Wazungu na matajiri wanawezaje kula hivi?

Wazungu na matajiri wanawezaje kula hivi?

Inategemea na mazingira.
Kwa siku za hivi karibuni asubuhi nakula chakula Cha nguvu, mchana nakula wastani, usiku naweza nikanywa Juice fulani hivi tu au chai na nikalala safi.
Hii Kwa siku za zamani sikuweza, ilikuwa lazima usiku Nile kama nataka kuhama 🤣
 
Kiukweli najiuliza matajiri na wazungu wamewezaje kula matunda tu kama msosi wa jumla hasa usiku?

Yaani eti anakula matunda tu analala!

Nikaona isiwe ishu, acha name nijaribu.
Saa 2 nikala matunda nikaelekea kulala.

Yaani usiku nipo kitandani nasikia watu ndotoni wanasema RIP. Nikaamka nikaanza kutazama bati, mpaka kufikia kumkosoa fundi aliyepaua.

Wadudu nao tumboni wanaulizana huyu jamaa leo vipi? Hali ama?

Nikaona isiwe kesi nisije pelekwa hospital bure kutundikiwa dripu wakadhani mie mgonjwa. Ikabidi tuu nisonge ugali usiku.

Najiuliza hawa watu tajwa wanaishije kwa kula hivyo vijitunda kisha wanalala vizuri tu?

Nimekoma aseeh
Kula hivyo ni kitu cha kujizoesha kwa muda nrefu, si jambo la kufanya mara moja. Na wengine wamezoeshwa tangu utoto.

Ukizoea kula kiasi fulani, vyakula fulani, muda fulani, kubadili inahitaji muda, hubadiliki mara moja.
 
Inawezekana, siyo wazungu tu. Kupanga ni kuchagua. Na kuishi maisha mazuri siyo mpaka uwe tajiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom