Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

Abdallah kichwa wazi a.k.a Selemani kipara vs subira kichupi a.k.a zamda mkaa uchi.... hahahaaaaaaa nyapulengaaaaa
 
Viviane long time fear.

It may look like i have everything i ever wanted but i dont. Our marriage may look ideal but it is one of the cut throat marriages in history. Labd kama Nadya na Leo wangeoana ndo wangekuwa na masaga kama yangu na mjedaaa. Jamaniii jmaniiii acheni tu. Ni zaidi ya sleeping with the enemy.

Current pressing issue ambayo mda wowote unaweza sikia nimetwangwa talaka tatu na kurudi kwetu ni ishu ya kuongeza mtoto. Well kweli tulikubaliana tuzae only 2 babies baaaas. Baada ya hapo tufaidi maisha tuzeeke wote. Medaanakwambia he doesnt plan to live for the kids ila he wants to live with the kids.

Kisanga cha watoo wa 2 kilianzia tukiwa tunaishi USA. Hio story ya USA ni ndefu sanaaa, ila kwa ufupi tu, tuliachana na mjendaaa kabisaaa. Yalitokea mambo mengi engi ikiwemo kumfumania na yule Dr. wa Sudan. Niliumia sanaaa japo even at the peak of my pain i knew i still wanted to spend the rest of my life with this moron. Uzuri aliomba msamaha, nikamchana tu bwana weee we si umepitiwa na shetani umefaidi tundaaa. Mi nakupenda na umalaya wako nakupenda hivo hivo ila lazima na mimi NIJIBU MAPIGO KWA KUCHEPUKA then we will be even na wewe utajua inauma kiasi gani. Akaweka ngumu hamna kitu kama hiko. Mimi mwanaume ale nimeenda kula uchi tu, we uta fall in love na kuweka mahisia hamnaaa biashara hio. Siwezi kukubli hio haimooo. Ukichepuka tumeachanaaaa mazimaaaaa.

Mimikiukweli sikuwa na nia ya kuchepuka ila nilitaka nimngoe vuzi 2, 3 tu ajue inavouma kuchitiwa. Nikaandaa mchaka mchaka wangu flani wa kumchezesha makida.Na simu yangu, najiumia sms mwenyewe nzuri nzuri afu naiacha ofisini hio simu. Toka nimwambie nita cheat alianza kukagua simu yangu, nikawa naiweka mbali nae kumtia tu jamba jamba. Basi humokwenye simu yangu kuna sms za mda mrefuuu sanaa nilijiandaa kama miezi 6 najitumia tu sms najijibu bonge oja ya chezooo. Sikuakanipora simuuu akazikuta zile sms. Alidataaa maana nili stage kama affair flani na mtu asiejulikana.

Nikamjaza kwamba tulienda wote Zanzibar ambako kweli niienda, Mwanza nakonilienda na Mombasa ambako nilienda pia na yeye alijua kikazi sasa kule sms zinaonesh tulikuwa wote tukajiachia sanaaa. Alipasua pasua ile simu na hakuridhikaa akachomoa na line kabisaaa. Basi moyoni cheko meno 32 nje nyamafuuuuuu kumbe vnaumaa eeeehhh. Akinijia juu namwambia mbona we uli cheat.

Hapo kati kukawa na vugu vugu kubwa maana Mjeda alikuja kwa mzee sio official kishkaji tu kama kujitambulisha bwana weee mi ndo mkaza mwanao. Sikuwepo kwenye kikao ila Mjedaanavosema Mzee alimwambia kama kazi yake ni JESHI LOOTE iwe polisi, FFU, TPDF, JKT, Navy, Fire, Magereza hatokaa ampe mke mtu yoyote alie jeshi lolote. Kama he is serious anataka mke basi aache kazihio na kitafuta cha kufanya. Bila hivo mke hapatiiiii. Alipanic maana jeshi ndo maisha yke sasa aache jeshi auze mchicha au? Afu ashaanza upata rank anaachaje sasa. He had inevsted his alredy. Na mke anamtaka pia. Akaeta posa ikakataliwa kisa mwanajeshi.

Sokomoko la affair likaungia hapo. Ukapasua ile simu na kuondoka na line, ikapita week hanitafuti wala nini. Nikasema acha kwanza upite mwezi jifunze kwanza. Ukapita mwezi. Nikaanza kumiss na kujiona mjinga huenda ndo vimesha unya jumlaaa jumlaa. Nikaanza kutafuta hapatikani namba zote. Nikaenda kwake nyumba karudisha jeshini. Nikaambiwa alienda course marekani ila tangu na hapo haku report chuoni, na hawajui alipo na kwa jeshi ashajifukuzisha kazi. Nikawaza nampata wapiii.

Nikaenda kwa mama yake, akaniambia yuko hai hilo usiwe na shaka ila hataki kkuona tenaaaa wala hataki kukusikia. Kwanza ana mwanamke wa Ki Latino sijui ki carribean ana uspaniolaaa amaizing. Nikaoneshwa na picha. Na wsia juu wewe endelea na maisha yako. Nikampeleleza yuko wapi hakuniambia na namba akagoma kunipaaa. Nilikuwa mdogo kama piriton.

Nikaanza kukonda kwa kasii. Dunia naiona chungu. Chakula hakipiiti. Baba ananiuliza nini tatizo namzuga tu. Bahati Mbaya mama yangu nae akaariki msimu huu wa mhangaiko. Nilidataaaa kabisaa. Sikuwa na wa kunifariji kabisaaaa. Nkabaki number 1, mpaka nikazeeka. Katika msiba akapiga simu Mjeda kunipa poleee. Makubwaaaa. Nikamuuliza msibani huji? Mama alikuwa kipenzi chak. Akasema i wish ila niko USA afu sina karatasi, na bongo siwezi kurudi jumla kuna mambo nayaweka sawa. Tukaongea juu juu tu kama friends.

Siku ya arobaini akapiga tena nikamwambia nitafutie chuo huko USA. I want to do anothe masters ni escape tu reality, maza kutokuwepo hapa bongo hapakaliki. For old times sake nitafutie tu chuo chochotehata state ingine, my dad will pay, i wonte bothe you at all napambana na hali yangu tu kwa sas,najua una mwanamke mspanish and i am fine with that, i swear sitoingia kwenye kumi na nane zako. Ningekuwa na mtu wa kunifanyia huo mchongo nisinge kusumbua. Maisha yameikaba na mimi i need to come to America the land of the free kidogo. Akasema poa. Akanitumia links, nika apply, mzee akalipa ada nikaenda ku report.

Akaja kunipokea na kwenda kuni deposit chuo kama mzigo. Na mimi sikuwa na papara, maisha popote, japo roho inaniumaa bado nampenda afu tumeachania mambo ya kijinga kijingaaa. Ilipita miezi 6, he didnt even say hi kwa simu wala kuja kuniona chuo. Wala hata ile tour meni hamnaaaa. Nikaanza kujichangan na watu wa kule. Huku na huku nikakutana na kaka anaitwa Diego raia wa Capre Verde.

Mtaratibuuu, mpoleee, mtu wa dini sanaaa. Akawa kanishawishi niingie kwenye mambo ya dini kiundaniii mnooo. He treated me well kwa kweliii. Sana mnooo mnooo. Life with him was simple and happy. Hana mambo mengi na mimi sina mambo mengi. Ni mwanaume ratiba zake ina elewekaaa huna haja ya kujistresss wala nini. We had plans anipeleke Carpe Verde na mimi nimpeleke Tz we make it official. Debate ilikuwa anataa tukakae carpe verde mi nataka tukae Tz hitimisho likawa tukaetu Sates kama vipi. Diego kwao nao walikuwa loaded, his dad wa a minister, he was on diplomatic visas, diplomaic passport alikuwa maisha boraaa. Nikajikuta niko sanaa kwenye cycle ya wa carpe verde cause mda mwingi ana functions Embassy au anaalikwa na wa carpe verde wenzie.

Huku na huku nikaja kusutwa hushirikiani na wabongo, unajifanya m carpe verde siku ukipata matatizo waambie wakutayarishie passport ya carpeverde. Nikamwambia Diego akasema we can be Tanzanians too, we can go to their events, nampango wa kuoa huko so i can learn. Moyoni najisemea wabongo wao wivuuu, fiftinaa na majunguu. Nikaanz kwenda kwenye events zao, uzuri niko a Diego so kama nipo sipo. Baadhi ya eventstuawa tukagongana na mjedaa akastukaa kuniona na Diego, yeye yuko na Mlatinooo hapo.

Uzalendo ukamshindaa akajipendekezakwa Diego na kuanza kumganda kuhsu mimi nani kwake, tumejuana lini, ana mipango gani na mimi.Mpaka Diego akaja kuniuliza is he your cousin or something? Why is he so concerned? Nikamwambia he is a fool dont take him seriously. Akashangaa nikamwambia Diego nilikwambia wabongo iko pasua veve kichwaaa.

Baada ya hapo T akaanza kunipigia simu ananitisha kwamba Diego sio mtu mzurii sijui nini kama kaka ananishauri. Nikamwambia kafeee mbeleeeee.Umeni deposit hapa chuo hujui naishije sahivi ndo unaja Diego sio mtu. Mbwa wewe pita kushoto. Kama luba. Nikamwambia kabl Diego hajaniua mimi m latino atakuwa ashakunyonya damu. Pambana na hali yako. Mara we can do a double date. Nikamwamba sitakiii, kila mtu abebe msalaba wake. Alianza kuhangaika kama nafsi inamtoka. Nikashangaa alikuwa hanitakii hanitaki kanitupa bongo, kuona Diego is treating me well kidogo ana panic. Haaaaaa. Alijua nitadoda na upweke. Thubutuuuuuu yake.

Ikawa christmass party upande wa wabongo sikutaka kwenda sababu kubwa jinga T lingekuwepo. Diego akakomalia sanaa nikaamua niende kumridhsha. Sina hli wala lile, Diego aka propose mbele ya kila mtu. kajieleza na kingereza chake cha kuunga unga he wants to make it official and join the Tanzanian family officially. I was so happy and i said Yes. I wish mnemuona T. Hahahaaaa! Kiboko ya boflo ni chai ya motooo. Chupi ilimbana, pumbu zikawa nzitoooo kwake. Huku na huku latino akaanzisha vagiii na T humo humo kwenye party, you still love her, and now she will be married soon. Ilikuwa vitukooo sio vidogo. Ofcourse i said Yes.

Nikamtorosha Diego tukajilie vitamuuu, watajijua na mabalaa yao. Siku hio Diegonilimpa mechi moj balaaa. Asngekuwamtumishi wa Mungu ningemwambia tujirekodi mkanda wa X. Basi tu namjua ni mkubwa kiroho sio kama lile shetani T. Hamuwezi amini T akaachana na mlatino na kuanza kunitongoza upyaaa. Nika mbolck sipendagi ujingaa kabisaaa. Kiukweli nilikuwa namkumbuka we had a special bond, and we shared best moments in life ila ndo hivo yaliopita si ndewele. Ananitumia watu khaaaaaaaaaaaa!

Siku hio kaniwahi chuo, i just need to talk. Nikasema nimsikize tu upupu wake. kasema i am sorry mambo eeengi. Nikamuuliza you ae sorry about what? That you cheated, or i counter cheated, or sababu naolewa na Diego be specific. Anajizungulushaaa tu. Sikuwahi kuacha kukupenda, na mimi nambana maswali miezi 6 ulio ni deposit hapa unakula masiha na mlatino ndo upendo huo? Kifupi hauwa na jipya nikamwambia pambana na hali yako. Ila ice btn us broke nikampa chansi ya friendship zone hakuwa na namna zaidi ya kuipokea.

Mama Diego nilikuwa simjui ila nili assume ni mzungu wa roho. Weeeeeee!Wakawa wamekuja kiofisi marekani ikatakiwa tw meet niiwa na Diego. Mama alijua kunifrustrate ananiambia engagement ring sio ndoa. Yaani ni jitu lenye roho mbayaaaa. You are not fammily. Social climber. Nikimwambia Diegoanasema mimi ndo nimekupendaa wale niachie mimi.Mama alijua kuninyosooo. i needed to alk to someone ambae sio Diego. Nani zaidi ya T.

Namsimulia matatizo yangu ndo anafrahia nilikwambia sio watu waleeeee. Khaaaaaaaaa. Siku nikiwa kwa Diego mama la mama likatinga na kuanza kunipekech tu. Afu Diego nae akaanza kuni blame mimi kwamba i am not even trying to get along with his mon sijui nini. Msidhani mama Diego lada mweusi muafrikaa. Mzungu afu mjerumaniii. Zaidi ya Adolf Hitler. Mzungu akikunyanyasa anakunyanyasa wazi wazi kabisaaa. Nikasusa nikataka kuwa mbali nao wote sio mama sio toto lake. Niende wapi wakati bwana wangu Diego ndo shoga angu, ndug yangu, best wangu. Nikaamua niende kwa T. Najiambia nammudu vizuriii.

Nimefika kwanza alikuwa na mwanamke sijui kamuokota wapiii. Kuniona akamtimua uchi, uchi alikuwa anakula mzigo au yupo kwenye harakati hizo akamtupia na nguo zake. Kwa scene hilo nikajua niko salama salmini. Wanaume huku ananitongoza nisolewe na Diego, huku anakua mzigo wa mtu asiejulikana balaaa tupuuu. Anajikosha its not what you are thinkinggg. Nikamwambiaaaah, mi najua mlikuwa mnaimba kwaya.

Kwanza kaanza kunishawishi na pombe, nikamwambia sinywi mimi na Diego tumeokoka tunampenda Yesu. Akasema atleast in my house usimtaje Diego. Please. Akaweka mzikii yeye anajidunga shots tu. Ni mnywaji kitamboo. Nikapoa nikasema nimpigie Diego, nimuelezee niko wapi. Simu hapokei. Akanitibu tibua vuziii zote. Huku T naeanakumbusha mamo ya Zanzibar, ile video anazo akanioneshaaa zikanitia nyege hatariii. Akanionesha na video ingine tulicheza Arusha hio. Zote anazooo. Hajazifutaga kumbee. Nikamuliza ndo unataka kumpa Diego au? Akasema ningekuwa na mpango mbona nishampa kitambooo. Siwezi kukufanyia hivo huu ukumbusho wangu. Makubwaaaaa.

Huku na huku tukaanza kukiss. Nilikuwa nimemiss huyu mtu jamaniii acheniii tu. Kukisiana nae na zile video balaa tupu. Nikafanikiwa kujiasua na kumwambia hapana. Basi ananihadaa hii ni good bye sex. Uaenda kuolewa na mtu mwingine atleast this one night tuagane properly. Ujue you are still my no 1.Kunihadaa tu si nimemfuma ndugu msomaji anataka kulipiga goma jipyaa mda si mrefuuu. Akanitia hila zakee, baby i know you missmy game. consider it bachelor party. Goody bye sex. Kwanza dhambi kulala na jitu jipya, mtu wa zamani ni kupasha kiporooo tu. Kama dhambi haiandikwi upya inakolezwaa tu winooo basi. Huku n huku na stress za mama D nikajaa kingi nikasema ngoja nijiliwazeee.

Mabusu afu mechi ya wizi yakanogaaa balaaa. Nikamkazia tumia condom. Anazo mbox yaani yule mtu asie jibanaa kabisaaa. Nikasema kwanza mwenyewe naibia tu sio mtu wangu wala nini atajiua na balaaa lake. Bwana bwana T mkali wa hizi kazi. Afu akawa anafosi kurudi kwenye chti bai ananipa mambo adimuuu balaaa. Anajitumaaa over performance. Na yale mambo yake ya baby nimekufikishaa, mara ngapi? Umeinjoy, that side of him that i loved ikawa imerudiii. Alinidatishaaaa. Huku na huku akavua condom kusud tu. Ukawa mjadala mrefu madai alini miss mnooo ilibidi tu afosi penalty.

Kuongea ongea nikamwambia nilikchezea chezoo. Akasonya na kutukana. Nikamwambia utoto ule sasa nimekua soon nitakuwa mke na mama mwenye familia yangu. Kumwambia hivo kama nimemtia utambii ndo kuanza mechi upyaaa. Mechi hii ya pili akawa anapigia kwa hasiraaa kali. Akanitaarifu kabisa sivai condom kabisaa nakujulishaa. Jicho jekunduuu. Weeeeee najuuuta ndugu msomajiiii. Alinisuguaaa kwa hasiraa mpaka nikahisi papuchi inawaka moto. Rah mpaka zikaanza kumix na maumivuuu humoo humooo nikachanganyikiwa na mimi. Afu hakojoiii. Moto wa kifuuu nausikiaaa nawaza kesho barafu zinanihusuuu. Nikawaza hapa bila kujiongeza leo natoka damuuu. Nachubuliwa sasa hivi. Nikaanza kumhadaa kisaikolojiaaa hata mimi na kupenda T. Sanaaaa. Nilikua marekani kukufata hoping tungeongea maybe kuyamalizaa. Every single day nilikuwa nangoja simu yako for 6 month. Siku nilipokuona a mlatino niliingia Mp. Namrudisha na enzi zetu za chuo namjaza, namjazaaa mpaka namuweka kingi. Akojoaaa.

Nikambadilishia story but now i have accepted you are not mine anymore, nimeji commit kwa mu mwengine. And i jsut said yes for him to marry me. Mamaeee. Ananihadaa we can still be together, twende bongo wote. Namwamba a little too late. subuhi nikasepa kwendakwangu nikakuta Diego yuko kwenye kochi anaingoja. Akaniomba msamaha yakaisha. Huku T ananitext mchepuko wangu. Siku akaja nyumbani kimasihara nikalala nae tenaaa bila condom. Na kama Mungu Diego hakuja wakati ilitakiwa aje, tukawa tume dodge bullet. Baada ya hio mechi ya pili nikalaa na Diego kama mara 3 nikaanza kuwashwa kwa bibi. Yaani kunawaka motooooo. Nikaenda kwa gynecologist akanipima na kuniambia mama hili gonjwa la Zinaa. Lazima utibiwe na mwenzio.

Nikajua tu gonjwa kanipa T mamaaaeee. Nikaenda kutibiwa pharacy za black market na wapikistan nikaponaa. Woga wagu ni Diego aje anishike uchawi nimempa gono. Nilikondaaa. Nae namuona mkono uleee kwa babu mda woteee, gono halidanganyi. Chupi inanibanaa. Nawaza ni confesss.

Hapo T nishamtukana tukana kanipa gono, simtakii simtakiii. Alikomaa mpaka mwisho sio yeye labda Diego. Namwambia Diego namuamini ni yeye tu ndo firauniii. Nika m block upyaaa. Siku hio kama utani Diego akaniambia inatakiwa tukatibiwe gono. Roho ikafanya paaaaah! Nimekwishaaaa. Najinyea nyea. Akniomba msamaha kwa kunipa gono. Nikatulia kwanza akaniambia alipiga one night stand na ths chick wa carpe verde stress zilizidi mimi na bi mkubwa story ndefuuu. Roho iliniumaa sana kwamba nimemnyanyasa T na kumbebesha hili gono kumbe muhusika ni Diego? Sikuongea mengi. Tukatibiwa.

Nika mu unblock T na kumuomba msamaha kwamba Gono mimi ndo nilimpa n lilitoka kwa Diego. Akajibu we hata UKIMWI nipe tu nitapokea. Diego akaanza kuwa haeleweki kabsaa yaani ana cheat wazi wazi kabisaana huyo bibie alie tupa gono. Nikamrudishia kipete chake, stress tu, nikahamia kwa T na shule nikaacha kabisaaa. Awe tu ananifanyaaa fanyaaa anavotakaaa, naburudikaa, ananilisha na kunipa pa kulala basi. Nd maisha nilichagua kwa mda huo. Na alikuwa ananifanya kweli kweli msidhani masihara kutwa mara hata 10. Hanikinaiii. Na hivi anailisha n ndo baba yangu na mama yangu wa US. Nilikomajee.

Ikaanza mipango ya nizalie mtoto, nizalie mtoto, unakaa tu hapa bre bora uzae uwe unalea. Angalizo nataka watoto wa 2 tu baaaaaaaaaaaaaaaaaas. Nataka niwasomeshe Yale. Mipango kibaooo. Alikuwa srious kweli na hilo swala la watoto wa 2 tu. Nikabeba mimba ya kwanza. Ikasumbua sanaa sanaaa. Mpaka nikamkumbuka mama nikasema angekuwepo ningerudi nyumbani kudeka mimi. Hayupo sasa.Tukawa tunahangaika wote. Alijitahidi kwa kweli. Baba alikuja kuniona akasema wazi he was disapointed nazaa tu sijaolewa wala kutolewamahar akamwambia na mjedaaa waziii. Nilikunyima mwanangu umefosi kingi.

Mjeda akasema tukaoane kama vipi. Nikiwa nimejichokea hivo hivo mimba ndogoila sumbufuuu hatarii. Gauni niliagiza online tu, nikaenda saloon ya wajamaica na mjeda akanyoa na kuvaa suti yake, tukaenda church kufunga harusi. Atleast i got to choose pete nayotaka online. Tukaenda kupiga picha basi ndo ndoa hio watu wanayooona naiaiiiidi wangejuaaa.

Nikazaa mtoto wa kwanza wa kike. Akiwa na miezi 7 nikajua na mimba ingine, nikat tuitoe, akagomaaa katu katu. Ilisumbua kidogo initoe rohooo. Nikajifungua kwa shidaa mtoto wa kike tenaaa. Akahakikisha nawekewa vijiti kabisaa vya miaka mi tano. I wished i gave him a son. Na i am going to give him a son. After 3 years nambembeleza paka leo tuongezeee mtoto hatakiii kabisaa kusikiaaaa.

Tena nikisema mambo ya Son hilo timbili lake sio la nchi hiii. Weeeeeee! Acheniii kabisaaaa. Anakwambia Obama mwnyewe ana watoto wa 2 wa kike karidhika sisi nani tujishaueeee. Clinton ana mtoto mmoja wa kike karidhikaaa. Jamaniiii. Hatakiiiii hatakiiii na anasema ukizaa tena akiwa wa kike je? Yeye watoto aliompa Mungu ndo hao hao wa kike na anajionea sawa tu. Kwanza baba yake mzazi hakuwa na watoto wa kiume kwenye ndoa yake na alizaa wa 5 so ni mambo ya ukoo.

Me i still want to try for a boy after all kuna technology these days. And we can afford it, why not. Na isitoshe ukute he is trying for a boy a wanawake wengine wa nje huko siwezi kukaa najibweteka namuamini. Ila ndo hataki hataki hii topic kuigsiaa kabisaaa kabisaaa. Nina matatizo kwenye ndoa yangu acheni tu. Afu umri unaeda na hili swala hatujafika muafaka.

ITENDELEA.
 
Vivi mi naona atulie tuu,hiyo shida yake kavile ya kujitakia.
angepata anaemlazimisha kupata baby boy ndo angejua dunia inaenda wapi(msururu wa watoto kibao)na kuzeeka kwa kuzaazaa hovyo.
.no clue story inaelekeaje hii.. hehhehe.
 
Jamaniiii! Nimerudiiii! Niliumwa mwenzenuuuu msicheze na migonjwa ya kuzoa zoa nchi za watu haisikii dawa za nchini humu. Nashukuru Mungu aliejuaa sasa nimeponaaa kabisaa kabisaaa. Mkae mkao wa kuingia 2018 na dude hiliii taratibuuuuuu! Kwa hasira naanza usiku huu huu
Pole KLM...! Nmekaa mkao wa kula!
 
Lol naona KLM umetupiga kitu cha triple hahaha sio kwa uchu tulokua nao kwakweli Asantiiii
Ngoja tatatiiiibu nianze nipoishia



Cc Smart911
 
Welcome back Lara one...sio kwa kutushindisha njaa huko..
 
Wanaumeeeee, wanaumeee Knyokoooo!

Kiukweli habari iliokuwa ina kiki ni issue ya Nadya kuliwa na Leo na usiku huo huo jamaniii hata kungoja kukuche kaenda kuliwa na mwanaume mwingine, tena wa kumuokota club. Khaaaaaaaaaaaaa! Sh just hit a new low yaaai hata sio low kafikia kabisa savage levels. Nuksiiiii sanaaaaa! Vivi ni beyond kukasirika mpaka kabakia kuhuzunika, anasisitiza hilo ni pepo a ngono. Na pepo kweli jamaniii. Walau hata ingekuwa asubuhi yake.

Mi Monica sikutaka kum judge sanaaa based on experience yangu mpaka nikazalishwa mtoto na mwanaume wa hovyo hovyo kiukweli nlimpa benefit of the doubts tu. Mimi wanaume nawajua jamaniii mwenzenu washanifanya vibayaaaa nafuuu uliwe kibogaaaa. Jiulize walinifanya nini zaidi cha kutishaa nafuuu uliwe kiboga. Hahahaaaa.

Mimi mwenzenu at the peak ya usichana wangu, mzuriiii mzuriii kweliii nikawa nimewivaa kama yai, nimemaliza chuo niawa na shoga angu ana kichen party. Tumepita pita maduka ya vyombo, tukapita duka moja kuna mkaka mzuriii anauza. Akatuambia duka lake akatuchangamkia sana. Akachukua namb zangu za simu.

Tukaanza uhusiano. Naeda pale dukani, naona mipesaaa anayofunga hesabu.Ananinunulia nachotaka, napelekwa nakotaka, nakula nachotaka. Tulipendana sanaa mnooo. Nakaa pale dukani, yaaani duka ndo lililo nitia uchizi. Kufanyana hotel za gharamaa gharamaaa tu, anachota pesa ya mauzo siku zinaenda. Nikaamua nimbebe mimba. Nikabeba mimba bwana.

Ikawa sasa inabidi ku make it official, tujuanee, wazazi wakaweka ngumu wanideposit kwa mkaka. Nishampanga mama bwana huyu mwananume sio hawa vinuka mkojo wa mitaania, mtu na pesa zake, mtu na biashara zake za china, wanashusha makontenaaa. Nikampeleka mpaka dukani akajionea mapesa yalivojaa kwenye drooo. Akaanza kufosi ndoa sasa.

Kikaa kikao, wakaja kwetu kujitambulisha. Hapo ndipo pilau lilipoingia shubiri. Katika utambulisho akaja dada mmoja shangingi shangingi sana, kavaa dhahabu mijikufuuu, hereni, bangili kama sio kilo 2 basi 3. Sio gram nugu msomaji KILO. Lace wig kama ya 1.2 she screamed money all over. Akaja na mumewe mbabu kizeee kabisaa ila kinaonekana mapesaa yamejaaa.Akajitambulisha ndo dada wa baba kijacho. Wakatajiwa mahari wakasema watarudihaina shida. Shughuli ikaisha salama.

Kimbembe kikaanza kesho nimeenda dukani nakuta baba Kijacho yuko nje, pembeni, yule dada mtu ndo yuko ndani, kama incharge na kijan mwingine design kamtoa moshi juzi juzi. Nimekaa pale nje kama hanionii yuko busy ana mkabidhi mahesabu huyo kijana mpya. Anaongea ongea umeibaaa mpaka unaoaaa mwanasheriaaa. Umeniibia sanaaa. Usijali mwanasheria atakutunzaaa.

Kiukweli nilistukaaa, nikavurugwaa ila nilimuonea huruma baba kijacho, nikamwambia twende kwetu. Hapo kawa mdogo kadataa. Njiani ndo kuniambiaukweli sasa kumbe nae kinuka mkojo tu, duka la dada yake kabisaa kabisaa haelewi kwa nini anamfanyia hivo hajui cha mtu mavi. Kuongozana nae kwake kumbe bandugu ana chumba kimojaaa tena cha uani kaibu na choo. Mtu akinya unasikia harufu yooote. Nilikaa dakika 10 nikashindwa kabisaaa.

Nikamwambia mama ukweli, alinichambaaa sina akili, nimemtia aibuuu mtaani, sijui nini. Nikawa niko nyumbani nalea mimba. Sina kazi, baba Kija hana kazi. Anakuja nyumbani kula sasa cha asubuhi, mchana na jioniii. Cha ajabu mama babaKija hamnyanyasi hata kidogo anamuheshimu sanaa, n baba nae anaona ni maisha tu. Wanaume wako simple sanaa, na ishu yangu alikuwa tu muelewa kwamba imetokea. Ila ma mimi ndo alinikalia kooni, atamsimanga baba Kija weeee mpaka kufuru akija mwenyewe kimyaaaaa.

Sasa ile kumsemana kumshusha wadogo zangu wakaanza kutokumuheshimu. Wanamuheshimu vipi mama kutwa kucha kumsema hana maana, analishwa na wakwe sijui nini. Baba Kija akaona tatizo lipo, ila sasa afanyaje maskini. Na duka la dada yake hakukaa kwa akili wala nini. Hakuwa na savings zozote pesa yote aliokuwa analipwa na kuiba tuliitumbua. Ila mwenyewe akajiongeza aanze kutembeza vyombo. Akaongea na dada yake awe anampa vyombo mali kauli anapita navo mtaani jioni anapeleka hesabu.

Mama alipingana sanaa na hilo swalaaa kidogo apate kisukariii. Monica hawezi kuolewa na mtu anaeuza vyombooo mtaani. Degree ya sheria unaishia kwa muza vyombooo. Maneno kibao. Umedhallisha ukoo, umevua nguo baba yako. Baba yangu mwenyewe supervisor kiwandani wala sio mtu na wadhfa sijui au vipi. Maneno mwengiii kapewa u supervisor kusimamia viarua sema mcheza dili sanaaa so kidogo pesa hazimpigi chenga. Hana kikubwa ila kidogo hakimshindi. Baba akasema mwche auze pesa utampa wewe za wembe. Mama aliongeaaa. Maskini aba Kija akipata hata kidogo ananipa hio pesa, ila sasa uzuri wote wa kupulizw na kiyoyozi cha duka na magari ya dada ukaishaaa. Akawa mweusi kafubaa jua. Pesa ya bia hanaa,akaanza kunywa virobaaa.

Nikajifungua salama mtoto wa kiume. Baba akasema tuishi wote tu ila sio pale nyumbani. Akaongea na mkwewe kwamba kuna mchezo wanacheza ofisi mtu anatoka million 8, yeye jina lake ndo limefika, atampatia hio pesa afungue duka la vyombo, kulipa frame na mtaji kidogo vyombo vingine achukue kwa dada yake, afu tukiuza tuwe tunamlipa kidogo kidogo. Aimuona kama Mungu wake wa duniani.

Uzuri baba ake biashara anaijua sanaaa, kaifanya mda sanaa, na ashajlikana. Kuwapata wateja wakewa zamani haikuwa ishu sanaa. Dada mtu hakufurahi yeye kufungua duka, ila yeye si mchaga wachaga wenzie wakaanza kumpa mizigo, mi ndo nakaa dukani, nashika pesa, yeye anatafut kazi. Kiukweli ndani ya miezi 6, tukalipa pesa yote ya baba. Ndani ya mwaka tukaanza kupata jina, maji mkuwa Mr. akasafiri kwenda China akanza kushea container na wenzie wa 4 wana shusha 40 ft. Badae wakabakia wanasha w 2 baadae anashusha la kwake.

Pesa ikawa nyingi sanaa, msicheze na pesa akapatana na dada yake wakaanza kufanya biashara pamoja sasa damu nzito. Akanihadaa mke wangu sahivi na pesa kaa nyumbani nakupa unachotaka nakulipa million 3 kwa mwezi, sitaki ufanye chochote. Nikagomaaa. Baadae akaanza unachongangania dukani ni umalaya si kingine. Nikaamua tu kukaa nyumbani. Manyanyaso yakaanza sasa. Nikaanza kuchakaa. Dukan kawaleta ndugu zake kiba. Pesa inaisha naenda kuomba pesa dkani napewa 15,000 jamani ya wiki nzima hapo kaenda china. Tena mtoto mdogo na madharau ya kichaga ananiambia pesa nyingi sanaa hio. Mama kijijini hatumiii hio.

Nyubani ma shemeji kama 6, wengine wanasoma wengine wako wako afu viburiii viburiiii. Siku ya siku kaaajiri mdada mchaga mwenzao ndo muuza duka, anajua biashara katoka sijui kwa waarabu gani mi natizama tu. Mimi siku hio nimetoka kuingia bafuni nyumba ilikuwa ya kizamani bafu sio master,shemeji kaja kuweka dawa na hirizi chini ya godoro mi sijui. Anarudi kaka yake eti katoka kutazamiwa kwa mganga mie namloga jamanii. Miee huyooo. Kaambiwa nimeweka dawa na hirizi chini ya godoro. Kufunua kweli vipooo. Nkafukuzwa nirudi kwetu bila mtoto. Niliumiaaa roho yanguuu.

Nikaa nyumbani siku moja nasikia mwanangu wanataka kumpeleka Moshi. Nikaenda na panga wasinitanieeee nikachukua mwanangu na kurudi nyumbani. Basi ndo kusema nisikanyage tena dukani wala nyumbani. Nikakaa week baba anampigia aje tuzungumze hataki akamblock. Bababa akasema siwezikukubali ngojaaaa. Akamfatadukani akagoma kuonana nae. Akaanza kumpigia kelele kwamba Mangi huna shukraniiiii, ulitelekezwa nikakulishaaa wewe na kukulelea mimba pesa ya hospital nimetoa mimi, mtaji nimekupa mimi afu sahivi unamnyanyasa mwanangu nasemaje sasa navua nguo hapa leo, mchana kweupeee nakuachia laana ijulikane mojaaaa. Na hata uspolaanika wakisiki watu baba mkwe wako nimevua nguo hapa na kuuza utu wangu watakujua ulivo na hamna mtu atakae kuja tena kununua. Mmmmmmmh! Akaona ngoma nzitoooo. Akaamua kutoka nje wazungmze.

Akakubali nirudi nyumbani, ila kubali yenyewei ili tu baba asimvulie nguo, na anajua mzee wangu zee la mjini hashindwi kuvua kweli ikawa balaaa tupu. Mzee akamwambia ukimnyanyasa kidogo nakuja kuvua nguo hapo saa 4 asubuhi na kaa uchi mpaka jua lizame. Ila kurudi sasa ngoma nzito, chumba knitenga, hali chakula changu mie si mchawi tena nataka kumlisha libwata, sijui nataka kumuua. Na mtoto pia sijui mwanga msaidiziii akawa anamfanyia ukatili mpaka mtoto akajua na udogo wake yule si baba yangu. Nikawazaaaa nakuwazaa kwani lazima kuolewaa. Hapa ndo ishakufaaa. Watu wananiambia pambana na ndoa yako, muombe Mungu. Mmmmmhhhh! Yatakwishaaa.

Wifi hatuongei mda kabl hata mambo ya kuloga na kuweka dawa, siku akaja mi nimejikalia kimyaa kama mfungwa, akaniambia wifi na maongezi na wewe, nikashangaaa. Akaniambia wifi kukweli wewe hujawahi kutukosea chochote basi tu warombo jeuriii sisi ndo tulivo sasa haya mambo yamefika pabaya. Mwenzio anatka kukua. Nikastuka Kuniuaaaa? Nimemkosea nini? Bwana mwenzio kashikwa akili na yule mwanamke alietoka kwa mwarabu, mimi nauhakika yeye ndo alie weka dawa ile. Sasa anamwambia wewe na baba yako mnataka kwenda mahakamani mgawane mali. Wewe mwanasheria utampukuta kila kituuu. Bora wakuue tu wawe na amani na hizi mali.

Hapa navokwambia waha kuchota unyayo,kitako wako kwa mganga wanapika makombeee huko na kupiga ramli za kufa mtu. Wameleta mtaaamu kutoa nyasa huko kwa kazi hio. Yule mwanamke mshirikina huyooo sijapata kuonaa. Anajua waganga mpaka wa Dubai. We chukua mwanao ondoka, na usiende kwenu nenda kusiko julikana Mungu atakusaidia tu bila hivo watakuumiza. Nakupa hii million 1 itakusaidia pa kuanzia. Usichukue chochote we toka na malapa kama unaenda dukani afu tokomeaaa kimojaaaa. Wakija kushtuka ushafika mbali sanaaa.

Huyu mpe mwaka tu niamini hana mia. Mwenyewe nimeacha biashara nae, hana usimamizi, management hana, wanamuibiaaa, wanamchota alikata mtaji kachukua mkopo million mia 4 bank. Huyu niamini mimi mwaka mwingi ataanza kutembeza vyombo tena. Pesa yote ialiwa kwa waganga na wataalamu. Mi naondoka kaa kama nusu saaa afu fanya nilivo kwambia. Mwenyewe haya mambo nimepewa na binamu yangu alie dukani kwenu nijiandae na msibaaa. Wapuuzi kweli.

Nilikufa ganziii. Nikaka dakika 10, lisaa niliona refu, nikambeba mwanangu stand ya bus, nikapanda shabiby mpaka Dodoma. Nimekaa Dodoma siku 2 napigiwa simu mama kafariki huku ghaflaaa. Nikarudiii. Kafariki vipi kakutwa katapika na hajakubwa, waswhili wakwa wanasema alikabwa na jini makata. Lile likitmwa halirudi bila roho. Nikaja kweli walitaka kuniuaaa, walivonikosa nyumbani kwangu wakaja kwetu wakamkumba mama maskini. Roho iliniumaa sanaaa. Akaja msibani mzazi mwenzangu, nikamfukuza mbele za watu, nikamchana live umetuma jini liniueee limemuua mama. Nakwambia mbele za watu ukiniuaaa nakwambia nitakulaa ukooo wako woooteeeeenitazikwa nao. Niguse na mwanangu uone. Watu wakamuondo msibani. Bado sikuridhikaaa, niktakaa maiti tumpelekee dukani kwake aile nyama, yeye si ndo kamuaaa. Niliumia sanaaaaa, sanaaaaa.

Baba akasema haya mambo hayana ushahidi kama kweli kafanya hivo yeye anamuachia Mungu, sisi wakristo tumtegemee Mungu atatulipia. Tusiwe watu wa visasi na kuhukumu tumuachie Mungu. Niliumia sanaaa sanaaaa. Baada ya msiba ikawa sasa business is closed, kuniua hawezi maana nishamchana mbele za watu, afu akawa hajui nimepoajee onajeee operation yao, akawa anahisi sasa mimi ndo nammaliza yeye, yeye si kapiga one kik one goal afu he missed sasa manake mi nawazidi nguvu si ndio. Wakawa wanajinyea nyea kuchinjambuzi kila baada ya masaa 6 kufanya makafara ya kujilinda.

Mi nikaondoka nyumbani na kwenda kupanga mbali kabisaaa, nikakata mawasiliano, kwenye kiduka chao sipitiiii. Hawajui niko wapi wala nafanya nini. Ndo nikakutana sasa na yule shostiii. Mwanangu akaanza kuumwa ndo nikakutana na waziri. Ila maneno mengi sanaa yalisemwaa, Monica malayaaa kaachika, Monica maisha yamemshindaaa, kaachwa anateseka maisha yamemla kibogaaa.

Watu hao hao baada ya yule bwana kufilisika kamili sasa mpaka karudi kwao rombo analima viaru na kulewa mbege na virobaaa ndo wanasema Monica ana akili sanaaa, yule hakuwa mwanaume, ule mkosiii mkosiii omba ukupitie kandooo. Hahahaaaaaa! Jamaniiii. Yule bwana yuko hai, huko kwao Rombo analima vibarua na kujenga jenga kulewa mbege na viroba mda wote. Yaani sio mtu wa kumtambulisha mwanangu alie zoea kumuita Waziri wa nchi baba, japo anajua waziri ni baba mleziii, ila moyoni atakuwa anahsi labda baba yake mzazi alikuwa Dr hivi, a Pilot au Enginerrr ila sio mnywa viroba asilaniii. Nawaza nikisema nimwambie nita muathiri kisaikolojia mjue. Ndugu msomaji ingekuwa wewe ungemwambia mwanao ambae umeinvest so much money into his future huu upuuzi. Anaweza kupata depression come on shule yenyewe IST unaanzaje kuwa na baba mnywa viroba? And my son is all i have and i am not risking his peace of mind for a looser who tried to kill me.

Baba tumepigiana kelele sanaa kwamba mwambie mwambie sitakiiii. Na sahivi kazi hana wote nawalisha mimi, na wadogo zangu na waume zao na wake zao nawalisha mimi, nimepiga mkwara ole wake mtu atakae mwambiaaa mwanangu mambo ya kisengery nimeapa nachinja mbuzi 9 kufuta undugu wangu nae vizazi 9. And the boy is not making it any easier for them. Ana maswaliiii who was my father? What didi he do for a living. Sasa mkiwa waongo muwe na consistency. Mjomba akae anamwambia alikuwa Pilot. Mamdogo anamwambia alikuwa Professor wa chuo. Mamdogo mwingine anamwambia alikuwa sucessful business tycoon. Akaja kunibananisha mama niambie wewe how come my dad didi everything, uncle swears he was a pilot, anty says he was professor, and another aunty says he was a tycoon. Nikamwambia yes my boy, he was a pilot, he taught part time chuo cha ma pilot South Africa because he was the best at what he does. And on the side he was major business tycoon. YOUR FATHER WAS A MAN OF MANY TALENTS.

Weee asipige when i grow up i will be like my father A MAN OF MANY TALENTS. Nikamchenchia semaaa nafuta hii kauliii kwa damuuuu ya Yesu ilimwagika Calvary. Akagomaa why? Hawa watoto shule tunapasuka misamba wenyewe kuwapeleka ila ndo zina wapa over confidence huwezi kuwaburuta navotakaaa. I kabidi tu nitumie siasa kwamba your Dad died early, sasa careful what you wish for, na wewe utakufa mapema shauri yako.

Mara kwenye sala za usiku aseme i pray for my real Daddy where he is, is happy and thinks about us. Jamaniii ana majaribuuu huyu mtoto. Chaaaaaaaaaaaaaa! Baba ananiambia mwambie ukweliii ataelewaaa na atakuwa upande wakooo. Sasa jamani ukweli gani manake ndugu wasomaji tuangaliage na ukweli wa kuwaambia watoto wetu.

Mkitaka kujua ana majaribu siku waziri kaja nyumbani mchana na mishe mishe zake tu, na yeye akatoka shule na wenzie mi spoilled brats wenzieee. Wakamkutaaa. Sasa si mtu wa jamii aafahamikaaa kwa suraaa. Wenzie wakawa exited sanaaa na waziri tu wa siasa akawapiga siasaaa za hapa na pale. Wenzie wakauliza so he is your pops man, how cool! He is so cool! Sijui kwanini na kwa vipiii asijibu YES HE IS MY FATHER BUT HE IS NOT MY REAL FATHER. Ilikuwa aibuuuu kubwaa. Waziri akawa diplomatic tu, wenzie wakaondoka bila kuaga.

Waziri akanipigia simu kwa masikitiko makubwa mnoo mnooo kwanini mtoto aseme vile after everything he did for us. After all the money anazolipa ada, kufinance destinations vaccations kila likizo hakai nchini, anampeleka mpaka vaccations na wanae wa kuwazaa, he still considers him not his real father? What has his real fathe done for him so far. Najitetea kwamba sio mimi mwenyewe mtoto bangi zakeeee. Waziri anasisitiza malezi yangu sio mazuriii. Mimi ndo namlsiha hayo maneno. Akatishia kujitoa kabisaaa ijulikae moja yeye sio father kamili kama vipi. Nilijielezea nilijitetea. Akatoa msimamo if he repeats that statement one more time ataondoka kwenyemasiha yetu jumla, nifanye nifanyavo to put him in his place. Mtoto huyu anataka kunipanda kichwani.

Nilirudi nyumbani nikamuita chumbani, nikachukua mkanda wa suruali yangu PURE LATHER. Nikafunga mlango. Niliml mikwajuuuu sio ya nchi hiii. Nilipambana nae man to man. mamaeee. Namuuliza baba ako unamjua wewe msengery mkubwa kama baba yako mzazi. Ashawi kulipa ada? Ashawahi kukunulia hata panadol? K mamayo zako, anajua unavaa nini, unakula nini, umeamkia wapi? au umelalia wapi? Weweaaejua unakula nini, unavaa designers, unaenda vaccations zaidi ya waziri ni nani? Hanisiiii mkubwaa wewe usie na shukraniii shubhamiiit, mshenzi wahid wewe ndo wa kumwambia waziri He is not your real father? Nilimpigaaa mpaka nikasema sasa namuua huyu mtoto. Nalo limedidnda HE IS NOT MY REAL FATHER na mikanda yote nilio mkoga. Hasira zinapanda zaidiii, dada anagonga mpaka analiaaa, dada utamuaaa mtoto ashajifunzaaa basiii harudiii tenaaaa. Yaani nkasikia kitu kimenikabaa rohoniii, mpaka nikaanza kuomba Mungu nisilinyonge tuuu hili toto halina idea na linachokisemaaa. Nikafungua mlango nikalitoa nje nikajifungia na kuanza kuliaaa na kumuomba Mungu msamaha na nguvu ya kukabiliana na hili jaribuuu. Nilijifungia mpaka kesho yake.

Nikaliamshaliende shule, kavimba alama za mikanda mwili mzimaa, jicho imevilia damu, dada anasema mwache alale tu dada hayupo vizuri nikamuuliza unataka kazi hutaki? Aende shule. Shule wakawaita ustawi wa jamiiii, wakampigia wazirii, wanataka kunifungulia kesi ya domestic violence, wainyanganye custody, ilikuwa balaa. Waziri akawapa wapa helaaa ustawiiiwakalimaliza chini ya carpet. Akanishangaakwanini nimempigaaa vile? Nikamwambia kiukweli mimi huyu mtoto kashanishindaaa. Akasema hamna tena kumpigaaa kama kuna ishu mimi nitazungumza nae.

Siku hio hio sikumkawizaa nikamtaarifu ukishikwa na nyege au pepo au ukiwashwa tu kusema wazirisio baba yako real au fake utajua mwenyewe naaapaaa, kwa jina la mama yangu alielala kaburini Neema, nakufukuza humu ndani, wewe si mwanangu, sitohusika na lolote juu yako kama utaenda huko kaburini kuishi na baba yako utajua mwenyewe, kama utamfata rombo mnywe viroba wote mkabebe zege wote utajua mwenyewe, kweli kabisaa i rest my case. Consider your self warned. Nikaingia chumbani. Alijua kuningo vuzi zote kwa kuchaa. Alinitibuaaa.

Uhusiao wetu ukawa wa tia maji tia maji hivo hiv ila alijirekebisha kidogo akajua na mimi Mom Mafia. Nikaanza tu kuhanaika na maombi ya kumtenganisha na ukoo wao na maroho ya ukoo wao maana nishaona mtoto wa simba ni simba. Like father like son. Afu na huyu Ben 10 nae ndo anataka aingie kwenye picha hapo azidi kutibua tibuaa mavuziii si balaaa ndo litazidi.

Maombi yalisadia akaja kuniomba msamaha mwenyewe dogo akamuomba na waziri kwamba alikosea and he was ungratefulll. Despite his real father hayupo he is more than a father to him. Huyu mtoto kama jitu zima vileee linaweza fanya kitu ukabakia unatoa macho tu. Tukaanza kwenda sawa kidogo sasa.
 
Back
Top Bottom