu kwa wasichana wenye pesa. Nilijitahidi sanaaa ndugu msomaji ila nasikitika i was too broke for the relation to work. Alini stress sanaa mnoo mnooo. Msengery mnyamwezi yulee simtakiii simtakiii mpaka kesho. Sikuwahi kula hata 100 yake. Aende tu salamaaa. Kama sio mkosi nini?

Nikaja kumpenda boya mwingine, malaya malaya tu, uhusiano uligubikwa na fumanizi za kutoshaaa, nikajikongoja hivo hivo tu, akaja kuoa mtu mwingine. Nilimfanyia matukioa lakini, hio story ya siku ingine tena. Ila inshort sikuambulia kitu napo. Sio kulogwa huku jamaniiii?

Nikaja kumenda kaka mwingine nae choko tu, malaya malaya, macho juu juu tu. Afu mi akili zadarasani sina ila kumsoma mwanaume na kumfumadakika tu. Nikaona foleni kubwa, kutiana janaba tu nikajiweka pembeni kwanza nijitafakari hili gundu mbona zitooo hivi. Wanaume 4 in a row na wote sio riziki kweli jamani ndugu msomaji? Sio kulogwa huku kweli?

Hao ni watu nilio wapenda mimi, kuna walio nipenda wao, nikabanana tu hapo hapo na kujinufaisha kidogo tu ndugu msomaji sio snaaa. Kati ya wote kuna mmoja mpaka kesho ni best wangu. Alikuwa ananihitaji mda nikawa simtaki hana kitu mie wa kazi gani. Ile misenge mingine yote nimeambulia kunyosolewa tu. Hamna hamna mara ikawemo akaja kutoka kimaisha katika dili dili zake anazozijua yeye mwenyewe akaja kunitafuta na nilikuwa nimechokaaa sio kidogooo. Akaniweka kwenye ramanani. Nikasema huyu naolewa nae.

Siku napiga simu akapokea mwanamke, na mtoto analia akasema anaoga. Kumbana mbanaa sanaa ndo kusema oooh sijaoa ila na mtoto. Muongo muongo nae, nikapeleleza nikajua ana mwanamke ana kaa nae na wamezaa mtoto ndio. Akajisemesha hampendi sijui nini ilitokea ndo maana kaja kunisaka after so many years. Nikalainika tukawa na mahusiano kabisaa na jua siku yoyote yule mwanamke atatimuliwa niolewe mimi. Subhna Allah!

Kila siku anaomba mda zaidi a solve hio issue, kuja kustuka yule mwanamke kazaa mtoto mwingine wake tena. Nikajua hapa changu sinaaa, natumika. Sio haba hapa sikutumika bureee, huyu kaka anajua kuhudumia mnooo. Alinipa kiwanja nashukuru Mungu akanitafutia hii kazi, akanifungulia miradi kama mi 4. Kweli ananipenda toka moyoni sema ndo hatukuonanan mapemaa. Akanitibua vuziii zote kuongeza mtoto na mkewe, yani alinitibua kwa kimbungaaa cha katrina.

We parted ways but we are still friends ila hamu ya kupenda imekula kwangu, wanaume siwaamini hata kwa kuwatania kabisaaaa. Sahivi nikipiga mechi nipewe changuuu kabisaaaa ndo mengine yafuate. Na mechi zenyewe kupiga mara chache sanaaa. Nimekuwa kama hanisiii. Sio mtu wa pombe, sio mtu wa sigara, sio mtu wa vi ben10. Nipo nipo tu hata sijielewi. Na hata sio mtu wa wanawake vile vilekama sio hanisi ndugu msomaji mi mtu wa aina gani? Vuzi unaweza isha mwaka sija nyoa namnyolea nani?


Nikimpenda mwanaume siku 2, ya 3 lazima aje kunitibua vuzi zoteee. Hawa short time nimepita nao si kimasihara, Naumia kweli maana sio maagizo ya Mwenyezi Mungu kuishi hivi ila nifanyaje ndugu msomaji??????????? Watu wananichukuliaje sijui, maana sionekani na mwanaume, wala mwanamke mwenzangu basi ijulikane moja kwamba flani yule msagaji, niko niko peke yangu kama jizi vile hahahaaaaa sieleweki sielewekiiii.

