We got your back Paul, we the good citizens of Dar es Salaam

Gondwe

JF-Expert Member
May 30, 2014
235
170
Huyu Mh. Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam kwa kweli hapo mwanzo sikuwa namkubali kabisa hasa wakati anapewa ukuu wa mkoa.

Hii ni kutokana na zile story za kumpiga mzee Warioba, ila tokea aanze utendaji kama mkuu wa mkoa nikajikuta nampenda sana kutokana na utendaji wake.

Watu walipoanza kumchafua na kumpiga mawe kutokana na vita ya madawa ya kulevya automatically nimejikuta mapenzi yanazidi kwake, coz kwa mtu yoyote mwenye akili timamu na mwenye fikra basi lazima atajiuliza kwa nini watu wanamshambulia that much, hata mtu aliyeua hashambuliwi hivi!

Nikatumia akili zangu nyingi kutafakari na kugundua kuwa wanaompinga wote wana maslahi either kwenye madawa ya kulevya ama ushoga ama ukahaba.

I love you Makonda na naihofia sana Dar Es Salaam bila Makonda, Go go go Makonda we got your Back
 
Yeye sio wa kwanza kushambuliwa kuhusiana na maswala ya elimu,alishambuliwa Zitto Kabwe,akakata fitna kwa kuweka hadharani ukweli kuhusu elimu yake.

Alishambuliwa Mwigulu akaweka wazi ukweli wa Elimu yake,kelele zote zikakoma.

Alishambuliwa John Mnyika,akajitokeza mbele ya umma akaeleza ukweli,kelele zote zikazima automatically.

Ndugu Luhenge baada ya kuteuliwa na Mh.Rais kuwa mkurugenzi wa moja ya halmashauri hapa nchini,ulizushwa uvumi kuwa elimu yake inatia shaka,mbele ya vyombo vya habari Mh.Rais alimtaka ndugu Luhenge kuonyesha vyeti vyake,alifanya hivyo na waliokuwa wanamshambulia walichutama kuficha aibu,mpaka leo hakuna mtu aliyemshambulia bwana Luhenge,

Swali,ni kwa nini ndugu huyu anasita kuwatia aibu wanaomshambulia kwa kuweka hadharani ukweli kuhusu elimu yake!!!
TUNAUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA,LAKINI HIYO HAIHALALISHI UVUNJIFU WA SHERIA KWA NAMNA YOYOTE ILE,AWEKE VYETI NA KUSEMA UKWELI KUHUSU ELIMU YAKE HADHARANI,BAAAAASI!!
 
Ongelea umoja maana uko peke yako usituzungumzuie! Sema " I " and not "we"
Tuko wengi sema tu tuko busy na kazi, halafu mbona kutwa kucha mnamchafua Mkuu Makonda tumekaa kimya, thread moja tu mnatokwa povu, tatizo wengine wenu hamna mapenzi ya dhati kwa hii nchi, ntatafuta platforms za kisiasa
 
Kama kuna mtu anasimama na kutetea Uhuni wa kuforge vyeti kwa sababu nyepesinyepesi kama hizi jua wazi kuwa hata yy kaforge vyeti hajui ugumi wa kukipata cheti au alipata sifuri na akabebwa hiyo Naye haujui uchungu wa kuforge.
Wacha maneno leta ushahidi wa wapi kaforge vyeti, unaongea na watu wazima na sio watoto, zaidi ya maneno ushahidi wa facts uko wapi? No evidence no right to speak,
 
Tuweke chuki binafsi pembeni Makonda pamoja na mapungufu yake kama binadam amefanya kazi kubwa sana hayo mapungufu mengine anaweza kuyarekebisha tumpe muda afanye maamuzi ya kiungwana kama kuna mahara amekosea akiri kwa kinywa chake
 
Wacha maneno leta ushahidi wa wapi kaforge vyeti, unaongea na watu wazima na sio watoto, zaidi ya maneno ushahidi wa facts uko wapi? No evidence no right to speak,
Mshauri asilie alete vyeti kama una nia ya kumsaidia
 
Back
Top Bottom