Wazungu waliona mbali sana!

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
wanabodi iwe nanyi!

zamani kulikuwa na kitabu kimoja chenye simulizi ya kitoto lakini ilibeba ujumbe muhimu hasa kwa waafrika.simulizi ya Yohana mjinga. nitawasimulia kidogo ili ambao hawjawahi kusoma wapate kuijua ndio niende kuileta kwenye maisha yetu ya sasa na wasomi tulio nao kazini.

Yohana mjinga alikuwa mjinga kweli! siku moja wakati anatoka shule alifika kondeni akamuona ndege mzuri na mkubwa kiasi, na yeye akawaza nikimpiga yule atafaa kwa kitoweo.bila kutafakari sana akaamua kumlenga ili ampige, kumbe mkononi alishika sarafu yenye thamani.akamrushia yule ndege,akamkosa.baadae agagundua kuwa alitumia sarafu badala ya jiwe! akarudi nyumbani yu mwenye hasira kali.Baba yake akamuuliza kulikoni? akajibu, nimepoteza sarafu yangu yenye thamani nilidhani nimeshika jiwe nikamrushia ndege, nimemkosa na sarafu imepotea.Baba yake akamwambia siku nyingine ukipata kitu weka mfukoni.

Siku iliyo fuata kule shule akapewa maziwa, akakumbuka kuwa alishauriwa akipata kitu akiweke mfukoni, akaweka! yakamwagika na kaputura ikalowa sana.Akarudi nyumbani, babake akamuuliza mbona hivyo? Akajibu uliniambia nikipata kitu niweke mfukoni, nimepewa maziwa nikaweka yamemwagika yote na kaputura yangu imelowa vibaya. Bba yake akamwambia, siku nyingine ukipata kitu, funga kamba uvute!

Siku iliyo fuata akapew nyama kilo tatu apeleke nyumbani. akakumbuka ushauri ule alio pewa. Akachukua kamba akaifunga nyama vizuri akawa inaiburuta kwenda nayo nyumbani, hata mbwa walipo ona wakaishambulia na kuila yote!akarudi nyumbani yu mwenye hasira kali,baba yake akamuuliza nini tena? akasema uliniambia nikipata kitu nifunge kamba kisha nikivute, nimepewa nya kilo tatu, hata nilipo ifunga kamba na kuiburuza mbwa wameiona wakala yote nimebaki na hii kamba! baba yake akamwambia siku nyingi ukipata kitu jitwishe!

Sku iliyo fuata akapewa punda.......

huyo alikuwa Yohana mjinga. Je ujinga umeisha miongoni mwetu? la hasha!
Hebu angalia watendaji serikalini walivyo waoga. utadhani Magufuli amesema wasifikiri kila kitu wanamsubiri awaelekeze! usafi wa miji hawjauwekea mkakati endelevu wanataka Rais aje awaelekeze tena namna ya kufanya usafi ni jambo endelevu.

Hakuna kiongozi anae kuja na ubunifu mwingine, wote wanamsubiri Magufuli abuni kitu,hawafikiri kama Yohana.Elimu bure imesababisha wanafunzi wengi kuandikishwa hivyo kuhitaji vyumba vingi vya madarasa, kuwashirikisha wazazi na wadau wa maendeleo wachangie watu wanaogopa eti watafukuzwa!!Tunahitaji kutumia akili kwa kila jambo ili kupambana na changamoto mpya.Au kiongozi anamsimamisha AFISAELIMU Kazi kwa kuruhusu wazazi wachangie ujenzi wa choo kilicho poromoka ghafla, huko ni kutumia akili kweli? Alamsiki.
 
Mkuu hiyo hadithi ya Yohana mjinga naomba kama kuna kitabu chake unitajie wapi nitakipata
hadithi nzuri sana nyakati hizi
 
Mbona Serikali ilishaweka kuwa siku ya usafi kwa Tanzania nzima ni jumamosi ya mwisho ya kila mwezi! Mikoani utanazingatia hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom