Week ya lala salama arumeru mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Week ya lala salama arumeru mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by OSOKONI, Mar 25, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Jumapili ijayo tutaenda kwenye vituo husika kupiga kura zetu,.Sote wana Arumeru tumesikiliza kampeni za vyama na wagombea na ninaamini tumeshafanya maamuzi.Kwa wale ambao bado hawajafanya maamuzi au wamefanya maamuzi mabaya wiki inayooanza kesho ndio fursa pekee iliyobaki.Fuatilia kampeni za lala salama na hakika mpe kura yako mgombea au chama kilichokujibu au kuwekea mkakati kero zifuatazo hapa meru!!
  1.Uhaba wa Ardhi

  2. Uhaba wa Maji

  3. Elimu ( uhaba wa shule,kumbuka shule ya msingi usa river ilifutiwa matokea kwa sababu za kijinga sana)

  4.Uhaba wa hospitali na vituo vya afya kwa meru yote

  5. Barabara mbovu (kumbuka zilivopigwa greda wakati wa mvua na kutuongezea mateso kutokana na tope)

  6. Ukosefu wa kituo cha mabasi hapa usa madukani

  7. Hali mbaya ya soko la Usariver, Tengeru, kikatiti( wakati tunalipa ushuru)

  Nakusihi sana usimchague aliyefanya yafuatayo
  1. Bingwa wa kutukana, kukashifu wengine kusambaza nyaraka za kuchafuana

  2. Bingwa wa kugawa kanga, vitenge, kofia, t-shirt pesa taslimu pombe na vyakula

  3. Aliyekuwa chanzo cha fujo na vurugu kwenye kampeni

  Jimbo la Arumeru mashariki lipo nyuma sana kimaendeleo ukizungumzia sekta zote,.Tunatakiwa wakati majimbo mengine wanatembea sisi tukimbie ilituwafikie,. tunahitaji kamanda mkakamavu wa kuongoza hizi mbio, Chagua mtu anayeyajua matatizo ya meru na amewahi kuyaisha na kupata adha yake, huyo atatusaidia lakini mtu ambaye hayjawahi kuishi meru, matatizo yetu anayasikia tu kwa watu hataweza kuongoza mbio hizi za kuyatatua,. Nawatakieni week njema ya lala salama, na hatimaye uchaguzi mzuri wa haki na huru,...
   
 2. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  you deserve to be called 'a greater thinker'
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Naamini wamekusikia na watazingatia ushauri wako kwani hata sisi tusio wapiga kura wa arumeru mashariki hatupendi mrubuniwe na kampuni ya mwigulu.
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Osokoni kula like yangu maana natumia mobile lakini umesema kweli. Naongezea wasimchague mtu mwa lengo la kumfariji ili alee familia. Wasichague mtu kwa sababu ni shemeji ya fisadi fulani na ameapa watu hata watu wafe lakini mkwe wake apite.
   
 5. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Hii ndio nafasi ya kipekee ya wana Arumeru kufanya maamuzi sahihi!Wakikosea hakuna rangi wataacha kuona!!
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  "Kuichagua CDM, ni kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa tumechoshwa na uongozi mbovu,
  Kuichagua CDM, ni kufikisha ujumbe kuwa wana-Arumeru tunahitaji maji, ardhi na miundominu inayokidhi haja zetu.
  Uchaguzi huu mdogo wa arumeru ni kipimo cha akili za wameru"

  By Vicent Nyerere.
   
 7. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...chagua joshua,chagua chadema ondoa mafisadi tanzania...
   
 8. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  you are the master of the conquired land and you deserve 2b respected as a great thinker!!,WARNING CHADEMA IS THE ONLY AND GOOD POLITICAL PARTY TO CHOOSE.Chadema ndo mpango mzima wana arumeru mashariki acheni kudanganywa na mafisadi kama enzi za ukoloni.Nawakubali wameru na naamin tutafanya maamuzi magumu hapo tarehe 1 april 2012 yan jmapil,piga kura linda kura yako mpaka kieleweke!Thanks.
   
 9. r

  rwazi JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wachague cdm wachague mabadiliko,jamaa wamechoka ile mbaya
   
Loading...