Mume wa Mtu Asiejulikana!
Najua ndugu wasomaji kabla hata hamjanijua mimi nani natokea wapi wala naenda wapi kumtumia tu Nadya $10,000 mshaanza mambo yenu ya kishamba kuniona nachunwa, sio muaminifuuu sijui nini acheni hizo mambo kabisaaa. Let me set the record straight once and for all! I am a God fearing man, a reponsible father and very loving husband to my dear wife. The woman of my life. Msininukuu vibaya sijasema The love of my life ndugu wasomaji take note ili twende sawa.
Iko hivi, my wife is the woman of my life kweli kabisaa nife hapa hapa kama nawadanganyeni ndugu wasomaji, mpaka hapa mnasoma mstari huu bado tu sijafa kwa hio basi ni kweli. Nasema hivo sababu gani, sababu bila huyu mwanamke nisingekuwa mimi leo hii. Nisingekuwa hiviii. Ningekuwa wapi sijuii. So this life i am living now i owe it to her. Ndo maana ya woman of my life.
Mimi nimetokea maisha duni tuuu, nimesoma mpaka chuo sikupata kazi mapemaaa. Demu wangu ambae katika love of my life anaweza ku rank 2nd hakunisubiri, aliwahi kupata kazi yeye akaolewa huko kazini na jitu jengine. Mimi nikawa naishi chumba kimoja.
Huku na huku nikakutana na mdada tu wa mtaani, sio kisuuu sio chochote yupo yupo tu, akawa kanipendaaa yeye. Sasa mimi kwa kujijua ukapuku wangu, naishi room moja, dari liko chini, kitanda nimenunua kwa mtu, godoro kushnehiii babu G ukilala chaga unazifikia, na kapu tu la nguo chafuuu navowajua wanawake wa mjiniii hapa nikajiweka tu pembeni. Mwanamke mwenyewe ana churaaa kubwa ambayo iko high in demand. Sikutaka stress.
Yule dada akawa tu mkarimu kwangu anafosi chance kwangu ila mimi sitaki wala nini, sio sitaki sikuwa na uwezo mzee baba nikajiepushia aibu. Yeye alikuwa anauza duka kariakoo. Msijue labda mduka wa waarabu mduka una mirupu rupu kibaooo, nooo! Alikuwa anauza kioski cha maji, soda sigara, imagine income level yake. Na bilikuwa certain kama hajaajiriwa basi cha kaka yake au bamdogo.
Huku na huku nikawa naumwa sijui msengery gani asimuelekeze getto langu akaja kuniona! Nilistukaa kidogo nichimbe chini. Hakustukaa kwamba mambo ndo hivooo mbwa kachokaaa mbwa kachokaaa kweli. Shuka ina tundu kama 6. Ile natakiwa tu nirudi mkoani kama vipi nafosi kukaa dar. Hapo homa imenikamata ile ileeee. Akanisindikiza hospital sina pesa ya kulipaa maisha chujio wengine tumepitishwa tundu za chujio la chai manina. Akaninunulia dawa msetooo. Kuna siku nasemaga Mungu nimekuonaaa kwa hakika. Dawa mseto ilikuwa ikinipiga chenga. Watu hawafi kwa malaria, watu wanakufa kwa umasikiniiii.
Akaninunulia na juice ya 200 ipo kwenye kikopo kama kikombe, matundaa na wali kwa mama lishe. Nilikuwa naondoka mwenzenu ndugu wasomajiii. Ooooohhhh! Nilimuona kama mungu wangu mdogo. Ndugu mjini ninao wengi sanaa ila ukiwa mzee wako hana kitu na wewe si mtu. Asubuhi akaniletea chai. Mchana alikuwa kko mdogo wake akaniletea chips kuku nikala afu nikatapika nili mandiiiii kwiooo kweli kabisaa kumtapikaa afu sekelaa niliwamind parasite wa malaria mwilini. Inshort akaniuguza mpaka nikaponaa kabisaa.
Baada ya kuponea kwenye tundu la sindano kuumwa , nikawa tu depressed, nimesomaa kwa shidaa, nimefauluuu sanaa, nimepamvana sanaa mpaka dawa mseto inanishindaa kweliii. Kama vipi bora tu ningetangulia nikapumzikaaa kwa amani nikajaribu maisha na kule. Hapo nakutana na wenzangu wana magariii ya mikopo si wako kazini. Mi nasotaa tu. Mpaka nikamuuliza Mungu wangu hivi mimi na baba zangu tulikukosea nini? Sawa baba angu alijificha porini asipelekwe shule na mkoloni, je mimi? Mbona elimu nimeikamata sanaa? Kazi sipatiii. Maisha yangu ya shidaa. Kama kukufuru tu nilikuwa sijibani nakufuru hata mara 60 kwa siku. Nikaanza kuona bwana bwana Mungu ana watu wake na mimi simooo katika hao watu wake.
Nishatembeza bahasha mpaka basi! Sasa Sara amvae ndo my wife wa sahivi, akaniambia mbona huna rahaaa, njoo uwe unashinda kariakoo unanisadia saidia hata kupiga story walau mwili uoge asubuhi upate maji akili itachangamka mtembea bure sio sawa na mkaa bure.
Nikaenda kariakoo siku ya kwanza hapo bado hata mahusianoo. Nimekaa kwenye kioski nje, naona wanaume wagwaduuu wanavo mtukanaa. Saraa chura yote hiooo unauza sodaaa! Bora uende Mombasa siki 2 tu ukija una benz. Mara Sara hivi hawa wanaume wa kariakoo hawakuoniii mtoto kama wewe chura chura wa kuuza soda kweli sio kufungiwa mjengoniii? Sara mtu wa Mungu sana anawaacha tu. Nikaingilia kati jamani tuheshimiane Sara mchumba wangu naomba heshima itawale. Basi wakaanza kuzuga aaah shemu lake leo umekuja kulinda si ndio? Hahaaaa! Mxiuuuu. Kariakoo pale kama una moyo mwepesi hukai. Nikasaidia saidia jioni akanipa 10,000.
Nilitamani kuuliza jamani profit zipoo kwelii? Ila ile buku 10 naihitaji balaa! Nikapokea tu. Kesho nikaenda tena sio sababu ya buku 10 but Sara was a very decent girl na yale mazingira ni hatarishi. She needed some one to stand up for her. Maana wahuni mara wanywe soda wasilipe. Balaaa tupu. Nikawa mimi sasa ndo nauza kioskiii.
Sara ana roho nzuri nyie anachokula yeye ndo nakula mimi, akinywa maji na mimi ananinunulia na jioni lazima anipe elfu 10. Hata nikimwambia ninayo ataniwekea kwenye shati. Kushinda nae sasa nikawa nimemzoea nikaanza kumpenda. Ikawa hamna kutongozana we just clicked. Watu wkajua mimi mume wa Sara basi. Nilikaa pale kioski miezi 6.
Nikaja kujua kioski cha kwake, aliuza duka la mtu aka save ndo akafungua pals sasa. Sara ni form 6 mtaratibu sanaa. Sikuwahi kukosa raha miezi yote 6 nimekaa kwenye kiosk chake. Faida ilikiwa inapatikana sema soda zinataka mtaji mkubwaa. Ila faida ya kulaa kuvaa kuweka vocha kwa siku haikosekani.
Nikaja kuitwa interview Bank. Nilifanya ile interview kwa uchungu sanaaa. Mno mno. Nijaitwa kazini. Zile buku 10 za Sara nikanunua nguo za kuanza kazi na nauli. Kidogooo maisha yakaachiaa. Haijuwa hataa position kubwa ni bank teller tu.
Nikapanga nyumba upande na kumshawishi Sara tuishi pesa ya harusi sinaaa kiukweli ndugu msomaji ikalazimu nijipasishie mke. Uzuri Sara mzaramo hata bure wanakupa mke haikuwa ishu sanaa! Nikawa sasa naishi nae, akabeba mimba. Na mimba yake anaenda kariakoo.
Naumia ila we do need the money! Bank nako njaa kali afu nilikiwa sijamaliza probation. Akajifungua maisha yetu bado ya kuunga ungaa na kamba. Lakini hamuwezi amini i never felt poor even once kwa kukaa na Sara. Hana makuu. Anajipandia dala dala sio mtu wa kitamani magari. Mimba kubwa yumo kwenye bus.Na yuko peace vibaya mnooo.
Huku na huku kama story akaniambia duka la jirani yule mpemba anaachiaa. Pale pazuriii sanaa! Mpemba alifeli usimamizi ila kazi unafanya sanaa pale. Nikamuuliza bei gani akasema inatakiwa kodi million 12 kilemba 5. Mimi nina million 5. Yeye sasa Sara ana million 5 wakati mi mumewe pesa yote tunakulaa na kujiachia sipendi kujibana banaa! Pesa hatuna ila kula nyama, kuku, kitoweo muhimu kila siku.
Katika story story nikamwambia mtu wife jwwnye business zake kuna mtu anaachia duka liko pazuri inatakiwa 17. Akasema mbona unakuwa kama shoga kama pazuri si umsapoti wife mchukulieeee. Nikasema unanitukana kwa pesa gani? Akaniambia si uende hr, raha ya bank mikopo ya 24hrs ufanye kazi mpaka ufe humu humu bado unalipa mikopo. Zikaendelea story zingine tu.
Nyumbani nikaaaza maisha haya mpaka lini? Nikakopaaa million 15. Sikumwambia wife sisi watu wa chini ndugu msomaji anaweza kuanguka pressure pesa yote ikaishia msibani. Mmmmmh! Nikaenda nikajificha ficha nikalipia kabisaa. Akaja nikamwambia hakulala usiku.
Sasa gharama za duka ukifungua ndo zinaanza kujitokezaa, mara TRA, manispaa, taka taka kibao. Pesa ikakata mzigo hatuna. Nilikondaaa! Duka likaa mwezi halifunguliwi. Yule yule mwanangu akaniambia zama saccosbaba hapa bank. Mi nakuazima million 5 unaweka unachukua 15 unanirudishia 5 zangu kumi unafanya yako. Nikamshukuru.
Tukachukua mzigo kariakoo kwa kuanzia. Mtaa wa stationery na mwenye jengo kasema pale stationery tu. Tulivo mbulula tukachukua mzigo wa pesa yote. Kuweka dukani watu wanaulizia vitu vingine na pesa tumeweka kwenye vitu vingine. Kutokujua mapema. Mungu mkubwa akatupigania mpaka tukatoka kidogo.
Sasa biashara inajiendesha maybe na pesa ya kula, hamna break through financially. Hivo hivo tukazaa mtoto wa 2. Ikapita miaka mi 3. Nikaa siku nikaamua kuacha kazi. Sikumwambia wife angenishauri vibaya. Maiaha yanataka ujasirii. Nikamwambia niko likizo.
Nikaanza kukaa dukani mwenyewe pesa naionaa. Mimi najiongeza kitu hamna nasema kiko stoo nakimbia najumua biashara si yangu na uchungu nayo. Madeni kule nilimaliza yoteee. Nikakaa kama mwezi nausoma mchezo. NSSF zilivotoka nikazama china ghuanzhou na pesa zote, tena na wife hatujibani.
Kufika kule bei sawa na kariakoo hapo sijasafirisha. Chupi lilinibanaa! Ninunue au nikibali kupoteza nauli tu Mungu atanipigania. Nimekaa siku 6 hoteli hatuoni cha kununua tena mda mwingine unakuta kariakoo rahisi kuliko hata china. Pale hotelini katika kumsimulia mtu akasema ngoja nimpigie mshkaji flani ana stationery. Akampigia.
Akamwambia hapo guanzhou hamna issue inabidi mpande ndege ingine $200 kwenda Yiwu. Huko ndo mambo yote. Akamrushia business card ya hotel. Visa inaisha, mzigo hatunaa. Isingewezekana kwenda Yiwu siku 2 hizo maana tulipewa 10 na tumekaa hio ya 7. Fungu la kukosa utakosaa tu.
Akatupa mawazo tukagonge visa Hongkong, ambayo ni Visa Free country ukifika ndo unajieleza wee wanaamua wakugongee au wakuchinjie baharini. Visa ya Hongkong China baridaa unakaa nayo raha mustarehe. Kufika mi nikagongewa frehs si nimejielezaa, wife akanyimwa afu akagongewa asikanyage tena hongkong. Balaaa!
Kurudi ikabidi wife arudi Bongo siku tuliopanga kurudi mi ndo niende Yiwu sasa. Na kweli kule mi stationery bei ya kutupaaaa kabisaaa. Sawa na unachukua buree. Nikanunua mpaka pesa ikakata bado sijaridhika. Kurudi mzigo ukaja kazi ilifanyika pesa ikaonekana.
Ikawa ndo ishu zangu hizo, wife akawa hataki kusafiri kabisaa ishu ya hongkong ili mtramatise wakamuingiza mpaka kwenye mashine inataka ujasiri mkubwa. Tukaweka formation wife anakaa dukani anasgika pesa vijana hawagusi pesaa mi natafuta kazi.
Pesa ilionekanaaa! Nikaporomosha ghorofa Bahari beach, magari nayotaka. Nikaanza kushika tenda maofisini si wanangu wako za stationery. Kwenye tenda naweka bei ya Yiwu afu naongeza 2000 tu maninaaa. Wahindi niliwala viboga wima wima tenda zote.
Pesa kumininika sanaaa nikawa nashukuru Mungu kwa kunipa chance nile na ninavovipendaa. It was time to enjoy and make it happen all i ever wanted. Nikaanza kutafuta starehe sasa pesa imekiwa nyingi mnooo! Bia siziweziiii naona chunguuu. Mziki sipooo kabisaa ukisota sana maishani kuna hasara zake. Wanawake niliwachukia enzi hizo walininyanyasa sanaa.
Inshort nilikuwa kama Mbwa afu apewe fuko la pesaa! Ni kazi bureee. Hana pakuitumiaaa. I was rich and bored. Huku na huku siku niko dukani akaja Nadya roho yangu ikastukaa tu isivo kawaidaa. Ujaji wake alikuja na mdogo wangu naemsomesha Malasia. Tattoo shingoni, kavaa raba, pensi fupi basi alionekan mtamu mtamuuu tu. Wife yupo hapo hapo.
Baadae dogo akaaga! Ila Nadya nilikuwa namuangalia kwa wizi nae kumbe kaniona akanikonyezaaa! Balaaa! Nikasema kumbe imooooo! Wife yupo napataje namba. Wakaaga. Nawaza toto nalikosa lile sasa ina maana gani kuwa na pesa. Nikimuomba dogo namba atanidharau. Wameondoka nikazugaa zugaaa nikajisemesha huyu Jully kasahau simu yake hapa ngoja nimkimbizieee. Hamna cha simu wala nini.
Nikawakuta nikamwambia Jully kanichukulie simu yangu dukani fastaa nina dili la maana. Akashindwa kuelewa mi natoka dukani huko huko afu simu akachukue yeye aliefika mbali ila ananiheshimu akaenda. Nikamuuliza mrambo unaitwa nani? Akaniambia Nadya. Nikamwambia naombanamba yako kwanza kabla Jully hajaja. Nikaisave NBC PROCUREMENT. Jully kaja wifi kasema mbona haipo, nikazuga embu niwahi chaap isijekuwa imepotea.
Sikumtafuta kama mwezi mpaka Jully karudi Malasia nikamchomekea kumpeleza kama Nadya yupo kule. Nikajua yupo kule. Hawa watoto kuwala hakuhitaji akili kunahutaji tu pochi nene. Vitendo zaid. Nikamcheki whatsup naomba account yako nikutumie hela ya soda. Namchapa $1000. Sisemi chochote. Mara $2000. Nae kauzu hanitafuti. Nikamchapa $5000. Akaanza kunitafuta yeye. Mi namuogopa mkeo ila nakukumbuka snaaa. Hapo hapo nikaelekeza Kibra nikachinjaaa! Kama una ni miss basi nije Malasia we sepnd quality time. Akaingia kingi njoo. Nikatafuta visa fastaa.
Nikamwambia wife naenda china one time. Hanaga shida. Nikatua Malasia nikamwambia kabisaa mi mgeni wako hukooo. Simjui mtu na sitaki Jully ajue mambo yetu. Anakoma mimi mtu mzimaaa! Nijamwambie nije na bei gani? Sema wewe bei gani itatosha kula bataaa hapo . Akasema pesa huku hitoshi we njoo na uwezo wako. Nikajikoki $15000 lazima ziishe. Ukitenda dhambi tenda kwa kujitanuaaa walau moto ukikolea ulifaidiii.
Nimefika napelekwa hotel zina ma porter wakati China nakaaga sehemu za kujibana banaaa. Nikasema moyoni ile $15000 mbona kama ndogo, tufanye $25000 itapendeza. Sehemu wazungu tupu nikaanza kujiona out of place. Si unajua mzee wa kko nina jinsi ya mkinga na shati langu la 20,000. Mmmmhhh!Uzuri akasema twende shopping nikawaza ile mironya ronya yote kwenye begi natupaaa. Hahahaaaa!
Nimeenda napigwa pamba nikijicheki kwenye kioo nimekuwa kijana bwana mambo si ndo hayaa. Nadya mbaya kanipeleka kwa sonara kanishawishi nixhukue nyororo moja la hatariii. Sikuwa na nia kulitest shingoni mbona kama limefikaaa nyumbani kwao. Nikanunua micheni mi 3. Alivochukua yeye msitake kujua mwendo wa seti seti tu. Vimoja vimoja havipendagiii.
Analalamika jamani mi sijawhi kutembea nanmume wa mtu we baba mbona unanirogaaa na pesa zako lakini. Nikamwmabia yule sio mke nimelipa tu mahari mchumbaaa. Hhahahaaa! Naweza hata kubadili mawazo ukawa wewe ndo maza house. Akadataaa!
Nilikaa pale wiki nzima, nilianza kunyweshwa pombe na nikaipendaa, disco umri huu likanoga, kamari nilicheza snaaa na mtoto lainiii ananipa vitu adimuuu. Kiukweli nilitamani niwe manji niweze kuafford yale ndo yawe maisha yangu. Wiki nzimasikupiga simu kwa wife afu ana mimba tenaaa.
Wiki ile kupiga hesabu mule mule $15,000 nikamuaga narudi bongo. Seriously i work so hard and i deserved treats kama hiziii. Kabisaaa! Nimerudi bongo mambo ya kutoka nje mabayaa sanaa! Namuona wife mzee, hana ladhaaa, hana jipyaaa! Mmmmmmhhh! Mwili unatamani, roho inamtamani yule mtoto tu mpakaminakuwa kama inataka kutoka.
Nikaanza mchezo kila baada ya mweiz naenda Malasia. Gharama zikaanza kunishinda nikawaza hapa inabidi nimrudishe tu bongo nimfaidi vizuri. Najua bongo bata reffuuu sana Milkion 3 tu kama $1500 sasaje.
Nikaanza kumuhadaa arudi, hatakiii. Akasema labda nimpangie nyumba, gari na kaziii ya mamillion. Nikatimiza masharti karudi. Hio kazi nilihonga pesa ndefu. Hamiishi hamuuu jamaniii. Mpaka mke wangu akajua nina mchepukooo. Manake kunogewa nashindwa kulala pakuche naenda chooni kupiga simu. Alinichanganyaaa!
Viashara zikaanza kuyumbaa, kuwa ngumuuu, pesa sipatiii. Nikaenda kwa mchungaji mkenya. Akasema njoo na mkeo ndo nitakuombea. Nilisita sanaa ila ndo nafilisika. Nikaenda nae. Akaombaaa! Akasema kinachonifili mke wangu anafunga na kuomba nifilisike. Nilikasirika ndugu msomajiii. Huko si sawa na kuniendea kwa mganga kunilogaaa! Kwanini? Mke akasema anaona pea zimekuwa kama shetani, anaumia anasononeka tumetoka mbali tumeoshi kwa ugumuuu kwa furaha heshima na amani. Pesa zinanitia ujingaaa! Bora pesa ziondokeee tubaki kamamzamani ndo nitampendaa. Jamaniiii! Na kweli yupo kwenye mfungo mkaliii na maombi mazitooo katika hilo.
Nukaambiwa tubuuu kwa mkeo ssma yoote lasivo unafilisika kweli. Nikasema ya Malasia, nikamtaja Nadya. Mama anaomba namuachanisha Nadya na huyu bwana, mume uliompa mtumishi wako Sara kwa Jina la Yesuuuu! Nafutaaaa na kusafishaa kabisa nguvu zote za kipepoo za mvuto na zinaaa baina ya Nadya na mume wa Sara. Jamaniii! Mmmmmhhh! Tembea uone. Maombi mazitooo! Nikawekew wakfu kwa mke wangu ole wangu mimi ni cheat!
Kweli baada ya yale maombi biashara zikaa vizuriii sanaaa. Inaonekn wife aliacha kufunga heheheee! Nikaanza kumuacha Nadya kisiasa. Kumuacha Nadya rahisi sana nikaanza tu ku!nyima pesaa. Akajitafakari akaanza yeye ooh we mume wa mtu. Tukaachana juu juu tu hakukuwa nanofficial notice.
Juzi kunipigia kanipa mtihani mkubwaa snaaa! Na ndo $10000 nimetoa bado kupewa rejesho. Wkafu wa yul mama nao unanitishia amani. Balaaaa! Kiukweli mimi Nadya nampendaaa. Ningekuwa malaya ningekwa na wanawake wengi ila nina mmoja tu huyo Nadya. Kwa pesa nilizo nazo mwanamke mmoja si kama tu sina jamaniii. Mniombee ndugu wasomaji nina majaribuuu makubwaaa sanaa mbele yangu.
ITAENDELEA