WB yamwaga dola milioni 653 kwa miradi mbalimbali nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WB yamwaga dola milioni 653 kwa miradi mbalimbali nchini

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Benki ya Dunia (WB), imeikopesha Tanzania dola za Marekani milioni 653 kusaidia miradi ya barabara, kuboresha miji, kilimo, pamoja na huduma za jamii kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kwa kipindi cha miaka mitano.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kadhalika, kiasi kingine cha dola milioni 12.5 za Marekani kimetolewa kama msaada na nchi ya Denmark kwa Tanzania ili ujenzi wa miji kwenye maeneo ya mijini katika mikoa mbalimbali nchini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkurugenzi Mkazi wa WB katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, John Murray Mclntire, alisema fedha hizo zitasaidia juhudi za serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema fedha hizo zitasaidia kujenga kilomita 1,181 za mtandao wa barabara katika mikoa mbalimbali. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kadhalika, alisema fedha hizo zitasaidia ujenzi wa viwanja vya ndege vya Bukoba mkoani Kagera, Kigoma na Tabora pamoja na kuboresha barabara eneo hilo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kati ya fedha hizo, dola milioni 186.5 za Marekani zitatumika kujenga barabara ya kutoka Korogwe hadi Same yenye urefu wa kilomita 172 na Arusha hadi Minjingu kilomita 98.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, WB kwa mara nyingine imetoa mkopo wa dola milioni 35 za Marekani kwa ajili ya mradi wa Tasaf namba mbili ambapo mara ya kwanza benki hiyo ilitoa dola milioni 30 za Marekani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkurugenzi huyo alisema fedha hizo zitasaidia upatikanaji wa chakula pamoja na kusaidia watu wasiokuwa na uwezo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Fedha nyingine zilizotolewa na WB ni dola milioni 163 za Marekani kwa ajili ya kuimarisha miji katika maeneo ya mijini ambapo Uingereza imeongeza fedha hizo kwa kutoa msaada wa dola milioni 12.5 za Marekani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Fedha hizo ni kwa ajili ya kuboresha makazi ya miji katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya, Mtwara, Kigoma na Tanga.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wa elimu, WB imetoa mkopo wa dola milioni 150 za Marekani kusaidia elimu ya sekondari.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika kilimo alisema WB imetoa dola za Marekani milioni 35 kama mkopo kuboresha sekta hiyo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema fedha hizo zitatumika kufidia pengo lililopo katika miradi ya umwagiliaji katika ngazi ya wilaya.[/FONT]
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mie sielewi serikali yetu hata kidogo wanasema wana deficit wanahitaji kukopa sasa wanapewa mkopo wa almost bilioni 700 hizi pesa zinaenda wapi?
   
Loading...