Mkuu hilo swali unaweza ukaona ni la kitoto lakini ,fikiria tena ?? Unazijua Western propaganda vizuri hivi unategemea nini kama kweli wametuchoka watanzania ? TISS watafanya nini ,?? Hapo kuna CIA,MI6,MOSAD nk wote kwa pamoja hao wanaungana
Sina tatizo na hilo amani tuliyonayo sio kwamba TISS ndio walio sababisha ikawepo ni Mungu tu na ashukururiwe kwa hilo ,hizo covert intelligence unazosema ningewaheshimu sana kama Twiga wanapanda ndege ya kijeshi ya Qatar ,makontena hayalipiwi kodi,meli ya pembe za ndovu zinakamatwa nje ya nchi ,kashfa za Richmond, escorow ,kama haya tu yamewashinda ni covert operations zipi za Mosad,CIA,MI6 na wenzake watazuia ???
Korea kaskazini wewe huijui.Hayo uliyoandika ni propaganda za magharibi.
Korea ni nchi pekee duniani ambako ni marufuku mwananchi kulipa kodi.Njia zote za uchumi na biashara zote kubwa ziko mikononi mwa serikali
Korea ni taifa ambalo linategemea mapato toka kwenye mashirika ya umma.Korea mashirika ya umma hufanya vizuri mno na faida zake ndizo hutumika kuendesha serikali.Korea ukiendesha shirika la umma kwa hasara au kulisababishia hasara wanakuua.Mashirika ya umma ndio engine ya uchumi wa korea.Sisi watanzania yalitushinda lakini tungekuwa tuliweza leo hii tungekuwa hatupigi goti kwa mtu wala kulalamika ajira hazipo.
Kwa hiyo siku hizi Zanzibar wanapokea Misaada moja kwa moja kutoka kwa hizo nchi wahisani bila kupitia Bara ????? Vyovyote vile swala la Zanzibar linatugusa wa Bara , kama waliweza kutuchimba mkwara kwa ishu ya Escorow watashindwa vipi kwa hili la Zanzibar ??Wanatakiwa wasome katiba ya jamhuri ya muungano na ile ya Zanzibar kablla ya kuchukua maamuzi yoyote.Huwezi kuiwekea sanctions Tanzania kwa sababu ya yanayoendelea ndani burundi!!
Zanzibar ni nchi huru yenye Raisi na sheria zake.Mambo ya uchaguzi wa Zanzibar si swala la Muungano.Wakicheza vibaya hapo hatima ya vitega uchumi vyao vilivyopo na wanavyotarajia kuwekeza vitaathirika.Mfano wakiweka vikwazo vya biashara kwa Tanzania mfano vya utalii.Watakao umia kwanza ni ndege zao zinazoleta mamilioni ya watalii wanaotembelea mbuga za ARUSHA,MANYARA,Mlima KILIMANJARO na Zanzibar,Halafu pia watakaoumia sana ni makampuni yanayoleta hao watalii ambayo yako nchini kwao,na watakaoumia zaidi ni wawekezaji wa kutoka nchi zao wenye mahoteli ya kitalii Arusha na Zanzibar.Kwa sekta hiyo tu wao ndio watakuwa waumiaji wakubwa.
Na Kwa Tanzania vikwazo hivyo vya biashara vya utalii vikiwekwa watu wa kwanza kuumia ni wa UKAWA wale wa KASKAZINI NA ZANZIBAR sababu wanategemea sana utalii kutoka kwa hao wazungu waweka vikwazo.
Usidhani vikwazo vinawekwa tu kwa sababu tu SEIF hamad KAWAOMBA wanaangalia Faida na hasara kwao za hivyo vikwazo.Wakiona watafaidika vikiwekwa wanaweka wakiona watapata hasara wakiweka hawaweki.Wanaangalia upande wao tu hawaangalii upande wa UKAWA au nani.
Nnakuunga mkono unaowasema. Mbona hawakuichoka ccm wakati walipokuwa wakifaidika kwa mali asili zetu. Ukweli wamemuona magufuli kaja na kasi nyengine ya kuweka watanzania mwanzo kuliko wao. Wanaona atawazibia ulaji wao. Hayo mataifa ya nje hayatoi msaada wa kitu.chochote kwa faida yetu bali za kwao binafsiKinachotakiwa ni UZALENDO kwa sisi kana Watanzania hii tabia ya kuwakumbatia Wazungu ndio inayosababisha ukosefu wa amani Duniani nchi nyingi ziliambiwa akitoka fulani maisha yao yatakuwa mazuri lakini mpaka leo ni maskini wa ajabu. Toka lini Mzungu akawa na huruma na mtu Mweusi? Kwa nini walilie CCM itoke? Hii nchi itaendelea kuwa chini ya mikono salama ya CCM mpaka pale kitakapopatikana chama mbadala cha Wazalendo na wafia nchi wengine kama CCM ndio tutairuhusu CCM ikajiunge na Malaika wengine Mbinguni.
Ivyo vyama vyenu vya kupiga dili na ukibaraka kwa wazungu vitaongoza baada ya sisi wazalendo wa nchi hii kufa kikabaki kizazi chenu cha mtoto wa kiume unapiga picha huku umebana ulimi.
Haha Kay unacheka nini ,mimi sina nalolijua kuhusu hao TISS ,hebu tufahamishe kidogoeti covert operations za TI whaat???
hiii hiiii hiii hiiii hii hii hiii hiiiii uncleben unaua mbavu zangu...uwiiiii
Haha Kay unacheka nini ,mimi sina nalolijua kuhusu hao TISS ,hebu tufahamishe kidogo
Mie mwanangu wa darasa la tatu hataki hata kusikia neno ccm
Kawaishe mirembe katakuwa kana kichaaa[/QUOT nilimpeleka wakampima akili wakamkuta mtoto genius hata class anafanya vizuri sana. Nakushauri umpeleke na wakwako huenda akawa na matatizo ya ubongo kwa kuipenda ccm
hawa jamaa ni kweli wakimuamulia mtu au nchi iingie kwenye dhiki ya haja wanaweza upuuzi wetu ndo kaburi letu na dharau zetu ndizo nguzo za hawa jamaa kutusambaratisha. Mkwamo wa kisiasa Zanzibar sio wakubezwa unahitajika umakini sana.wazungu waipige CCM tu
Hahaha sawa mamaangu nlifikiri unajua ndio maana unanicheka ,ila mleta mada atakua anawajua maana hilo la covert operations nimeliskia kwake ,kwani si kuna kiapo wanakula hivyo siri zitabakia tu kuwa siri ,tutaishia kuotea ila ukweli wanao waohahahahaha
ahaa uncleben, mie huwa nawasikiaga tu wanapokuwa wamefanya kazi ya kuwapa police intelligence kuhusu chadema...hahahaha, otherwise mie niko gizani tu kama wewe babaangu, labda swali ni kwanini sisi wakina yakhe hatuna tunalolijua kuhusu hii kitu inayojiita usalama wetu... au labda ni kwasababu hakuna lakujua zaidi ya hapo?
...mie uncleben nafikiri ni kutokujua kwangu ndio kunanifanya nicheke cheke tu...hahahahaha
He wewe unahakika na unacho sema kweli umesikiliza vizuri hotuba ya Mugabe ya Addis Hukusikia kikwete. Hii kali Mtu mzima wewe kweli? na Ulisikiliza hotuba yote? please tafakariNimeisikiliza hotuba ya Mugabe, hakulitaja jina la Kikwete na maana halisi si hiyo hapo juu ya kile Mugabe alichozungumza. Hata hivyo, kuna tofauti ya CCM na nchi tajwa hapo juu. CCM wanabadilisha uongozi wakati katika nchi tajwa hapo juu, viongozi ni wale wale.
Mkuu ccm ni zaidi ya utawala wa idi amini maana yule alikuwa anaua na watu wanajua lkn ccm wanaua akili za watu kwa kuwanyima elimu na kuwatawala kinyamaUtawala wa Dictator Mugabe ni better than U-Dictator wa CCM hapa
Hivi wewe unayejidai unashule wakati daily unashinda lumumba kudowea posho toka kwa wazito wenu alafu unawabeza wenzako wanaofanya kazi na kupata ridhiki halaliMkuu tupo tunaojiekewa wasikutishe hao vijana wa miaka ya 95+kichwani horobo shule hawakutaka wanafanya kazi ngumu mshahara mdogo afu wana wanawake wazee hasira zao zote wanamaluzia mitandaoni na vitecno vyao vya bure.
Mkuu hapa jambo muhimu ni kujiuliza je hao libya walizaliwa na hayo machafuko?au machafuko yalitokea hewani tu na kuanza kupigana?jibu ni hapana kuna chanzo na chanzo kilianza kama hapa kwetu,lazima ujue kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha,serikali ikizidisha dharau sana raia wake matokeo yake inakuwa mbaya sana.Pamoja na kuwa kila mtu ameichoka CCM kwa kkiwango kikubwa lakini hayo unayoyataka yatokee ni ya hatari zaidi....amani ikipotea yatakuwa ni majuto makuu siyo tu kwako bali mpaka kwa vizazi vyako......bado tuna nafasi ya kurekebisha mambo katika nchi katika njia ya amani kuliko kuanzisha fujo ambazo madhara yake ni makubwa kuliko unavyodhani......
Kwa kiasi kikubwa sana raia wa Libya wapo kwenye majuto makuu hata yale madogo waliyokuwa wakiyadharau sasa hayapatikani....ni muendelezo wa mauaji na kila aina ya unyama...