WB yaipa Ilala Sh41 bilioni kuboresha miundombinu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WB yaipa Ilala Sh41 bilioni kuboresha miundombinu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 9, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuesday, 07 August 2012 20:09

  [​IMG]Pamela Chilongola
  BENKI ya Dunia (WB) imetoa mkopo wa Sh41 bilioni kwa ujenzi wa miundombinu Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

  Fedha hizo ni sehemu ya Sh150 bilioni ambazo ziliombwa na halmashauri nne za Dar es Salaam kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

  Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani, Meya wa Ilala, Jerry Silaa alisema Serikali iliomba mkopo WB kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya Da es Salaam.

  Slaa alisema miundombinu hiyo ni barabara, mifereji ya maji, uzoaji taka, urasimishaji makazi, uboreshaji mapato ya halmashauri, ujenzi wa miundombinu kwenye makazi yasiyopangwa na utawala bora.

  “Uboreshaji miundombinu ya barabara na mifereji ya maji ya mvua, zimetengewa Sh21 bilioni, ukusanyaji na usafirishaji taka ngumu umetengewa Sh5.3 bilioni, uboreshaji miundombinu kwenye makazi yasiyopangwa Sh 8.4 bilioni,” alisema Slaa na kuongeza:

  “Urasimishaji na kutenga maeneo ya huduma kwenye makazi yasiyo rasmi imetengwa Sh1.6 bilioni.”
  Pia, alisema mradi huo ni wa awamu ya kwanza ambayo itahusisha kata za Kiwalani, Gongolamboto na Ukonga na kwamba, wakimaliza wataingia awamu ya pili.

  “Uboreshaji huo utakuwa Kata ya Kiwalani mitaa ya Minazi mirefu, Yombo, Kiwalani na Kigilagila; Kata ya Gongolamboto itahusu mitaa ya Gongolamboto, Ulongoni, Guluka Kwalala na Mongolandege na Kata ya Ukonga mitaa ya Makazi, Mazizini na Mwembe madafu,” alisema.

  Naye Diwani wa Kata ya Kivule, Nyasika Getema alisema kwenye kata yake ametengewa Sh6.29 milioni kwa ujenzi wa barabara ya Mombasa-Moshi bar.
   
 2. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Vichekesho vitupu yani hadi uboreshaji mifereji tunaomba pesa worldbank? na je yale navinyesi ya wahindi yanayomwagwa kule vingunguti spenco jelly silaa ufikirii kama yanahatarisha maisha ya wakazi kule? basi mngetenga kama bil 7.2 kati ya hizo kutengeneza underground infrastructure mpaka baharini kaeni chini tafakarini msijifanye kuwa magamba ni kupanga jinsi ya kufisadi tu.
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapo sasa! Upembuzi yakinifu, mchakato, mchakato, mchakato, hela kwisha! Miundombinu hakuna! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
   
Loading...