Weekend nikasema nipite kuhemea vitu huko masokoni na madukani, Basi Mambo ndio yalikuwa Ni hivi

Joannah

JF-Expert Member
May 8, 2020
18,404
42,489
Hapa kwetu nyumbani Tanzania ndio tunalala Sasa kupumzisha mwili, Huko UGHAIBUNI ndio mnaamka sijui? anyways nitajua vizuri nikifika hukohuko....
Basi bwana, leo weekend nikasema nipite kuhemea vitu huko masokoni na madukani, Basi Mambo ndio yalikuwa Ni hivi🔥🔥

Picha linaanza. Amita Bachani kafia kwenye maua.

Litre moja ya mafuta ya kupikia 6600

Mchele 2000@1kg

Unga wa mahindi 1600@1kg😳

Mkate 1500mdogo,mkubwa wake 3000

Tunda nyanya la kupikia 150 @1

Nyama 8000@1kg

Dagaa wa Bukoba 10000@1kg

Samaki Sato 10000@1kg

Mkononi Nina kijipesa kidunchu nilichopambana week mzima kwa jasho na damu, nikabaki nazungukazunguka humo madukani Kama mtalii kafika Zanzibar,

Nimeisikitia Sana nchi yangu nzuriii Tanzania , yenye MITO na mabonde mengi ya NAFAKA, imekumbwa na Nini nchi yangu? Ile Mito na bahari na maziwa hayazalishi Tena samaki? vipi kuhusu mabonde yetu hatuna Tena nafaka?

jamani mkate 1600tsh na wasivyo na huruma wamepunguza tuvipande tuwili, usiulize nimejuaje Mimi Ni mama najua!!

Jamani unga wa mahindi ndio 1600 kweli? au ndio wamechanganya na soya kidogo ndani yake? Hapana kwa kweli.

Jamani, ndugu zangu wa Tanzania haya mambo yanaanzaga hivi hivi , hatua thabiti zisipochukuliwa mapema tukifika mwakani miezi Kama hii Ndio tutajua hatujui.

Basi Mimi kama Mimi,nimeamua kwenda nchi za mbalii hukooo ughaibuni, watanzania wenzangu mnipokee jamani , hii nchi hii wabaki wenye mizinga ya nyuki. Niko hapa Nina hasira zangu nasearch search niende zangu nchi gani kwenye fursa. SIELEWIII🤯🤯🤯

NB: MY HEART IS BLEEDING FOR MY MAMALAND
 
Nchi ardhi ya kutosha unga wa mahindi 1600 duh
Ilitakiwa vitu kama hv viwe sh 100 kg imezidi sana 500 nyanya senti kadhaaa
Mimi pesa ss hv natumia tu mahesabu sana naona ntaumiza kichwa changu 😀😀😀
 
Nchi ardhi ya kutosha unga wa mahindi 1600 duh
Ilitakiwa vitu kama hv viwe sh 100 kg imezidi sana 500 nyanya senti kadhaaa
Mimi pesa ss hv natumia tu mahesabu sana naona ntaumiza kichwa changu 😀😀😀
500 Safi kabisa,2020 tulikuwa tunakula kwa 700tsh...wamepandisha kinomanoma yaani
 
Dawa ya kutibu maradhi haya kwa kudumu ni kuiondoa chchm madarakani maana tukiri hawana cha kutupa tena raia, maana raia tumepauka utahisi ni wakimbizi kumbe kikatiba kabisa ni raia wa nchii hii
Sasa mbadala wao Nani?maana Mwenyekiti wa Chadema kawaasa BAVICHA wasiwatukane UVCCM maana Ni ndugu zao...yaani ukichiimba hii kauli kiundani mwenyekiti nae kakabhiwa mzinga analamba asali yake,hataki kelele.....
 
Sasa mbadala wao Nani?maana Mwenyekiti wa Chadema kawaasa BAVICHA wasiwatukane UVCCM maana Ni ndugu zao...yaani ukichiimba hii kauli kiundani mwenyekiti nae kakabhiwa mzinga analamba asali yake,hataki kelele.....
Siasa ni ujasusi lazima kuwe na mipango mingi sana kucheza na akili za watu, itajulikana
 
Back
Top Bottom