Jamiiforums.com's three-month global Alexa traffic rank is 30,305. The site is located in Tanzania. Compared with internet averages, the site's audience tends to be users who browse from work; they are also disproportionately highly educated men between the ages of 25 and 45 who have incomes under $30,000 and over $60,000 and have more children. This site belongs to the "Mila na Sanaa" category. Roughly 27% of visits to Jamiiforums.com are bounces (one pageview only)........
Facebook.com ni$1,831,009,645
Kwa kuangalia hiyo value yao ya Facebook unaweza kuana kuwa hakuna ukweli wowote kwenye hizo values, Facebook iko valued at more than $60 billion kwenye open market.
Alexa inategemea statistics zinazotoka kwa watu walioinstall toolbar yao last time I checked, hii haiwezi kuleta accurate valuation.
Haya makadirio huwa yanapotosha sana kwasababu vigezo
wanavyotumia ni kama alexa ranking na (yahoo/google)
backlink.
Tatizo la alexa ni kuwa siyo wote wanaotumia hiyo addon
kwenye browser zao kwahiyo data zao siyo sahihi.
- Nilazima udownload alexa addon kwenye browser ili waweze
kukusanya data
Tatizo lingine ni kwamba mapato ya website yanategemea na
aina ya traffic. Unaweza kuwa na traffic kubwa sana (according
to alexa) kama ya twitter lakini ukashindwa kui-monetize.
Mfano mzuri ni facebook ambayo ina traffic kubwa sana lakini
mapato yake ni chini ya $1 billion kwa mwaka wakati huo huo
mapato ya google ni $23 Billion kwa mwaka.
Hii ni kwasababu watu wanapotumia google huwa wanatafuta
information kwa hiyo wanakuwa katika mood ya ku-click aidha
ads au SERP (search engine result pages). Wakati wale wa
facebook wanakuwa katika mood ya kuangalia nani kafanyanini.
Hivyo sirahisi kwa wao ku-click facebook ads ndiyo maana
mapato yake hayaendani na traffic yake.
Wanasema makadirio ya mapato ya Google ni $3,400,153.46
kwa siku, Hii siyo sahihi kwasabau Google wanatengeneza zaidi
ya $60 million kwa siku.
Mfano mwingine ni hii website ya magicofmakingup.com,ambayo
ni namba moja clickbank kwenye mambo ya self help. Huyu
jamaa anauza kijitabu chake pale clickbank na anatengeneza
zaidi ya $2,000 kwa siku lakini hawa jamaa wa sitetrail.com
wanasema hii website inatengeneza $144 tuu kwa siku, gimme
a break.
Kang uko sahihi lakini mfano tajiri mmoja anakuja kukuomba ushauri kama mtaalam wa IT kuwa anataka kuinunua Jamiiforums au issmichuzi Anataka ummpe kadirio la bei ya juu ya chini kama mtaalam wa IT Utamwambiaje.??
Na utatumia vigezo gani au tools gani kuthaminisha tovuti kama mthaminishaji huru.
Kwanu naona ni complex process. Hiyo thamani ya Facebook au google inawezekana ni uwa sana au ndogo but ni vitu gani wanazingatia. zaidi ya hits. utajuje kama watu wa wa FB au google hawaja cook data zao kuipaishia tovuti zao. I meana hao open markey wametumia vigezo gani.
lakini alexa haichukia data kutoka tu kwa watu wenye toolbar pekee . kwa mujibu wao wenyewe wamedvance analysiss mechanisma yao. though sijaelewa bado.
Utatatumia mbinu gani au tools gani kutambua value sahihi ya site kama issa michuzi?Au simply Blog ya issa michuzi unai value vipi kiasi gani na kwa nini ?
Ila siyo niche zote zinalipa kunabaadhi zinapesa zaidi mfano golf, Mesothelioma, online gambling (sasa hivi ni illegal US), dentist in (weka mji), win a lottery etc. Sababu ya hizi niche kuwa na faida ni kwamba watu wanaohusika na mambo haya hawafikirii sana kutoa pesa kupata wanacho kitaka.Unajua tovuti yangu ina wapenzi wengi sana wa Nintendo wii, ngoja nikuonyeshe stats zangu uone jinsi wanavyo penda kuvinjari hapa na kama utaweka matangazo yako hapa (adsense) utaweza kupata walau (with disclaimer) kiasi hiki.
Kuongeza value kwenye paid subscription site unaweza kusema, "nimetengeneza hii software amabayo itaweza kuongeza memba 10 kwa siku hivyo utaongeza memba 300 ($9000) kwa mwezi, hebu fikiria mwenyewe jinsi utakavyo tajirika bila ya kuhanganika. Wewe unachofanya tuu ni kumiliki tovuti na pesa inaingia benki kama vile unamiliki ATM
Kwanza kabisa naomba ieleweke sitazungumzia value za tovuti za makampuni makubwa kwasababu wao wanajumuisha vitu vingi mfano asset, stock, technology, patents, employee, na mambo mengine mengi ambayo ni yakinadharia zaidi.
Kuhusu blog ya michuzi (na blogger/worpress hosted blogs kwa ujumla) kwakweli siwezi kusema mengi kwasababu japokuwa watu wanasema ni yake ukweli ni kwamba siyo yake, yaani siyo mmiliki wa blogspot.com domain, mmiliki halisi ni google. Google wanaweza kuifuta wakati wowote unless kama amebackup content. Kwahiyo ni vigumu kupata kadirio halisi wakati haumiliki tovuti 100%..........................................................................
So ku evalueate Michuzi or JF itabidi uangalie log/Analytics zao kisha uamue value yake.
Hili ni tatizo kubwa kwasababu hauna control mfano kama unataka kuongeza madoido kweneye tovuti kwa ku-install forum script kama hii ya JF (vBulletin) ili watu wachangie au kuweka elgg script ili uongeze interactivity ya social networking, haya mambo hayawezekani kwenye blogspot.com kwasababu hauna control ya root domain.Thanks kwa maelezo mazuri mkuuu
Lakini hata kama blogsopt ni mali ya google bado zinaweza kuthaminishwa. Nadhani sio tatizo.
Sababu hata ukimiliki tovuti 100% unaweza usiwe na hata 1% ya umiliki wa server harware ilipo tovuti. So kwangu kigezo cha blogspot kuwa mali ya google haizuii uthaminishaji. may be sema tovuti kuwa chini ya kivuli cha blogspot au wordpress .inaogeza risk na kupunguza value ya tovuti.
sasa turidi kwenye mada . alexa na hao wengine wametoa data zao za thamani ya Jf na issa michuzi.Je kwa mtazamo wako zinaendana na uweli? Ni kubwa sana ni ndogo sana
Hazitakiwi kuzingatiwa kabisa. kama hazitakiwi kuzingatiwa kabisa can u come with approximate figure.
Sijui hata wakuu wa jf wenyewe wanaithaminisha vipi tovuti yao? Just curious to know.
Kwahiyo tunarudi pale pale kuwa mambo haya ni kama uzuri wa mwanamke inategeneana na mtu.
Ndio maana nakuuliza unipe model inayoweza kuzaa formula na kuja na specifi value. ya hii site xyz.
...............Nafikiri hii itakuwa ni project nzuri sana na nina pendekeza iwe ni yet another mtazamaji project at JF.
Kama tutazingatia factors nyingi tatakaribia kwenye ukweli kwa mfano tukiangalia haya:
...........................................
- potential traffic increase
- Any legal issues (has the site been sued before?)
- alexa ranking
- google pagerank