Jinsi ya kujiajiri kupitia wordpress

tzhosts

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
380
468
logo.gif


Je Umewahi kusikia kuhusu Wordpress?

Kama hujawahi basi ni kujuza tu kwamba wordpress ni content management system(CMS) kwa ajili ya website.CMS ni mfumo maalum ambao unamwezesha mtengenezaji wa tovuti kusimamia maudhui ya tovuti yake kwa urahisi.Wordpress ni nzuri sana kwa kusimamia blogs lakini hata tovuti za kawaida pia unaweza kuitumia.Kuna wordpress za aina mbili ambazo ni wordpress.org ambayo hii inahusika zaidi na usimamizi wa mfumo wenyewe kama mradi wa open source ambao watu mbalimali huchangia katika kuboresha mfumo husika na kutoa updates mara kwa mara.Mfumo mwingine ni wordpress.com ambao hawa hutumia mfumo huu kwa ajili ya kutoa huduma za kuhost websites.Hata hivyo kwa sasa hivi huduma kama hio ya wordpress.com inatolewa pia na kampuni nyingi ikiwamo mimi.Ndio tzhosts.com pia inatoa huduma ambayo inafanana na huduma ya wordpress.com.

Leon nimeona sasa niwaeleze namna ambavyo unaweza kujiajiri kwa kutumia wordpress kama zana yako ya biashara.Kuna namna nyingi ambazo unaweza kuamua kuweka mfumo wake unaofanana na wordpress.com.Njia ya kwanza ni kwa kununua server kutoka kwa wauzaji wa whole sale wa servers.Unaweza kununua server yenye cpanel au unaweza kununua server yoyote hata kama haina cpanel mradi uwe na uzoefu wa kusimamia na kuiendesha.Cpanel inarahisisha usimamizi wa server yako kwa kukupa user interface na hivyo hulazimki kutumia command line(CMD).Kwa kawaida server utakayonunua inaweza kuwa ni ya windows au ni ya LINUX.Kwa ushauri wangu na uzoefu wangu server za LINUX ni bora kwani kwanza ni bure,pili ni maarufu na salama.Iwapo kuna ulazima wa wewe kutumia server yo window hakuna tatizo.Nitoe tu angalizo kwamba ninapotumia neno server usifkiri naongelea kitu kipya hapana.SERVER ni operating system kama ilivyo windows 10 kwenye computer yako ambayo imeondolea zile functionality za kidesktop na kuwa special kwa ajili ya kuhudumia computer nyingine.Ndio maana unaweza kutumia computer yako ya kawaida kuwa server kwa kazi mbalimbali.Ili compyuta yako iwe web server inahitaji kuwa na mfumo maaluma wa kusimamia wavuti ambao unaweza kuwa ni apache,ngix au kwa upanda microsoft IIS.

Hata hivyo kama ni kwa ajili ya kujifunzia unaweza kuinstall program maalum kama WAMP stack kwa upande wa windows ambapo hii hukuwezesha kuweka mifumo yote ya lazima ya kufanya computer yako iweze kufanya kazi kama web server.

Nirudi sasa kwenye wordPress.WordPress kama CMS ina uwezo mkubwa sana.Imetengeneza kwa kutumia php na kuungwaa na Mysql kam database na taarifa zako zote ikiwamo post zitatunza na kusimamia na mfumo huu.Wordpress inakuwezesha kusimamia tovuti yako kwa urahisi kwani inakuja na Plugins na Themes ambazo zinafanya utengenezaji wa tovuti uwe rahisi.Kwa kutumia wordpress unaweza kutengeneza website nzuri ndani ya muda mfupi sana.Iwpo unao ujuzi wa CSS(Cascading Style Sheet) na html + php basi unaweza kutengeneza theme yako mwenyewe au ukarekebisha theme zilizopo kwenye wordpress ili ziwe vile unataka.

