Wazungu wanatuchanganya sana

Mr.Wenger

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
2,558
6,091
Wakuu kuna mambo mengi sana wazungu wametukoroga koroga lakini me nataka kujua mambo mawili yafuatayo;

1.Usomaji wa SAA
Kwanini mshale ukiwa kwenye 9 tunasema saa tatu au ikiwa kwenye 10 tunasema saa nne. Kwanini saa isisetiwe ili iweze kusomeka kama invyoonekana yaani kama mshale upo kwenye tisa iwe ni saa tisa. Au saa ziwekwe kwenye mfumo wa masaa 24 tuanze kuhesabu moja mpaka 24. Hivyo walivyoweka lengo lilikuwa ni nini na kwa faida gani?

2.Weekend (mwisho wa wiki)
Kwanini Jumamosi na Jumapili zinachukuliwa kama weekend (mwisho wa wiki) wakati tafsiri sahihi ya neno mosi na pili inaonesha ni mwanzo. Sasa iweje jumatatu ndo wiki inaanza na si jumapili? Naomba wataalamu wa kiswahili mje mtujuze nini lengo la kusema wiki inaanza jumatatu
 
Unahaki ya kurekebisha saa yako ikawa katika lugha ya kiswahili, kwa Kiingereza j'pili ni Sunday na Saturday ni j'mosi
 
Mimi naweza kubadilisha hata mshale ukikaa kwenye tisa mimi nikaisoma kuwa saa 12!! Ila kwa nini hii ya wazungu imerasimishwa kiasi hicho? Maana hadi shule ya msingi tulifundishwa hivyo kuwa mshale ukikaa kwenye saba basi ni saa moja!! Swali la kwanini ndiyo limeegemea hapo.
 
Kama umesoma sayansi basi utaelewa kuna kitu kinaitwa SI unit (standard international units) kwenye mambo mbalimbali
 
Wakuu kuna mambo mengi sana wazungu wametukoroga koroga lakini me nataka kujua mambo mawili yafuatayo;

1.Usomaji wa SAA
Kwanini mshale ukiwa kwenye 9 tunasema saa tatu au ikiwa kwenye 10 tunasema saa nne. Kwanini saa isisetiwe ili iweze kusomeka kama invyoonekana yaani kama mshale upo kwenye tisa iwe ni saa tisa. Au saa ziwekwe kwenye mfumo wa masaa 24 tuanze kuhesabu moja mpaka 24. Hivyo walivyoweka lengo lilikuwa ni nini na kwa faida gani?

2.Weekend (mwisho wa wiki)
Kwanini Jumamosi na Jumapili zinachukuliwa kama weekend (mwisho wa wiki) wakati tafsiri sahihi ya neno mosi na pili inaonesha ni mwanzo. Sasa iweje jumatatu ndo wiki inaanza na si jumapili? Naomba wataalamu wa kiswahili mje mtujuze nini lengo la kusema wiki inaanza jumatatu

Kaka nadhani Kiswahili kimechanganya kiasi cha kuona kiingereza kina makosa,
Kiswahili kina mchanganyiko mkubwa wa Kiarabu, Kibantu na hata hicho kiingereza chenyewe

Kwenye habari za siku, Waarabu wao siku ya kwanza ni Jumamosi, kwa wayahudi wao siku ya kwanza ni jumapili, so sisi tuko kwenye kiarabu kwamba jumamosi ndio siku ya kwanza, lakini kwa kiswahili cha Kikongo, Jumatatu ndio siku ya kwanza
 
Wakuu kuna mambo mengi sana wazungu wametukoroga koroga lakini me nataka kujua mambo mawili yafuatayo;

1.Usomaji wa SAA
Kwanini mshale ukiwa kwenye 9 tunasema saa tatu au ikiwa kwenye 10 tunasema saa nne. Kwanini saa isisetiwe ili iweze kusomeka kama invyoonekana yaani kama mshale upo kwenye tisa iwe ni saa tisa. Au saa ziwekwe kwenye mfumo wa masaa 24 tuanze kuhesabu moja mpaka 24. Hivyo walivyoweka lengo lilikuwa ni nini na kwa faida gani?

2.Weekend (mwisho wa wiki)
Kwanini Jumamosi na Jumapili zinachukuliwa kama weekend (mwisho wa wiki) wakati tafsiri sahihi ya neno mosi na pili inaonesha ni mwanzo. Sasa iweje jumatatu ndo wiki inaanza na si jumapili? Naomba wataalamu wa kiswahili mje mtujuze nini lengo la kusema wiki inaanza jumatatu
North corea hawana ujinga
 
Hilo la 2 ni wewe mswahili ndio ulilipanga mwenzio ana monday to sunday
monday ni start day and sunday ni siku ya mwisho ya juma!
Sasa kwanini wamerasimisha ikawa ni mfumo dunia nzima hii ni kuchanganyana
 
1. Hilo la saa ni kosa la wabongo wenyewe mimi siku nyingi nasema asilimia kubwa ya watanzania hawajui kusoma saa au wanakosea. Mshale ukiwa kwenye 3 hiyo ni saa 3 sio 9. Hakuna nchi yoyote ambayo wanasoma saa kinyumenyume kama Tanzania.

2 hili la siku pia sio kosa la wazungu sisi wenyewe ndio tumeamua weekend iwe jmos na jpili mbona nchi za kiislamu weekend ni alhamisi na ijumaa. Wengine ni ijumaa na jumamos.
 
Kama umesoma sayansi basi utaelewa kuna kitu kinaitwa SI unit (standard international units) kwenye mambo mbalimbali
Na kwa kuongezea "kimataifa" siku mpya Na tarehe ina anza saa sita usiku. Kwa mfumo wa AM /PM saa sita usiku ni 12am Na mfumo wa 24hrs saa sita usiku ni 00:00 hrs. Huu mfumo wa kiswahili siku au saa kuanza saa 12 alfajiri Na kuisha jua linapozama jioni haujakubaliwa maana nchini Iceland jua linaweza kuzama wakati mwingine saa nne usiku Na kuchomoza saa tisa usiku ! Kutegemea Na majira ya mwaka.

Yote hii ni kusaidia mfano safari za kimataifa za meli, ndege, treni n.k watu "wasichanganyikiwe " wakiwa Tanzania au Iceland kote watumie mfumo mmoja unaotambulika kimataifa.
 
Kwa waarabu wiki inaanzia jumapili
jumapoli-yaumul ahad,
jumamosi-yaumul sabat,
jumatatu-yamul ithain,
jumanne-yaumul thulathaa,
jumatano yaumul arbaa,
alhamis-yaumul khamiis na ijumaa ni yaumul jumaa..mapumziko kwao ni alhamim na ijumaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom