Inaonyesha umepitia mengi sana we bibi!.. nishaanza kukuogopa halafu weka picha yako dhahiri usiniletee hizo demo..πUnanikumbusha machungu ujue......
Nimekumbuka enzi nakula bamia la chukuchuku kama kifungua kinywa.....
Khaaa....!!!ππππππ
Inaonyesha umepitia mengi sana we bibi!.. nishaanza kukuogopa halafu weka picha yako dhahiri usiniletee hizo demo..π
Labuda.Kaanzie sura ya kwanza ya simulizi za Kasinde ndani ya jarida la JF utakutana na mambo ya crush na kila aina ya visa na vimbwanga. Hapo utaona yote niliyopitia na picha za tangu utoto hata sasa.
Nakuja fastaaaaaBuu G,
Hapa mwendhio nshalowa ndembendembe nasubiri kukaushwa nirejee kwenye mstari.
Aahahahahahahhaaaaa.
Acha masikhara kuna tako na trakooo.[emoji16][emoji16] my dada utakuwa ns mzigo wa kiwango gani hadi watu wakushangae...maana ta.ko sio habari tena siku hizi, asilimia 60 ya wanawake nimaokutana nao wamefungasha
Unatangaza kuwa una kunduz la nguvu sio?Habari za uzima kila mmoja pale alipo kutoka pembe nne za dunia.
Binafsi yangu ni buheri wa afya tele mwenye changamoto kiasi cha mboga, zilizo ndani ya uwezo wangu nazitatua kwa wakati na zilizo nje ya uwezo wangu napishana nazo kama bodaboda barabarani.
Twende kwenye mada kuu kabla sijachakachua hapo kwenye salamu. Leo nawaletea kisa kilichonitokea sokoni alfajiri wakati naenda kununua bidhaa kwa ajili ya kuziuza kwa wateja wangu wa huko kitongojini ninakokaa. Utangulizi kidogo, tangu mwezi wa saba mwaka huu, niliamua kufungua genge la matunda hapa mtaani ninapokaa maana magenge yako mbali kidogo na yaliyo karibu hayakuwa na matunda mengi na ukiyakuta basi yamesinyaa kwa kukaa sana gengeni.
Baada ya kuona uhitaji wa watu pale mtaani na kusikia wamama wawili watatu wakilalamika siku wakiwa na uvivu wa kwenda sokoni kufata matunda au wakihitaji matunda na muda wa kwenda sokoni ni hafifu. Basi nikakamatia fursa na kufungua kigenge pale mtaani, bi Kasinde nikakinakshi na mbaombao na makreti ya plastiki.
Ili kukidhi haja ya wateja wapate matunda fresh yaliyotoka sokoni siku hiyohiyo, nikaamua niwe naenda sokoni kila siku na gharama ya usafiri na hadi kuuza tunda nna faida yangu ya kujaza kibaba. Nikajiongeza kuweka baadhi ya bidhaa mbalimbali za gengeni zinazohitajika mara kwa mara majumbani.
Namshukuru Maulana kigenge kikazoeleka na kinawateja hadi wa mtaa wa pili na watatu kwa huduma bora, tabasamu na utani wa hapa na pale. Mteja akija gengeni kwangu si mtoto, kijana mzee lazima ataondoka na tabasamu na kesho atarudi tena. Mziki wa taratibu haukosekani gengeni kwangu kuniliwaza kipindi nasubiri wateja na saa ingine hunyanyuka na kucheza basi wateja burudaani ahahahaaa. Huo ni utangulizi looh, somo la muhtahsari wa habari sijui ntafaulu lini walaahiβ¦. Najikuta tuu nashindwa kufupisha habari. Haya tuendelee kabla sijasahau nlichotaka kusimulia heheeβ¦
View attachment 1606825
Kisa cha leo kwanza wakati natoka nyumbani Mbagala nilichelewa maana matunda mazuri kwa bei ya mkulima lazima niyadamkie alfajiri, hivo na zile haraka nikatoka bila vuvaa dera kwa juu badala yake nikaliweka kwenye mfuko wangu ambao huwa naweka kiroba cha kubebea matunda baada ya kununua, na nikasema nikifika sokoni ndo ntalivaa kwa juu ili kupunguza tafrani sokoni na kujihakikishia usalama wangu. Nilitoka nimevaa kaboka mchizi na blauzi ili nikifika sokoni nitupie dera niwe huru kuinama kuchagua matunda bila kuhofia kukaa vibaya.
Ile nimeshuka kwenye daladala natembea kwa haraka nikiwa naelekea sokoni nafungua mfuko wangu nitoke dera nivae, heeee..!! nakutana na mtandio wa deraβ¦.. Nikasimama ghafla na kujiuliza, sasa na hii kaboka mchizi na kiblauzi ntachaguaje matunda??? Si watu wataanza kuhesabu pingili kwenye mbavu looh!! Nikaishiwa pozi, nikasema nikienda hivihivi na kaboka mchizi masaburi yataleta za mbwatambwata, bora nusu shari kuliko shari kamili.
Kama askari hachagui bunduki kwenda vitani mradi ina risasi, basi nikajifunga mtandio wa dera nikaingia sokoni. Ile naingia nasikia sauti ya mwanaume inaita, weee dadaβ¦!! Wee dadaβ¦!! Weee dada weeweeeeβ¦!! Sikugeuka ila nikapiga jicho mbele sikuona mwanamke, piga jicho la kishushushu kulia na kushoto kwangu huku nikiwa naendelea kupiga hatua kuingia sokoni waapii sioni mwanadada yeyote. Sauti inayoita ilikuwa inatokea kwa nyuma upande wa kushoto, nikageuka nyuma upande wa kulia nione anayeitwa pia hakukuwa na mwanamke karibu zaidi yangu. Nikiendelea kupiga hatua ile sauti ikaita tena, weee dada weeweeeβ¦ lote hilo lakooβ¦!!??
Nikajiuliza ni mimi itakuwa maana hakukuwa na mwanamke jirani, ilaβ¦β¦.. lote hilo lako ni nini? Mmhhh!! Nikapuuzia nikafanya manunuzi yangu. Wakati natoka napita palepale nilipoingilia huku nikiwa nimejitwisha kiroba cha matunda kadhaa nikasikia tena sauti, huyo anaondoka. Safari hii sikuweza kugeuka maana nilikuwa nahawahi daladala nifikishe mzigo mapema, biashara asubuhi jioni mahesabu.
Kilichonifanya nilete huu uzi, ile sauti nimeendelea kuisikia siku nzima leo, wee dada, weedada weeweeeβ¦.!! Lote hilo lakoβ¦!!?? Bado najiuliza lote hilo nini? Likichwa? Limikono? Litumbo? Mmmhhh kila nikijikagua sioni nina lininiβ¦!!
Najua kuna wataosema kesho nikamuulize, hapana sitomuuliza japo sokoni naenda kila siku, nimeona nisimulie hapa labda hiyo sauti itaacha kujirudia rudia.
Ahsanteni kwa kunisikiliza, Alamsiki.
View attachment 1606827
NB: Picha ni mfano, si uhalisia wa genge la Kasinde.
Kasinde Matata.
Kasie katika ubora wake anataka kutuaminisha kwamba anayo chura ya kuwafanya watu wapagawelote loakooooo
You included![emoji16][emoji16] my dada utakuwa ns mzigo wa kiwango gani hadi watu wakushangae...maana ta.ko sio habari tena siku hizi, asilimia 60 ya wanawake nimaokutana nao wamefungasha
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] aah wapiYou included!
Kasie mtata acha matata bhanaπππHabari za uzima kila mmoja pale alipo kutoka pembe nne za dunia.
Binafsi yangu ni buheri wa afya tele mwenye changamoto kiasi cha mboga, zilizo ndani ya uwezo wangu nazitatua kwa wakati na zilizo nje ya uwezo wangu napishana nazo kama bodaboda barabarani.
Twende kwenye mada kuu kabla sijachakachua hapo kwenye salamu. Leo nawaletea kisa kilichonitokea sokoni alfajiri wakati naenda kununua bidhaa kwa ajili ya kuziuza kwa wateja wangu wa huko kitongojini ninakokaa. Utangulizi kidogo, tangu mwezi wa saba mwaka huu, niliamua kufungua genge la matunda hapa mtaani ninapokaa maana magenge yako mbali kidogo na yaliyo karibu hayakuwa na matunda mengi na ukiyakuta basi yamesinyaa kwa kukaa sana gengeni.
Baada ya kuona uhitaji wa watu pale mtaani na kusikia wamama wawili watatu wakilalamika siku wakiwa na uvivu wa kwenda sokoni kufata matunda au wakihitaji matunda na muda wa kwenda sokoni ni hafifu. Basi nikakamatia fursa na kufungua kigenge pale mtaani, bi Kasinde nikakinakshi na mbaombao na makreti ya plastiki.
Ili kukidhi haja ya wateja wapate matunda fresh yaliyotoka sokoni siku hiyohiyo, nikaamua niwe naenda sokoni kila siku na gharama ya usafiri na hadi kuuza tunda nna faida yangu ya kujaza kibaba. Nikajiongeza kuweka baadhi ya bidhaa mbalimbali za gengeni zinazohitajika mara kwa mara majumbani.
Namshukuru Maulana kigenge kikazoeleka na kinawateja hadi wa mtaa wa pili na watatu kwa huduma bora, tabasamu na utani wa hapa na pale. Mteja akija gengeni kwangu si mtoto, kijana mzee lazima ataondoka na tabasamu na kesho atarudi tena. Mziki wa taratibu haukosekani gengeni kwangu kuniliwaza kipindi nasubiri wateja na saa ingine hunyanyuka na kucheza basi wateja burudaani ahahahaaa. Huo ni utangulizi looh, somo la muhtahsari wa habari sijui ntafaulu lini walaahiβ¦. Najikuta tuu nashindwa kufupisha habari. Haya tuendelee kabla sijasahau nlichotaka kusimulia heheeβ¦
View attachment 1606825
Kisa cha leo kwanza wakati natoka nyumbani Mbagala nilichelewa maana matunda mazuri kwa bei ya mkulima lazima niyadamkie alfajiri, hivo na zile haraka nikatoka bila vuvaa dera kwa juu badala yake nikaliweka kwenye mfuko wangu ambao huwa naweka kiroba cha kubebea matunda baada ya kununua, na nikasema nikifika sokoni ndo ntalivaa kwa juu ili kupunguza tafrani sokoni na kujihakikishia usalama wangu. Nilitoka nimevaa kaboka mchizi na blauzi ili nikifika sokoni nitupie dera niwe huru kuinama kuchagua matunda bila kuhofia kukaa vibaya.
Ile nimeshuka kwenye daladala natembea kwa haraka nikiwa naelekea sokoni nafungua mfuko wangu nitoke dera nivae, heeee..!! nakutana na mtandio wa deraβ¦.. Nikasimama ghafla na kujiuliza, sasa na hii kaboka mchizi na kiblauzi ntachaguaje matunda??? Si watu wataanza kuhesabu pingili kwenye mbavu looh!! Nikaishiwa pozi, nikasema nikienda hivihivi na kaboka mchizi masaburi yataleta za mbwatambwata, bora nusu shari kuliko shari kamili.
Kama askari hachagui bunduki kwenda vitani mradi ina risasi, basi nikajifunga mtandio wa dera nikaingia sokoni. Ile naingia nasikia sauti ya mwanaume inaita, weee dadaβ¦!! Wee dadaβ¦!! Weee dada weeweeeeβ¦!! Sikugeuka ila nikapiga jicho mbele sikuona mwanamke, piga jicho la kishushushu kulia na kushoto kwangu huku nikiwa naendelea kupiga hatua kuingia sokoni waapii sioni mwanadada yeyote. Sauti inayoita ilikuwa inatokea kwa nyuma upande wa kushoto, nikageuka nyuma upande wa kulia nione anayeitwa pia hakukuwa na mwanamke karibu zaidi yangu. Nikiendelea kupiga hatua ile sauti ikaita tena, weee dada weeweeeβ¦ lote hilo lakooβ¦!!??
Nikajiuliza ni mimi itakuwa maana hakukuwa na mwanamke jirani, ilaβ¦β¦.. lote hilo lako ni nini? Mmhhh!! Nikapuuzia nikafanya manunuzi yangu. Wakati natoka napita palepale nilipoingilia huku nikiwa nimejitwisha kiroba cha matunda kadhaa nikasikia tena sauti, huyo anaondoka. Safari hii sikuweza kugeuka maana nilikuwa nahawahi daladala nifikishe mzigo mapema, biashara asubuhi jioni mahesabu.
Kilichonifanya nilete huu uzi, ile sauti nimeendelea kuisikia siku nzima leo, wee dada, weedada weeweeeβ¦.!! Lote hilo lakoβ¦!!?? Bado najiuliza lote hilo nini? Likichwa? Limikono? Litumbo? Mmmhhh kila nikijikagua sioni nina lininiβ¦!!
Najua kuna wataosema kesho nikamuulize, hapana sitomuuliza japo sokoni naenda kila siku, nimeona nisimulie hapa labda hiyo sauti itaacha kujirudia rudia.
Ahsanteni kwa kunisikiliza, Alamsiki.
View attachment 1606827
NB: Picha ni mfano, si uhalisia wa genge la Kasinde.
Kasinde Matata.
Kasie katika ubora wake anataka kutuaminisha kwamba anayo chura ya kuwafanya watu wapagawe