Imesemwa hapa ni Chit-Chat kwa hivyo tusiyape umuhimu yale wanayoyasema, lakini mimi nahisi uhalisia wa mtu huonekana kwa maneno yake kwani kinachotoka mdomoni (in this case kwenye keyboard) ndicho kilichomo mawazoni mwake. Mtu wa aina hii hata aingie jukwaa gani, liwe hili, MMU, Siasa, Doctor...kamwe habadili hulka yake. Maoni yake yanafanana popote aingiapo, hata ukimtia chupani.
Cha kutia moyo, wakati wao wanahisi kuwananga wenzao ndio kujikweza kwao, kinyume chake ni kujionesha ni kwa kiasi gani bongo zao zimefilisika. So Lizy, YM, Kigarama, Rejao, Nitonye....wasameheni bure watu wa namna hii, hawajijui wala hawajui wakisemacho bali wakiwazacho.