BLACKMAIL VS BLACKFEMALE!
Mimi Mjeda ni mume wangu namjuaa kama nimemzaa mwenyewe. Tangia hio trip anaipanga sijui kumfariji Leo ilinitia shakaa kubwa sanaaa! Sawa Leo kafanywa ndivo sivo na Vivi still it doesnt justfy baba wa familia uache familia yako na business zako za msingi eti unaenda kumfariji mtu na vuzi zake kweliii. Mi sikutaka kusema mengiii ila i did smell ADULTRY.
I was seriously hopping wanaume wenzie watasema No, ni ujingaaa na atashushuka arudi nimfariji uongo na kweli. Mtu mzito kama waziri wa nchi kuunga mkono hii hoja nikajua tu moja kwa moja ni syndicate yao tu kufosi kingi watelekeze familia hizo siku 3 wakafanye umalayaaa. We ukiona wanaume wanaungana mkono kwenye jambo la kijinga jua lao moja na moja lenyewe la kijinga tu.
Mi sikutaka ligi yeye si mtu mzima na ashatia nia ya kuzini. Ningeweza kumchana pale pale live ila angemanipulate situation to his advantage nikaonekana nina wivuuu buree.
Mi nikatumia female inteligence yangu play the fool cards, collect evidence, withhold evidence mpaka zitoshe ku convic alafu baada ya hapo nitawambia what next. Mi nikalia tu na Mungu wangu, Mungu unaona navojitunza kama kweli huyu baba anaenda kuchepuka na kuzini naomba umuumbue mchana kweupeee saa 4 asubuhiii. Mungu hushindwi na hujawahi kushindwa na hutashindwa kamwe.
Foul namba 1 he picked the wrong destination for his crime. Kachagua Chugaa! Mzee wangu mimi Chuga yote wanamjua, wananijuaaa nje ndani. Nimzaliwa chuga na kusoma chuga. Chuga kila kona nina ndugu. Yule reception nguru doto ndugu yangu. Sikumuuliza yeye angestuka nikamuuliza Monica amuulize waziri. Alivosema ngurudoto nikajua mkono wa bwana mkubwa.
Nikampigia simu hatujaongea miakaa anamjua shemela wake si bampost face book na insta kila siku. Akabiambia ndo kafika kwa sms. Nimewapa vyumba flani akiingiza demu namuona kwenye cctv ya corridor hapa. Kuna demu anaongea nae.
Wameingia chumbani. Nikamwambia usitoke hapo hata zamu ikiisha zuga ziga ujue demu atatoka saa ngapi na atatoka vipi. Akaniambia anatoka mda huu, wigi limeloa chapa chapa. Wamepiga show bafuni hawaa. Niliumiaa ndugu msomajiiii! Mi najitunza maninaa yeye full kuniachiaa.
Nikamwambia fanya umfotoe huyo bi dada au wafotoe wote itakuwa poa sanaa! Na hizo cctv anaingia chumbani achana nazo nitakiharibia kazi bure. We wafotoe tu na Tecno wereva. Ikaja picha wanakula nyama choma linajichekesha meno 32 nje baba la familia.
Kikubwa nilichoki note kwenye hio picha kavaa mpete wa kisharoo sehemu ya kidole cha ndoa. Nikasikitika sanaa. Kesho anapiga niko ndani na dada nikajua siwezi kujikaza nitambwatukia afu atastuka wakati operation badooo. Dada lenyewe bayaaa. Anaambiwa sijarudi nimekaa hapo hapo afoka foka namchora tu.
Kesho nikapaa report tena kaenda kulala nae tena! Huo si one night stand ni affair sasa. Picha zinamiminika wako club, wapi, mi nikazikalia tu. Rich anakunywa sumu taarifa ninayo. Kaja ndani cha kwanza nikaukagua ule mpete hana na pete hana nikasema huyu pa kumuanzia hapo kwenye pete hapo hapo atainyaaa. Akaja Leo kamuita nje mi nikatokea jikoni nawachungulia anampa pete anavaa. Nikasema bahati yako.
Tangia anasema Rich kanywa sumu, anajifanya kupanic mi namchora we mwana jeshi kaua watu kibao Dafur ndo astushwe na Rich kunywa sumu anasimulia kama ka panic sanaa. Leo nikamuweka kiporo siku hio.
Usiku alivo shetani kangangania mchezooo, wakati ushahidi wangu haujakamilika kumtia hatiani mshtakiwa. Picha wanakula nyama, wako wote hazina mashiko kabisaa. Bado nahitaji ushahidi zaidi kuitokomeza hii tabia. I had to find evidence that puts him in thr scene ya kuzini kabisaa akose pa kutokea. Nikimvaa sasahivi atafukia tu mashimo na kuteleza. Favor was on his side.
