Litwapasi waboreshewa Miundombinu ya Majisafi

Litwapasi waboreshewa Miundombinu ya Majisafi

DAWASA

Official Account
Joined
Oct 7, 2010
Posts
201
Reaction score
121
Wakazi zaidi ya 200 kunufaika na maboresho hayo

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la uboreshaji wa miundombinu ya mabomba ya maji ili kuimarisha huduma ya maji katika Barabara ya Litwapasi, Mtaa wa Taifa, Wilaya ya Temeke ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma ya Maji Kwa wananchi.
​
WhatsApp Image 2026-08-21 at 18.22.00.jpeg

​
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mhandisi Moses Mbonye, kutoka Mkoa wa Kihuduma DAWASA Temeke amesema uboreshaji huo umekusudia kuimarisha huduma Kwa wakazi wa Sorele, Litapwasi, Msweke, Taifa ambao wamekosa huduma kutokana na Matengenezo ya miundombinu ya Barabara yanayoendelea.

"Maboresho haya yametokana na ukarabati wa Barabara unaoendelea ambapo miundombinu ya DAWASA iliathirika, ubadilishaji unafanyika Kwa kubadilisha mabomba ya zamani ya inchi 4 na kuweka mapya kwa umbali wa kilomita 1.2 ambapo zaidi ya wateja 200 watanuifaika na maboresho hayo." amefafanua Mhandisi Mbonye.
​
WhatsApp Image 2026-08-21 at 18.21.49.jpeg

​
Uboreshaji wa miundombinu Kwa kutoa ya zamani na kuweka mipya ni sehemu ya jitihada za Mamlaka katika kuhakikisha Huduma ya uhakika ndani ya eneo lake la kihuduma​
 
Back
Top Bottom