Unajua hili la kupiga, huwa nalitafakari sana halafu nashindwa kupata jibu.
Unampiga mkeo, kisa? I mean kosa gani linalostahili kipigo? (kukutukana, kukusaliti, kutokukupikia au?
Mfano kakutukana, maana yake si hakiheshimu; sasa ukimpiga ndio ataanza kukuheshimu?
Au labda umekamata text message ya mapenzi; ukimpiga ndio utamfutia feelings za huyo anacheat naye?
Au una mpiga kwa kuwa umekasirika:
Je kupiga ndio reaction yako kila unapokasirika? Boss wako akikukasirisha unampiga? Au mwanaume mwenzako unampiga? Obvious ni hapana.
Unampiga mkeo kwakuwa ni dhaifu wewe (coward), umeshindwa kureason naye ndio maana unaishia kupiga mtu ambaye si sawa yako, kwa maana hawezi kujitetea. Na kwa ukawardi wako huna uwezo wa kumuacha au kumfanya akupende, akuheshimu kama mwanaume. Ukawardi wako ndio umemfanya akudharau in the first place. Kipigo sio tu kitaongezea dharau bali kitaleta chuki na uhasama pia.
MWANAUME hapigi mwanamke, bali anasababisha respect, admiration, love n dependency.
Hii ni conclusion niliyofikia mimi Kaunga.