Nika withhold evidence kwa sasa. Kataka mchezo, kumpa sitakii na sitaki ajue kama yupo chini ya uangalizi wa FBI. Nikaamua tu kumpa mambo kama sio mimi.
Tegemeo langu kubwa lilikuwa Leo sababu anajua inavouma kuchitiwa nikimtekenya kidogo tu ata testfy against mjeda. Siku mjeda hayupo nikampigia simu akaja. Haniangalii usoni. Nikamuuliza Arusha kimetokea nini? Anajikausha amnaaaa! Juu ya nani au nini? Nikamwambia juu nothing unusual happenede kwa Mjeda. Akajikaza akasema nothing he can think of!
Nikamtekenya Leo i am your friend right? Akasema Yes! If hypothetically speaking my man cheated on me, you will tell me right? Akajibu absolutaley! Nikampigilia msumariii. You wont sit on my coach, look me in the eyes and lie to me in broad day light would you Leo? Akaanza kubabaika sasa.
Nikamwambia Nadya cheated on you you know how ot feels,kama mtu yoyote akicheat mimi lazima nitakwambia even if it means kupoteza urafiki na Nadya na wote nitakwambia Leo. I hope you will do the same for me! Hakujibuuu! Akaaga tu.
Mjeda akarudi na zawadi ya mkufu, miaka hajanipaa zawadi, leo nimemkaanga rafiki yake yeye aja na jizawadi. Sio anivesary sio nini. Picha nimezikalia tuliiii. Anajishuku mpaka kuwasomea watoto bed time stories! Jitu kosaji linajimaliza lenyewe.
Waziri si mmudu, Rich ana matatizo makubwa siwezi kumvuruga zaidi japo najua nibgemtekenya tu angesema maana nae kamegeqa siku si nyingi. Ila huu umalaya wao wa kikundi uliniudhiii sanaaa. Ina maana gani sasa? Nilipanga kuutokomezaaa.
Mpaka hapo na vipicha tu sasa ndo nini. Nikawaza nikamcrop mume wangu kwenye picha moja akabaki dada tu yule hata jina simjui. Nikaanza kumuulizia kwenye groups zangu anatafutwa nanndugu yakd gani sijui uongo tu nilizushaa. Alionekana ngurudoto mara ya mwisho. Ukaenda mpaka mwezi sikumpataaa! Nikakata mpaka tamaa.
Siku niko game na wanangu nmuona yuleee! Roho ikafanya paah! Nikamfata na kumsalimia kwa bashasha kubwa. Akastuka maana hanijui. Nikajitia kumfananisha. Nishamsuka mwanangu mkubwa amuite Aunt anganinie ndo aunty yake.
Baada ya kumwambia nimekufananisha ana dreads kichwani, oaban vizurii nikajitia nimependa dreads zako sana ubatengenezea wapi? Akaniambia Sinza kwa Ras. Nijamwambia nipe namba . Nimependa sanaaa!
Nikaenda kwa Ras nikamuonesha picha huyu dada kanielekeza! Ras akasema huyo boss wangu wa BBC ila hakai hapa anakaa Lagos yuko likizo. Tena kesho anakuja kubana. Nikatengeneza tu kucha na kope. Kesho nikaenda tenaa! Nae akaja jioni kama Ras alivosema mida yake jionii.
Huku na huku wanawake nikamdanganya nauza nguo, bikamuonesha insta profile ya mtu naponunua mi nguo. Akajaa akaniomva namba, nikampa nika sav na yake.
Nikaanda nyama choma, bikawaalika wote waziri, rich, jimmy, Leo na wake zao. Nadya alikuwepo, Stella alikuwepo, Monica alikuwepo. Muheshimiwa alikiwepo, Tyrone alikuwepooo, Leo alikuwepoo. Team nzimaaaa ilikamilika. Tumekaa wote geti likagongwa. Kabla sijafungua nikasema jamani nina mgeni wangu special, milima haikutani binadamu hukutanaaa! Whatever you do in darkness comes to light! Mgeni huyu anatokea Lagos. Hamna aliestukaa wala nini.
Nikamuingiza bibie Reporter aje report live toka High Table! Wa kwanza kumuona getini alikuwa waizri. Akapokea tu simu isioitaaa! "Ndio muheshimiwa raisi. Nakuja sasa hivi navoongea nimeanza kuja huko. Wakapishana getini. Dada akasema like i met him before. Nilivoset meza wanaume nimehakikisha wanalipa geti mgongo, waziri peke yake ndo alikuwa an face gate so akajichomoa kinamna fastaaa!
Dada kafika pale anasema you are so sweet! I dont have many friends in Dar! Sautii tu ikampenya mjeda mpaka kwenye Pumbu. Sasa si komandoo yule! Maana dada ana tone ya kinigeria kidogo. Mjeda akataka atafute namna asigeuke waonane. Ila chale zishamchezaa.
Wa kwanza kugeuka alikuwa Leo, akabaki kama sanamuuu! Dda akamwamvia do i know you? Hace i seen you some where. Leo akajitia i was on preast training nimesoma misa nyingi sanaa so itakuwa uliniona kanisani. Anamuangalia Rich, Rich akageuka kuona soo akajitia busy na simu. Kubwa langu la maadui likajifanya haligeukiii ngooo.
Kama nilijua dada kiti niliweka wawe face to face. Akahisi picha la kifatacho ITV. Dada anazunguka yeye akapiga 360 degree u turn kumpa mgongo anataka achomoke ki silencer. Nikamdaka baba ake hujamsalimia mgeni! Wanawake wote tunamuangalia. Why is he giving attitudes, mi najua kwanini.
Hamuwezi amini alichofanya, alijitoa akili akatimua mbiooo hizo kama Huseein Bolt anaita Waziriii, muheshimiwaaa, subiri mara mojaa wakati mheshimiwa katoka kitambooo. Kakazana mkuu! Huku kampa dada kisogo. Moja kwa zoteee! Tulikaa mpaka saa 1 usiku hakurudii hamuweiz amini. Watu wakasambaratika. Na ushahidi ukaondokaaa. Wanaume walikuwa wadogo kama piriton!Kmamae.
Saa 5 karudi, anajikosha mheshimiwa alinitumia sms ya ghafla sanaa! Sorry niliondoka vile! Yule mgeni atakuwa kniona sio. Ila mheshimiwa nimemfaa kweli leo. Kanishukuru sanaa! Nyama choma vipi ili happen. Anajiona mshindiii! Nikawa nanata nae na beat tu.
Akaja kusema kwanza yule mgeni nani? Sitaki watu wa ajabu kwangu. Kwanza kuanzia leo napiga stop cook outs zozote hapa kwangu sitaki function yoyote. Anajitekenya mwenyewe anacheka mwenyewe. Anasisitiza hapa kwangu shughuli hakunaaaa sitakiii tenaaa! Nikamwambia sawaa!
Nikavaa pajama nikapanda kitandani nikalaa. Geti likagongwa mbio kaliwahi! Sijui alijua dada karudi yule. Nikaona kapewa bahasha, kaifungua kakaa chini kabisaa. Akatoka na kibiriti akaichomaa. Uso umemshukaaa! Mi ndo nilimchezea chezo la bahasha la mipicha yake na yule dada. Nika type kinote CCTV video loading!
Nimekuja kwako, nimekula chakula chako, nimekaa na mkeo, nataka million 30 lasivo mkeo anapata nakala ya cctv za hotel, picha hizi na vingine surprise. Pesa tuma account namba hii.
Akaja chumbani kasawajijaaa! Anajifanya kunichota hivi yule mgeni wa leo umekutana nae wapi tena? Nikamwmabia game alinifata yeye, akasema ananijuaaa! Na kweli ananijua sana mi ndo nimemsahau. She was so nice. Muulize mwanao mkubwa atakwambia. Akachokaaa.
Akaanza risala sasa, mke wangu nakupenda sanaaa, ikitokea siku nimechepuka ujue ni shetani tu. Namtega itategemea kama cha fastaaa nakusamehe kama umetembea na mtu huyo huyo zaidi ya 1 time mmependana. Nitapima kwa kina mazingira. Nangangana jua nakupenda sanaa, naipenda familia. Siwezi kukwamvia ila kuna watu wananisukia mipango michafu ya kutuachanisha mimi na wewe. Dunia nzimamikinitenga nitaelewa ila sio wewe mke wangu ndo kila kitu kwangu. Promise me you will stay by me. Nikamchora kuna tatizooo? Yupo hamna hamnaaa!
Nikam minya pumbu tena kuna mtu kanipigia kasema anataka kunipa habari za Arusha ngurudoto sikumpatiliza sasa unavonambia hivi mi ndo nampigia sasa. Akadkia naniiii? Namba iko wapiii? Nipe simuuu! Mi nakunnywa zangu wine tu. Umalaya mnauoenda na wake zenu mnatupendaa shubhamiiit!
ITAENDELEA