Wenzangu wana stress wapate mume, sjui mtu awape jina lake, sijui mambo kibao. Mi natafuta something very simple nipate tu mtu tunae elewana baaaaaaaaaaaa! Anijue mimi Nadya nataka nini na mimi nimue anahitaji nini, tuwe tu soul mates baaaaaaaaaaasssssss. Hilo karatasi wala sinahaja nalo, huko mbali sanaaa, hizo level za juu sithubutuuu wala kuchungulia humo.

Nikiona mtu anapata mtu wanaelewana ana break up kisa harusi hamna, najisikitikia, laiti mimi ningepata hata kile kidogo asichokitaka mwenzangu mbona ningekuwa mwenye furaha sanaa. Kupata tu hata bwanaaa, ana jali Nadya kala nini, wapi, kalala wapi, awe mwaminifuuu na ametuliza akili kwangu mbona ningesoma misa ya shukraniii.

Wapiiiiiiiii! Imefika stage naongea mwenyewe kwangu upweke. natizama movie najisimulia mwenyewe. Yani kuongea mwenyewe tena sio kitu cha kujishangaaa. Sijibaniii naongea hatalisaa lizima. Nifanyaje sasa. Nawaza kama nisingekuwa mtu wa morals na virtues ila siwezi kudanganya mwenzenuuu. I just cant be selfish enough to play with some ones emotions just like that.

Zamani kina vivi wakinitania roho inaniumaaaa ila sahivi nishakuwa sugu, mda mwingine utani naanzisha mwenyewe, msejaaaa.

ITAENDELEA KESHO SAA 4
 
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Msione niko kimya mambo ni fire! Yaani niko busy hatari hatariiii. Still i managed to make time kuwapeni story. Vile nimekaa kimya mmenifariji sanaa kunicheki inbobo, Lara story lini, story lini. Mnanijulia hali na nini. Niseme tu Merci!!!!!!

Sasa nasafiri this weeke transit nakuwa na masaa kibaooo na wifi za bureeee, why not nisiwaletee mastory. Maaana nina mastory kibaooooo. Sijui nianze wapi nimalizie wapi. So much has gone down na najua vile mnapendaga ubuyuuuuuu.

Stay Tuned! Tunaanza usiku huuuu huuuu. Nitaipeleka mpera mpera kidogo, tushakuwa wahenga mda ni tatizooo.
Nasikitika sana hujanitag, maana daily nakuchek kama kuna mzigo ushautupia.
 
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Msione niko kimya mambo ni fire! Yaani niko busy hatari hatariiii. Still i managed to make time kuwapeni story. Vile nimekaa kimya mmenifariji sanaa kunicheki inbobo, Lara story lini, story lini. Mnanijulia hali na nini. Niseme tu Merci!!!!!!

Sasa nasafiri this weeke transit nakuwa na masaa kibaooo na wifi za bureeee, why not nisiwaletee mastory. Maaana nina mastory kibaooooo. Sijui nianze wapi nimalizie wapi. So much has gone down na najua vile mnapendaga ubuyuuuuuu.

Stay Tuned! Tunaanza usiku huuuu huuuu. Nitaipeleka mpera mpera kidogo, tushakuwa wahenga mda ni tatizooo.
This old bih is here,Old is gold,Give us the Goodies Jimama
 
Issa been long time hoe! Nini shida magu au? Binafsi nimekumisimo! Power ya lara1 ipo pale anapoweza kuongelea professional za watu kama "mjua yote" kama kuna mtu shughuli yako haijawahi tajwa humu pole , kulikuwa forex traders, Doctors, wafanya biashara mbalimbali, wauza ngada, bankers, wakulima, walimu, researchers kwa msaada wa watu wa marekani, waporaji teh! Etc.

Asante kwa kuniita, Karibu jukwaani jembe.....
 
Lara oyeeee, ndio naanza sasa kuimeng'enyua story
 
Igweeeeeeeeee lara 1 .....am so happy mana hata kuingia humu nilikuwa najionea tabu kukutana na mimada ya ajab dahh,,,

Team stelah najiona kabisa kwenye kufunga na kuomba halafu huyooo anasepa basi tena kuangukia siko ili mradi pete kubwa nikismama ubungo wa chalinze anaiona hakuna namna siku zinasogea na.mm naitwa mrs,
 
Back
Top Bottom