Wazo: Rais aongezewe mshahara

Yusomwasha

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
2,092
838
Wakuu,

Naona rais aongezewe mshahara hata angalau milioni 30 kwa mwezi kuliko kulipwa milioni 9.5 kwa mwezi wakati ana majukumu mazito hivyo.
 
Naungana na wewe kwa sababu kuna baadhi ya wenyeviti wa vyama vya upinzani wanachukua mshahara mkubwa tu na hakuna chochote wanachokifanya zaidi ya kubwabwaja bwabwaja tu
 
Naungana na wewe kwa sababu kuna baadhi ya wenyeviti wa vyama vya upinzani wanachukua mshahara mkubwa tu na hakuna chochote wanachokifanya zaidi ya kubwabwaja bwabwaja tu
Tuwekee mshahara wa mwenyekiti wa chama tawala tuone kama mshahara wake ni mdogo kuliko hao wa upinzani isitoshe JPM amechaguliwa kwaajili ya kuongoza nchi tofauti na uongozi wa kichama ambao anaadhibiwa na wanchama pekee
 
wa chama tawala hata kama uwe ni mkubwa ni haki yake kwa sababu chama tawala ni means za kupata pesa kwa maana ya kuwa na miradi mbalimbali ya chama

sasa vyama vya upinzani mara nyingi inategemea uchangiaji kutoka kwa wanachama na wafuasi bila kusahau mashabiki sasa nitawaona watu wa ajabu kama watakuwa wamejiwekea mishahara mikubwa na ya mamilioni

ndio maana tunasema kama wana ubavu waweke tujiridhishe
 
wakuu naona raisi aongezewe mshahara hata angalau milioni 30 kwa mwezi kuliko kulipwa milioni 9.5 kwa mwezi wakati ana majukumu mazito hivyo
Zakumuongeza zipo escrow zikifuatiliwa zile rais itabidi aongezewe Mshahara kama itashindikana basi mheshimiwa rais atuvumilie tu mana na sisi pia huku uswahilini tuna njaa na hamna anaetupa chakula tunapambana lakini mafanikio bado madogo

Elimu ndogo.com
""""""""""""""""""""""""""""""""""
 
Naungana na wewe kwa sababu kuna baadhi ya wenyeviti wa vyama vya upinzani wanachukua mshahara mkubwa tu na hakuna chochote wanachokifanya zaidi ya kubwabwaja bwabwaja tu

Kwahiyo mshahara wa mwenyekiti wa upinzani ndio standard za mshahara wa rais? Huyo rais ni ,wenyekiti pia?
 
mshahara wa raisi milion tisa sidhan kama kuna usahihi labda niione salary slip. haiwezekani mla maharagwe wa shirika la serikali alipwe milion zaid ya 35 halaf mkuu wa nchi eti milioni 9!
 
Wazo zuri aongezewe ili asijefikiria kuanzisha business akiwa Ikulu kama baadhi ya watangulizi wake.
 
Mnataka aongezewe ili azipeleke wapi?? Kula bureeee....kulala bureeee.... matibabu bureeee....umeme bureeee....maji bureeee..... usafiri bureeeee....... bado tu mnataka aongezewe????? Muwe na huruma wakati mwingine. Au mnataka na yeye aishi zaidi ya malaika??? Wote tuishi kama mashetani hii nchi iwe jehanamu sasa.
 
Wakuu,

Naona rais aongezewe mshahara hata angalau milioni 30 kwa mwezi kuliko kulipwa milioni 9.5 kwa mwezi wakati ana majukumu mazito hivyo.
Mkuu... Ilikuwa tarehe 1/4/2016...April fool.... Sitaki kuamini na wewe umekuwa mjinga.... Pamoja na wote walio kuunga mkono kwenye hii hoja..
 
Back
Top Bottom