Unawezaji kujiajri katika wordpress?Kuna mbinu nyingi za kujiajri kupitia wordpress.Baadhi ya njia hizo ni kuwa developer wa themes na kuziuza,developer wa pluggin na kuziuza.Customizer wa themes na plugins kwa ajili ya watumiaji tofauti.Unaweza kuwa Blogger na kuweka matangazo katika blog yako huku ukiandika makala mbalimbali na unaweza kutoa huduma ya kufanya Hosting ya wordpress site.Ndio

Watu wengi sana wamezoe kuuza hosting kwa kutumia Reseller program amazo zinakuja na cpanel licenses kadhaa ia kwa kupitia wordpress hutakuwa na haja ya kununua leseni nyingi za cpanel.Unanunua leseni moja tu au kama wewe ni mtundu wa Command line basi unaachana na cpanel na unaweka Control panel nyingine ya BURE ambazo nazo ni nafuu na rahisi kutumia.Kwa wale ambao wanamiliki website watkuwa wanaelewa umuhimu wa kuwa na Panel na jinsi inavorahisisha usimamiz wa server.Unaponunua server yako unaweza nunua dedicated server au ukanunua shared server.Kama ndo unaanza nunua shared sever kwanu huwa ni nafuu ingawa integrity yake huwa ni ndogo na unaweza kuwa limited.Kama ni mzoefu nunua dedicated server ingawa bei inaweza kuwa juu ila utapata thamani ya pesa zako.Kwa kuwa lengo lako ni kuuza huduma za wordPress itakulazima kuinstall wordpress kwenye server yako na kuifanyansetup za multisite ili iwe na uwezo wa kufanya kazi kama wordpress.com.

Baada ya kusetup site yako unaweza kuamua iwapo unataka watu wawe na uwezo wa kutengeneza blog wenyewe au lazima wakulipe kwanza ndo uwatengenezee.Hizi zote zitahitaji wewe ujifunze na kuelewa ufanyaji kazi wa wordpress na jinsi unavoweza kutumia pluggin kuongeza uwezo wake.Kumbuka kwa kutumia wordpress unaweza kutengeneza mifumo ya aiana mbalimbali ikiwamo E-commerces sites,online learning systems,forums directory na membership sites kwa gharama nafuu sana.Gharana za kuhost kwa kupitia wordpress ni nafuu zaidi kuliko traditional hosting na kwa wastani unaweza kutengeneza faida ya kati ya shilingi milion 1 hadi 3 kwa mwezi kwa kutegemea masoko yako na uwezo wako wa kufanya kazi.


Je unapenda kujifunza jinsi ya kuanzisha hosting Business kwa kutumia wordpress pekee?Je unapenda kujiingiza katika biashara ya kuuza na kusambaza huduma za hosting kwa gharama nafuu.Tuwasiliane kwa email info@tzhosts.com au blog4moneytz@gmail.com ili tukufahamishe kuhusu fursa zilizopo katika ulimwengu wa kidigitalia

Karibu ujifunze
 
SME nikampuni ya uhakika kutoka Marekani inayolipa kwa masaa, kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi, miezi hadi mwakaa

Naweza kujiungaje??

Jisajili kwa line yako kisha downlod App ya kampuni utakutana na offa yako ya Tsh 10,000/= iwekeze ukitaka uanze kuvuna faida 🤑🤑

Malipo hufanyikaje??

Malipo yote hufanyika Kwa njia mbili kama ifuatavyo👇

M PESA na mfumo wa USDT Kwa wale wenye Wallet

Vifurushi vyake vikoje??

Baadhi ya vifurushi vyake ni hivii hapa 👇

Ukiweka Tshs 30,000/= utapokea sh. 1440 kila siku kwa siku 7 kwa muda wa wiki 5

Ukiweka Tshs 80,000/= utapokea she 4320/= kila siku kwa mda wa siku 15 kwa muda wa wiki 10

Ukiweka Tshs 200,000/= unapokea shs 12,000/= kila sikuu kwa siku 30 kwa miezi mitano

Ukiweka Tshs 500,000/= Utapokea shs 34,000/= kila sikuu kwasiku 60 kwa miezi 10

Utawekeza tena na tenaa

Withdrawal

Kiwango cha chini cha utoaji ni Tsh 5000/= kwa njia ya m-pesa au USDT

withdrawal fee ni 15%

Jisajiri link


Ingia kwa group 👇
 
Kuweni makini kuhusu biashara za kuresale host unaweza ufanye ilimradi uwe na domain kisha unaingia kwa tovuti zinazohost napendekeza hii ifastnet.com kisha chini kabisa kunahiyo option wabongo hawaaminiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom