Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

Weekend Story! Bigger Levels, Bigger Devils

Living to the expectation. Queen V.

I am queen V. The queen herself, the legend, the real life barbie. Sio kazi ndogo kabisaaa kuwa mimi. It is more than anyone can manage. I am full package. People wish to be me, but they dont know what they are wishing for. Nawaaambiaaa.

You might think i live this life cause my pops is loaded ila hapana. I always wanted to marry a proper guy, who can give me a proper life, and i can enjoy the rest of my life properly. Being my pops daughter it was supposed to be piece of cake, cause a lot of family friends live proper lives, and i am a beutiful girl so money was supposed to follow money blah blah but it didnt.

I was raised to be a wife and a mother nothing more, Daddy princess nothing more. People were always nice to me, or us with my sisters and brothers, matter of fact they were more nice to my dady's money. I dated couple of guys from the clans you and i know are loaded. It was always either the guy comes from London or New York and his pops is involved with pops either way. The guys were extra nice, nikienda ma kwao mama zao ndo extra extra nice kwangu mpaka naona wazi wazi hapa pesa ya mzee inaabudiwa.

Kosa nikifanya mimi naombwa msamaha. And it was always speak to your pops about this for me, talk to your dad about this, always using me as laverage ina a baragain to get on the better side of pops. Watu wanasema bwana wewe hupendwi inapendwa pesa ya mzee wako. Acha simu za malalamiko umenichukulia bwana angu sababu ya pesa ya mzee wako, Mungu atakuulani nakwambia, si mnatumia pesa zenu kutuonea maskini. Utalaaniwa Vivi na uzao wako wote. Mapicha picha sasa wakati the guy swore he was single on his dads grave. The hustle is real.

Nikaacha kudate and i really wanted to marry young sababu home, gate kaliii sanaa, na dada alizalia home, so dad was super disapointed akaongeza ulinzi, i just wanted to do dad proud. Ushaona mtu anataka harusi na hataki kudate. Vikaanza vita vya kutolewa barua na watu wa ajabu ajabu wanaotaka favors na mzee.

Hakuna mtu alieniumaaa sanaaa kama Side. Nilimpenda sanaaa, na alikuja na gia anataka kunioa. Na side mdigo wa Tanga anajua mapenzi, kubembeleza, kudekeza, aliniganda kama luba. Side was young but he had already washed his hands so he dined with the kings. Alikuwa anapiga kazi na zmee sanaa na anaaminika. Na kilichonitia utambi, hakuwa mtu naemjua maisha yangu yote. Design aliibuka tu. Siku ya kwanza ameniona akaniambia nakupenda nataka nikuoe.

Hakutaka dating wala nini, akaleta barua. Mzee alimkataa akasema Side kijana wa mjini, level zake mishangingi ya mjini kama Nadya ila sio mimi. Mi nikangangania posa ipokelewe. Mzee akaipokea kwa roho safii tu mtoto akililia wembe mpeee. Nikawa obssesed na harusi hakuna mfanowe.

Kumbe Side kutoa ile pesa akawa anaitumia kama laverage kukopa pesa kwa mzee kila siku. Anadai kayumba. Mzee anachukulia kama mkwe wake kayumba anampa tu pesa. Na Side anazidi kuyumba. Akampa full bail out. Sasa kuna Mzee Issa ni right hand man wa mzee tangu tunazaliwa. Akawa design kamstukia Side. Akapeleleza na kujua Side ana mke wa kiarabu yuko Oman na anawapururaaa hao waarabu sio kitoto. Ndo maisha yake hayo. Kuoa au kuposa kwa matajiri aanze kuwachuna mapesa.

Wakawa wanataka kuizima hii ishu kimya kimya nisijue. Wakamuweka wanted, wachaga nyoko wale, wakamfata na bunduki akarudisha baadhi ya pesa na zingine analipa kidogo kidogo mpaka kesho. Mi sikujua chochote nikipiga namba ya Side haipatikani. Nikaanza kupata hofu.

Siku niko mjini nakula restaurant tena peke yangu, mara wanaongelea kuhsu Mzee wangu. Mzee mwenye ma bus flani,bintie yake si aliposwa na Side huyu mwarabu wa kariakoo. Oooohhh, kamchunaa sio kidogo. Kaja kustuka kampa zaidi ya million 300. Juzi wamemfata na bunduki kumtikisa karudisha 100 tu, zingine wameandikishana. Yule Side falasi sanaa, angeendelea kuwapurura waarabu tu, kavamia wachaga wale pesa zao yenyewe chimbuko lake ujambazi atawaweza.

Kidogo nizimie. I felt so much shame kumuingiza baba kwenye upuuzi kama huo. Nikasema sitaki tenaaa mwanaume anaenijua mimi nani wala natokea wapi. Ulipita mda sanaaa. Tatizo chuo wanajua mimi nani kila sehemu nayojulikana wanajua mimi nani.

Siku mtu dada yake akawa anaumwa tuko chuo mwaka wa 3. Akaniomba lift nimepeleke. Nikampeleka sasa uswazi gari haifiki. Mnapaki mnatembea. Nikaenda mpaka hapo. ukamuona mgonjwa na nini, hali yake ikawa sio nzuri. Akasema kuna jirani yake alimkopesha alfu 20, tusiondoke hatumpatia hio pesa. Tukakaa kidogo ni nyumba ya kupanga wana share upande, huyo muhusika yuko uani..

Tukaenda kupeleka hio pesa, kwa nje kaanika sare za jeshi, tukaingia tukamuona kijana almost makamo yetu. Tukataka kumpatia akagomaaa. Akaomba namba zetu maana mgonjwa ikiwa vovoteatujulishe. Shosti akamptia ya kwake, mimi nikanunda. Sio type zangu kwanza, kabisaaa. Mambo ya kurushana vichura chura sio.

Akaanza kusumbua apewe namba yangu. Shosti akataka kumwambia mimi ni nani na achukue time. Nikamwambia wewe usimwambie mpe, afu mi najua nitamfukuza vipi, kumbuka anakuuguzia dada yako, shemejio mlevi mbwa. Sasa ukimtibua vuzi ataeteseka mgonjwa. We nachie mimi nimlainishe.

Akaanza hi, sijui nini. Nikamwambia mimi sina pesa, kwanza sina wa kunisomesha kwetu kijijini na mambo kama hayo mradi tu kumkatisha tamaa, na mwambia vile vitu vinavokata nyege kwa speed ya 4G. Hahahaaaa! Nitumie 20,000. Anatuma kama jinga. Namwambia sasa suala la mimi kusoma, ananipa moyo atanisomesha.

Mwanzo nilianza kama mchezo tu, sasa baadae the lies were too deep, it was too late kumwambia all these were lies. Na uzuri hakuwa kwenye cycle yangu kabisaaa. Akitaka kuniona niko busy nasomaaa, nimesafiri hivo. Pesa yetu 20k nakula kama Hamisa mobeto kila baada ya siku 4. Akaanza kuwa anakuja chuo kuniona na nini.

Ballaa likaanza siku kanikomalia namba uje home, ni muhimu muhimu. Mmmmhhh! Nikatumia kikata nyege level one na shida ya 50,000 fasta. Akatuma akasema naomba uje seriously. Nikaanza mambo ya ada, mradi tu nisiende. Akasema suluhisho ya hilo ndo leo nimepata we njoo utajua huku. Hutahangaika tena ada.

Nikamwambia shosti ampeleleze dada yake kuna nini huko, akasema hadhani kama kuna issue serious, shoga akaniambia wewe neda. Kataa maneno usikate wito. Nikamwambia nisindikize. Akakubali. Tukapaki gari letu huku CCM, na kuchapa lapa mpaka huko uchochoroni. Ye akaingia kwa dada yake, mi nikawa najizoa zoa kuingia kwa kijana sababu nyumba za uswazi kila mtu anakukazia jicho unavojipeleka machinjioni.

Alifurahi kuniona nyie kama kaona keki sijuiii. Nikakuta form ziko pale juu. Akaniambia jaza kwanza hizi form. Nikawa nazisoma. Inshort ni form za mimi kuingiziwa mshahara wake kila mwezi. Nikauliza vipiii? Akasema kwa furaha i wish you could see him how happy he was, anaenda program ya UN Sudan 3 years. Kwa hio ananiandikisha mimi kama mwenza wake huko jeshini kwao. Mmmmmmhhhhh! Nikasema uongo wangu leooo uta ni Ufoo Saro mchana kweupeeee.

Nikiwaza nimwambie ukweli nawaza huyu mjeda mguu wa kuku anaweza hata kuwa nao hapo chini ya kitanda, akanimaliza na kunipiga muhuri wa gaidi la kibiti. Jesuuuuuuuuuus! In Nigerian voice. Nikawa nimepigwa bumbuwazi. Ananiambia utalipa ada, utasoma kwa raha you dont have to worry. Chupi niliovaaa nikahisi inanibanaa na kunikata mapajaaa, nikahisi K imekuwa kubwa chupi imekuwa ndogo ghaflaaa.

I felt bad about myself, really bad. How selfish. Kaka wa watu ashajaza form zake, ahaamua hatma ya maisha yake based on my silly lies. Nikaanza kuamini kweli nimelewa vibayaaa. Nikakata shauri nitamwambia akiwa Sudan huko, sahivi anaweza kuniua mimi, mgonjwa, shosti ikawa mambo ya Ufoo Saro bureee. Nikajikazaaa, nina roho ngumu nikijipangaaa. Nikaamua nimpe na mchezo ili asistuke kabisaa, wala asihisi kuna tatizo lolote. Nikaja zile form kw bashasha najiliza kwa uchungu huku nadai furaha.


Mjeda hataki niondokee, shoga ananitumia sms twende we shangingi utaombwa mambo sasa hivi sio kaka yako huyo. Kila nikisoma mazingira naona sio shirikishi kabisaa. Nikabadili gia angani na kuanza kujiseksisha, lengo nimpe kimoja tu cha fastaa nipate kujiokoa na nafsi yasi. Mjeda alikuwa na ugwadu kama Papii Kocha, na hivi pesa zake nimekula sanaa hizi buku 20.

Msitake niandike mengi ila mkae mkijua ATAKE KUIOKOA NAFSI YAKE ATAIANGAMIZA NA MIMI NDO NILIPOANGAMIA kujitia kupima kina cha bahari na mguu. Cha fastaa kikaishia kulala hapo hapo. Shoga anatuma sms mpaka saa 7 we malaya gari iko ccm kule shoga angu uswazi huku tutakuta balaa. Mda huo napigwa tu runguuu la kipepe mfululizo. Mjeda na hivi mtu wa mazoezi rungu la kipepe ni under estimation ya masacre ilionikuta siku hio. Kuondoka asubuhi na sikuagaaaa. Nilimwambia nachukua maji bombani, tena nimevaa bukta yake ya adidas na tshirt lake, sina sidiria sina chupi. Nina funguo tu na simu. Pochi niliacha.

Nikampigia shoga twende. Kufika wameiba power window, wamechomoa taa zote, wamechomoa tairi na rim zake. The hunger is real. Shosti tumwambie mjedaa, nikamwambia haina hajaaa. Tuokoe nafsi zetu, namtwangia Issa atajua la kufanya. Nikamsomesha tu Mzee Issa nilifata dudu sehemu sasa wamekomba power window, wamekomba tairi wamekomba kila kitu. Akauliza wapi temeke. Akasema zinakuja sasa hivi. Najua ananunua. Akaja kijana. Wewe kumbe mwanetu, samahani bwana hatukujua wa nyumbani. Wakaanza kufunga vile vifaaa. Mjeda anapiga simuu kwa fujo. Nikajificha kwanza.

Wakarudisha kila kitu, akampigia Mzee Iss bwana ishamalizwa issue yote. Akaanzakushoboka kati yenu nani mtoto wa mzee? Nikamkazia sisi wanawake wa Issa tu. Akatukana Mzee yule atafia kwenye nyuchi yule, haya shemeji zangu samahanini kwa usumbufu. Siku ingine mkipaki semeni tunaenda kwa Cobra. Tukaondokaaa. Namsimulia sasa shoga kuhusu form na rungu la comrade mjeda lilivonipata jana.

Akasema umeliwa kizamani sanaa shoga angu. Umekopwa kwa karatasi tu. Haendi UN wala vuzi la UN hilo chezo tu upagawe umpe uchi wa bureee. Utanambiaaa. Hamna kusmeshwa wala nini, ndo usha kopwa mchana kweupeee. Mi najua unamchezea mijokeri huko ndani kumbe unapigwa last card afu ukajaa manina zako. Huo uongos hoga angu, huku uswazi mwanaume akikwambia kitu jua tu anataka uchi waaaaa usikiwekee akilini. On the bright side uchi wako hajauchukua bado unao mwenyewe. Nyie mbwa kala mbwa. Alietoa pesa katoa pesa bandia, alietoa noti katoa noti bandia. Ngomaa droo hio.

Niliborekaaaa! How could he? Japo nimemchota akili sawa sio kunila kingi kizembe namna ile. Na nimempa mambo ya 3D nikijipa moyo he is different kumbe he is the biggest scammer of the all. Basi tu bahati yake, tena bahati yake anajua kufanya ila vinginevo ingekuwa hasara kamili. Haaaaaaaaa. Mpaka form zina mihuri ya jeshiii kabisa kmanina kweli kweli. Haaaaaaa.

Nikaanza kuchat nae kiugumu sasa. Ananiambi baby njoo please naondoka kesho, leo tulale wote, mafaaan kweli tena shubhamit mshenzi wahid anatumia karata ya jana kupata uchi leo. Mmmmhhh! Nikampa jokeri la bibi niko mwezini baby wangu. Nilitaka ajikoroge tu next time, wakati anadai anaondoka wiki hilo hilo kwenda Sudan. Akaniuliza siku ngapi nikajibu mi mgonjwa mgonjwa siku 10 zote niko mwezini. Akaniambia basi njoo tu.

Kilichonifanya niende ni lengo moja just to rub to his fase kwamba he is the jack ass nimejua kwamba kanitapeli uchi. Nimbananishe mpaka aseme ukweli kwamba yeye looser hamna UN wala nini. Nikajiandaa na mission ya Mr and Mrs Smith. Nimefika pale jioni sikwenda na gari wala nini, napakti zangu 4 za pad utanitaka tena yale makubwaa kabisa Free Style sitaki ujinga.

Balaa likaanza kaleta ndizi nipike kwenye mkaaa. Mmmmmmh1 Kucha yangu ya 70k naanzaje kuimenyea ndizi. American nails wanayoijua ile kucha watanielewa. Akasema natoka kidogo naja. Nikamuuliza dada, wapi kuna mama nitilie mzuri, akanielekeza. Nikaenda fastaa na hot pot nikarudi na ndzi zangu sahani tatu. Zimetiwa nazi shata shata huwezi kudhania.

Nikampa dada ile nyama, na minyanya na kila kitu nikamwambia mkaa wako weka humu. Nikabandika maji yanachemkaaa, yanakaukia najaza. Karudi usiku, hapo nimesogoa na dada mpaka basi, dada pia hajui mimi nani na kama niko vipi. Mda wa kula napakua tabasamu kubwaaa sanaaa. Kukiona chakula kile akastukaa kitu. Nikajuchuuza mzima mzima baby najua kupika nazi shata shata.

Akauliza umepika wewe, niko ndiooo. Mi mchagaaaa. Akawa anakula kimya kimya tu. Na mimi nakula mkavuuu. Akasema hujpika wewe. Nikamkazia nimepika mimi, tena nakuwa offended kabisaaa alaaa. Akasema hujapika wewe na hujui kupika kabisaaa. Nikasusa na kuacha kula nikanunaaa. Akasema mimi nimenunua ndizi bukoba, wewe hizi ni ndizi malindi za msohi hakuan upichi wala chemical equation upike malindi ziwe bukoba. Umenidanganya, na mimi sipendi KUDANGANYWA.

Roho ikafanya paaaaaaaaaaaaaaaaaaah! Nikasema nikitoka salama sirudiiii tena huu ujinga. Nikasema kweli sijapika na sijui kupika. Akaniambia kwenu hamna shida, ingekuwa kuna shida usingekuwa hujui kupika umri huo, na mimi nilikuona tu there was something about you. Chupi nikahisi inaweka nyufaaaa. Uzuri mama ntilie nawaamnia akashikwa tumbo la kuhara choo kipo ndani. Kaingia tu chooni, nikanyakua pochi moto. Najiambia wakitaka kunibaka namtaja tu Cobra. Saa 5 afu chocho za hajaaa. Niko speed ya 4g.

Kona ya kwanza, ya pili wana hawa hapaaaa wakani tight wakachukua simu, wakachukua hereni na cheni. Wakaanz akujadili tumbake au tumuavhe. Nikawaambia mimi mwanamke wa Cobra nibakeni tu ndo mtamjua. Wakastukaaa. Umemtaja nani? Cobra. Wakampigia simu, akasema mwanamke ananitwa nani? Nikawaambia mchepuko wa mzee Issa. Cobra akaongea naooo mda mrefu sanaa, wanalalamika wabakie hata na simuuu tu kwa usumbufu. Hmad mjeda huyu hapa. Sasa pozi alilotukuta sio la kukabana ila ni majadiliano.

Cobra yuko loudspeaker analalamika mi mwenye mwaamke namtaka huyoo sio kwamba simtamani ila babu Issa sio mtu wa kumchukulia mwanamke, bora umminye pumbu atakusamehe sio kumegeamwanamke, haina jisni hio penalty na vitu wanipe vyote, anawaambia huyu ndo demu wa juzi wa gari. Nikawa wa kwanza kumuona mjeda nikawaambia mjeda huyoooo. Wakasepa nikaokota vitu. Akauliza ulikuwa unongea nao nini na unajiamini nini kuondoka namna ile. Kafuraaa, nusu anichape makofiii. Anafsi kijeshi jeshi.

Nikakaza siendi naenda hostel. Anatumia ubabe twende nyumbani. Watakurudia tena wale wakubake na safari hii sitokei. Nikamjibu tu jeusir mimi nawamudu wale. Kama kunibaka ungekuta washamaliza. Anazidi kuvimba wewe mwanamke jeuri sanaa wewe, unanijibu mimi? unajua mimi nani? Kidogooo, kidogooo nimwambie wewe msengery tu utaniambia nini kwa taarifa yako mi flani. Ila nikakaa kimya. Akaanza kushuka sasa anabembeleza twende tukazungumze. Yale ya ndizi yameisha. Nikawaza huku cobra kanilinda mbele huko je? Cobra atanichokaaa. Nikarudiiii.


Njia nzima anjiongelesha kiupolee sanaa kama mtu. Kufika ndani kajaza maji kafunga mlango, afu kanikalisha face to face aka mana to man hio, ananiambia SIPENDI KUDANGANYWA. NASISITIZA SIPENDI KUDANGANYWA! MWANAMKE MUONGO SIMPENDI KABISAA KABISAAA. hYA UNA BLEED UKO PERIOD AU UONGO? Mmmmmmmmhhhhhhhhhh! Hahahaaaaa! Ukisikia k kukushuka ikaburuta chini na kuwa nzito ndo mda huo. Nikajibu ndio na bleed. Nimemtulizia jicho. Akasema nauliza mara ya 2 na ya mwisho. Nikajilaza nimesema ndio niko period. Akaanza kuchekaaaaa! Mwanamke mkavuuu wewe, bahati yako, nimekupiga mikwaraaa umekunya kunyaaaa. Usingekuwa period ungejisalimisaje fastaaa. Nikasonya tu kimya kimya.


Nikaamua na mimi kumtikisa Sudan unaenda mkoa gani? Akanitega Sudan unakujua wewe? Akanipata. Nikamuuliza safari lini? Akajibu umenichoka kiasi hiko? Nikapanda kitandani na kugeukia ukutani kulala. Nasema nikitoka leo sirudiiiii kutembea na hawa mbwa kachokaaa. Sirudiii. Nimekomaaa. Asubuhi nimeamka akaniwahi na mabusu tele tela kama sio yeye wa jana. Na mimi nikajikaushaaa. Nikaoga fastaaa, na kuaga. Akaniambia no tunaenda mahali. Nikamkazia naenda lecture. Akaanza kuomba unajua zile form nimemwambia mama sasa kasema anataka kukuona. Nikamkazia naenda lecture. Akaanza kupanic we huna shida ya ada, nendaa, na usirudi hapa. Nikajibu sawa. Nikachukua vitu vyangu na kutoka. Nikamuaga dada, alikuwa malangoni, na mjeda yuko mlangoni, akaniuliza lini tena mdogo wangu? Nikamjibu kwaheri hii ya kuonana dear, ndo nishapewa notice nisionekane tena hapa. Mungu atakujalia upone. Nitakuwa nakupigia simu. Mjeda kuona naharisha nje mambo yetu akazama ndani kwa aibu.

Alikuwa kanifika hapaaaa kooni. Afu design nishaanza kumpendaaa ile mechi ya juzi ilileta balaa kubwaa sana moyoni kwangu. Nae analeta mambo ya kisengery hasomekiii. Njiani nikasimama kwanza nikaliaaaa na mengi, afu nikaendelea na safari. Nimefika ccm nikakumbuka sikuja na gari. Nikaanza kutafuta bajaza, Porte ikawa inanipigia horn kwa nguvu inanifata nyuma, moyoni nikasema huyu choko angejua mzee wangu ana ma bus ya mkoani, Yutong tena nyingiii na gari naloendesha mimi angejipanga upya. Akaja kunisimamia miguuni. Nikawa namtazama tuuuu, uswazi porte ndo kila kituuu. Akashusha kioo, kumbe mjedaaa bwana ndo ana ki porte. Mmmmmh!

Nikamuuliza unasemaje, oooh ingiaaa bwana. Nikaingia cause sikutaka anijazie watu na kubwa sikutaka cobra anione nae. Alivokuwa proud na hio Porte hahahaaaa, ungemuhurumia. Anawasha full Ac. Nikamwambia naenda lecture kwa kumkazia so kama nishuke nishuke tu mapemaaa. Akawa ashabadilika kawa mwema tenaaa. Anajielezea ni muhimu kwenda kwa mama yake, sababu kaanda sherehe ndogo sasa nisipoenda itakuwaje. Nikamhurumia.

Kufika huko kwa mama mtu, hamna sherehe wala nini mjeda ni chronic lier. Nilichukiaaa sio kidogo. mama wa watua najitahidi kuwa polite, kachinja kuku na wali mweupe tukala, nikawa nimemuweka mjeda kiporo. Njiani akasema nakupeleka hostel kuna nyaraka muhimu sanaa za nchi hiiziko kwangu zinatakiwa na boss wake. Tunachukua tunaondoka. Hatukai. Nikawa nasema tukifika sishiukii maana nimeaga kwa matarumbeta hata siku haijapita narudi kulala kwa bwana si kujiaibisha huko.

Kaingia ndani kakaa kaaa, kakaaa. Nikazima gari, nikaipaki ccm n kumfata huko ndani. Akasema kumbe unajua ku drive, nilikutega tu. Nilikasirikaa mara 2000. Nikajua hamna cha nyraka wala nini alitaka tu kunirudisha nyumbani ki silencer. Akaanza kujisemesha mi naondoka jmosi, we still fighting mambo ya kijinga, leo tukae basi bila kugombana, mi hizo nyaraka sipeleki kama jeshi kuniukuza wanifukuzeee tu, i jsut want nikae na wewe, tu hug na kukisss bila kugombana. Akanionesha simu imeandikwa boss inapigaaa. Sipokei wala siendii, tukae tu the 2 of us. Aaiweka chini akenda kwenye friji, anastukia mi nishaipokea nasema haloo!

Mtu wa upande wa pili akasema /makibuyu huyu choko najua labda kapata matatizo haleti document kumbe anatomba mwanamke mda huu na kampa simu yangu mimi apokeee. Akafululizaaa matusiiiii ya nguoniiii. Nikastukaa na yeye kastukaaaa. Nikajizoa zoa na kusema samahani hapa chrage kibandani, kaiacha mda umeme hamna achajiwe nimeona unapiga sanaa. Simu ikakatwa. Nishajiaandaa na vitasaaa, nikajua iwavo iwavo nachezea vitasa.

Akasema you know what kesho kutwa naondoka and i said leo sitaki ugomvi, nataka tu , tukiss na ku hug tutagombana siku ingine, nakuweka kiporo. Hili soo nalia hirisha kwa siku hizi 2 kwanza. Ila ujifunze usishike simu yangu utaongea na raisi uzimie. Nikawa kimyaa nimevurugwaa. Akja kuni hug its okay. Mabusu moto moto hasiraa ikashukaa kidogoooo.

Nikaanza kumuuliza unamjua mimi nani? Anajibu nachojua wewe mwanamke wangu, japo muongo muongo nakupenda hivo hivo na shangingi shangingi pia maana mpaka gari unajua kuendesha na ada sina, hata kama ulikuwa mdangaji haijalishi ila kuanzia sasa ni mwanamke wangu ole wakeeee basha ataeshoboka hapo yaaani yaaani sitaki kusema sanaaa. Nikakaa kimya.

Shoga angu akapiga, wewe malaya mjeda kakumalizaaa, unajua kulikuwa na test ya ghafla nimekufanyia msengery wewe, umepakatwa kwa bwana huko mi nafanya test mbili mbili kubabake. Roho ikafanya paaaaaaah! Nikawaza mambo mengi sanaaa. Hili picha la mjeda sijui linakotoka wala linakoenda shule nimeitelekezaaa. Nikawa sielweiii yaani sielewi.

Nikasimulia uongo wa mjeda kwao kuna shreheee afu hamna lolote. Akauliza walipika wali kuku? Nikasema ndio. Akaniambia kiuswaziii shere hio kubwa sanaaa. Mmmmmmhhhh! Nikashangaaa sanaaaa. Sikutia neno wala nini. Huku mjedaa cassanova akajivunze mapenzi upyaaa. Mpaka maji kwenye friji ananifatia. Chakula anagizia tu. Mda aliotoka ni kwenda kupaki gari na alinifungia kwa nje.

Mi najua mda wowote najua anasema haendi kokote tuendelee na maisha mengine. Ikafika jmosi asubuhi anapaki kabisaa. Moyoni nasema kwa fix huyu ukute anaenda Arusha. Hahahaaaa! Namchora tu. Akaniachia crad ya bank na pass word nisingeshangaa codes za uongo. Nikapokea kimasihara. Ananiambia hizo hela zitazoingia tumia usijibane ila fanya ufanyavo mama umpeleke laki 3 kila mwezi zinazobaki fanya mambo yako, pendeza na nini lipia ada.

Ananiambia geto langu litunze, ikiwezekana hamia hapa achana na hostel, nishalipia kodi miaka mi 2. Najua mjeda anaenda arusha ananizingua tu. Nisindikize kazini naondokea kazini. Hapo ndo nilihakikisha mshenzi anaenda Arusha hana lolote. We sudan uondokee kazini sio airport kweli? Nikamsindikizaa. Nishaanza kumpenda so hata akinidanganya vingine nacheka tu moyoni.

Tumefika ananikabidhi porte uitunze naipendaa sanaa hiii gari yangu, gari ya ujana wangu. namba ya fundi wangu wa service hii. Uzuri kuendesha unajua so utaifaidi, haili mafutaa kabisaaa. Yaani ukinisalitiii, nimeweka ulinzi wa pentagon sitaki kusema sanaaaa. Ma kiss saa zima. Akasema nashukuru tumjuana kabla sijaondoka japo hatujawa na mda sana ila wewe ni mtu sahihi kwangu. Mmmmmmhhhhh! Nawaza kwa mikwara huyu kaenda tu hapo Arusha ananichagizaaa.


Nikarudi pale geto ndani ya porte, nikapafunga fresh na kusepa na porte ya mjeda. Nikawa na gari 2. Ila porte nilitokea kuipenda sanaaa, bai tu kuliko Rav 4 langu. Kilichokuja kufanya nijinyeee ni picha alizonitumia akiwa Sudan kweliii, kwenye combat, mbele ya vifaruuuu, serioulyyy!!!!!!!!!!!!!!!! Kumbe kaenda kweli Sudan and everything was real! Haaaaaaaaa!

ITAENDELEA KESHO
Wall
 
Jamaniii sichezi mechiii wala nini na sijakamatwa na Unga bado! Nimeumwaaa kifuaaaa huku balaaaa! Nashukuru shoga angu Mzambiaa kaniuguzaaa! Kuna winter Balaaaaa! Na wabongo wenzangu piaaa wamenisaidiaa sio kidogo. Leo narudiiii!

Kesho runaendelea na story
Hasa si utafute Boloyanki ya maana mwenyewe utashangaa winter hausikii kitu kinageuka summer ghafla
 
Uwiiii nasoma ado ado
Mdo mdo kitu konkiiiii
Dah Lara mungu akuweke miaka mia
Ngoja kwanza nsome kwa utulivu comment baadae
 
Back
Top Bottom