TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye amezungumza na vyombo vya habari juu ya uamuzi wa Serikali kulifungia gazeti la Mawio.
Katika Press hiyo iliyofanyika leo maelezo Mhe Nape amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa taarifa zinazoandikwa kwenye Magazeti ni sahihi na zenye kuaminika.
Nape amesisitiza kuwa uamuzi huo hauna lengo jingine lolote na hautokani na sababu nyingine yeyote isipokuwa ni kujenga na kuimarisha mfumo wa habari wenye ukweli na weledi unazingatia taaluma na Uzalendo kwa Taifa.
Kwa miaka mingi kumekuwepo na utaratibu wa watu kuandika habari zenye kuchafua wengine bila ushahidi, habari za uongo na uzushi zikakithiri kwenye media na sasa utamaduni huo wa zamani umefika mwisho. Sio tu kwa kufungiwa Mawio bali mengine yamepewa onyo na yako mengi zaidi yatafungiwa ikiwa hayatazingatia sheria, kanuni na miiko ya tasnia ya Habari nchini.
Zama za kuandikana kwa visasi zinaelekea kuisha Tanzania na hakika tunajenga taifa la watu wenye kuheshimiana na kuthaminiana.
Serikali imesema itahakikisha inaimarisha mahusiano yake na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari...