Wazushi mtandaoni. . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazushi mtandaoni. . .

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Lizzy, Feb 1, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ni rahisi kweli watu kuwa nyuma ya computer na kumuattack /bash a.k.a kumponda mtu mwingine kwa muonekano wake hata kama mpondaji hamjui mhusika kwa sura kwasababu tu yeye haonekani. Yani anapata confidence ya bandia ambayo uraiani hana na kushambulia wale wasiomuona/wasiomfahamu.

  Je. . .hawa watu wao sura na maumbo yao binafsi yanalipa kweli hata wawezeze kuwakashifu wengine? Wakijiangalia kwenye vioo wanajifurahia?Wanajipenda?Mitaani wanaangalika mara mbili au ndio hasira za kutokua na hayo yote wanashushia kwa wenzao?
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Lizzy Luu..

  kwa maoni yangu ni kwamba kuna watu wanadhani wao ni wazuri kuliko wengine..
  na wameshajiwekea picha fulani kichwani mwao kuwa mtu mzuri yuko hivi.. na hivyo
  ndivyo ilivyo hiyo picha ikija vingine basi..

  haya sasa
  kuna wale ambao watafanya wawezalo kumuweka mtu mwingine chini ili wao wajisikie
  vizuri.. Hawana ile "Self esteem" mpaka wamponde au waongee maneno fulani mabaya
  kuhusu mwingine...

  either way
  Dunia ni jalala la maonyesho..
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kiukweli kabisa Lizzy sio mtandaoni tu ingawa kwenye mtandao ndio inaweza kuwa asilimia kubwa ila hata huku mtaani unasikia mtu anasema yule dada ana miguu kama spoku za baiskeli wakati yeye hajajiangalia au hajui kuwa kuna watu na yeye wanamuongelea vile vile. Ila hii ya mtandaoni imekithiri sana mfano mzuri tu ni juzi pale BC kuna jamaa alikuwa kwenye Skype akasema mbona fulani (sitaki kutaja jina lake) sura yake nzito tofauti na avatar yake kwa kweli nilijisikia vibaya ila nikaamua kupotozea tu na huyo member aliyemsema hivyo mwenzake namkumbuka vizuri...
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Weee Kurwa unaweza ukawa unajiona ni mzuri ukahangaika kuponda wengine kweli?
   
 5. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lizzy pole bibie najua mashambulizi dhidi ya Young Master kwenye ile siredi yamekukwaza lakini ndiyo dunia ilivyo. Nafikiri siyo kwenye sura tu hata kwenye "core issues" za kitaifa watu wanawashambulia wenzao kwa sababu tu wao hawaonekani kiuhalisia wao. Kuna watu hapa ikiwekwa sheria ya kujitambulisha kiuhalisia wote watafutika ghafla!
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Loh. . watu bana!!
  Hapo angeambiwa aonyeshe yake tuone kama ni laini tofauti na anaemponda basi, kama tusingeshangaa basi tungekimbia!!
   
 7. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  duhhhhhhh TF nimejaribu kucheka lakini imeniwia vigumu...
   
 8. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Sio mtandaoni, hata hadharani wapo wanaowaona wengine si chochote wakijilinganisha nao. Ila wanapopata nafasi ya kujitafakari wanajijua si lolote, hivyo kuneutralize ya moyoni kwa kinachotaka nafsi wanaishia kujikweza na kuwananga wengine
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kigarama nilikua naifikiria hii ishu mapema kweli kwasababu nilishaona kipindi kile cha msiba Regia. . .
  Ila hii ya YM kwakweli imezidi. Kuna wengine hata kama sio hapa hua wanasababisha wenzao wanapoteza kabisa kujiamini, na wale wadogo wadogo wanafikia hata kujiua.

  http://www.metro.co.uk/news/870057-suicide-teen-natasha-macbryde-was-bullied-online-even-after-her-death
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Uzuri na urembo upo ndani kwa nje mnajiongopea-FidQ
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ukimwambia aweke ya kwake sasa...kuna msemo unaosema wale wanaoponda sura za wenzao mara nyingi huwa wanakuwa na inferiority complex
  Lol...acha tu ndio mambo yalivyo mtaani mixer mtandaoni..
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Doto ,
  Kumbuka kuna watu ambao hawaridhiki na walicho nacho ..
  waweza kuwa wazuri wa kila kitu nje "mwili" lakini bado something is missing
  kwa hiyo kwa wao kujisikia vizuri ni kupoteza muda wao kuponda au kutosifia
  wengine ili nafsi zao ziridhike... Shame on them ...
   
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Lizzy huku duniani kuna watu kazi yao ni moja tu, kujikweza wao na kuwashusha wenzao! Yaani mtu anahakikisha kila unachofanya/sema anakikosoa tena sio kwa lengo la kukusaidia ila kwa lengo la kukufanya uache kujiamini... Kwenye uzi wa YM hilo pia limejitokeza na asipoangalia anaweza akajishusha thamani na kuanza kujichukia, sijajua wametumia vigezo gani kukosoa ile picha yake manake kiukweli vile ndivo ambavyo Mungu amemuumba!... Kabla hatujamua kuwashambulia wenzetu mara sijui ana sura mbaya, miguu mibaya, anaenda kama anarudi hebu na tujitizame je unayeshambulia mwenzako wewe u mkamilifu kiasi hicho?
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mbaya sana, badala ya kuangalia mapungufu yao watafute namna ya kuyarekebisha ama kujipendezesha kama inawezekana wanakomaa na watu wengine.


  Uzuri upo ndani na nje. . . wanaochagua mmoja ndio wanaojiongopea.

  Kaaaazi kweli kweli!!!
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Yaani wamenishambulia hadi nimekosa raha! Hii dunia tabu tupu
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Shame on them indeed. . .
  Wanahitaji somo la kujiamini!!
   
 17. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  prrrrrrrr!!hawana lolote hao lizzy,...sura zao kama avatar za watu fulani humu...nitonye, mphamvu na wengine wafananao na hao....
  wangekua km preta cjui ingekuwaje!?!loh!!
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli ubinadamu kazi!!
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Waambie wewe Lizzy maana nikisema mimi watasema waje wanikague
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole bana. . . .
  Unafanya kupotezea tu maana mpaka hapo umejua wao sio bora kuliko wewe.
   
Loading...